Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Katika miaka ambayo nimefanya ATCL katika 18 sijawahi kuona kampuni ilivyopata hasara kama wakati huu,,ndugu zangu hasa wale wlipa kodi nimona vyema tuichambue hizi kashfa nani atabeba lawama ATCL ikifa??????SA TENA?MMhh,wanablogu kampuni hii kila mmoja alisikia kilio cha watu je kwa haya mambo yafuatayo tutafika ???

1)MAHUJAJI WAMETOA HELA KWENDA HIJA,,,LAWAMA HIZI TUMTUPIE MWENYEKITI WA B.....AMBAE BAADA YA KUULIZA SANA INASEMEKANA
HATA KITENGO HUSIKA HAKIJUI NINI KINAENDELEA;;;INA MAANA HII ILIKUWA NI DILI YA WATU AU??NA WAKINA NANI WALIOHUSIKA,,MAHUJAJI HIVI SASA WANALALA MAHOTELINI NA KILA HOTELI KWA SIKU SI CHINI YA SH 40,000 NA ATALIPA HIZI,ABIRIA WAKO 1000,JE 40,000*1000 KWA SIKU TANO NI SH NGAPI??

2)MAHUJAJI WAMETOA USD900 NA HABARI KAMILI WENYE NDEGE WANATAKA 1200 USD JE HIZI USD 300 ZINATOKEA KWENYE KAMPUNI HII HASARA ABEBESHWE NANI?.
 
3)Je hawa wahusika ni nani ..tunaomba waheshimiwa na wanablogu tusaidiane jamaninhili ni shirika letu leo likifa ni aibu kwa kila mtanzania,,

4)Hawa wakubwa wanaoendelea kusafiri kila siku wakila hela za kampuni wana lengo gani kwa watoto wetu wa baadae??watanzania tuwe macho jamani hili swala ni kudhalilisha sisi waislamu maana kesho ndio mwisho na je watalipwa na nini jamani???

wahusik tunaomba mtujulishe lengo lenu lilikuwa nini nini??au ndio ten percent hii????TAKUKURU mzee HOSEA TUNAOMBA ULIFWATILE HILI SWALA TAFADHALI KABLA HAWAJATUMALIZA INAONEKANA WANA NIA MBAYA NA KAMPUNI,,JE TUTAFIKA LIPI BORA SOUTHAFRICA AIRWAYS AU TUBAKI WENYEWE TUJIUE WENYEWE???? KWENU WANA BLOGU
 
Where is the so called "Muslim brotherhood" in Dar es Salaam??Nilishangaa kuona jana kwenye luninga eti " Mahujaji wamenalala na kuswali airport! Aibu! Wako wapi Waislamu wa Dar es Salaam?
Je imeshindikana kuwasitiri hawa ndugu zetu mahujaji alau wapate sehemu decent ya kulala na kuswali?Kwa mabiashara, majumba na mipesa mliyokuwa nayo. Je imeshindikana hata mkachanga hela watu hawa wakatafutiwa guest iliyoko karibu na airport waweze kuswali na kulala vizuri??
Uko wapi umoja wa kiislam hapa???
Mimi ni Mkristo aka "mgalatia" in JF nina uwezo wa kumchukua mama mmoja aje akae kwangu hadi hapo atakapopata usafiri.
Mwenye info naomba anitumie kwenye PM.
 
..kwani,nani anahusika na kuwepo kwao hapo?yaani,aliyewaandalia/kutowaandalia hiyo safari?

..hawa hawana uhusiano na bakwata?na je?hawana ndugu dar?au wameamua kukaa hapo uwanjani kwasababu wanazozijua?labda kushinikiza huo usafiri upatikane?

..si lazima waende guest,misikiti ipo mingi,wanaweza pata huduma huko!

..anyways,si jambo zuri walilofanyiwa na yeyote aliyehusika!
 
DSL liliotokea limetokea. Sijui ni nani aliyekosea. Concern yangu hapa ni wao "waislamu" wenzetu kuishi airport wakati Waislamu wa Dar wapo na mijumba mikubwa....migari...mipesa...
 
ATC aibu!

2007-12-10 17:16:36
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Shirika la Ndege nchini, ATC limelaumiwa kwa kufanya kitendo cha aibu ya mwaka kwa kuwasotesha kwa wiki nzima mahujaji zaidi ya 300 ambao wameshakamilisha taratibu zote za safari.

Aidha, Shirika hilo limetakiwa kuwalipa fidia mahujaji hao kutokana na gharama walizoingia mara kadhaa wakati wakifika uwanjani hapo ili wasafiri, na kisha kuishiwa kupewa kauli za ‘njooni kesho, rudini kesho kutwa.

Aliyetoa kauli hiyo ya kulaani kitendo cha ATC na kukiita kuwa ni cha aibu ni Kiongozi wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Ni aibu na fedheha... Serikali inapaswa kuwajibika kwa sababu, kama ndege iliyotegemewa imeharibika, ni yenyewe ndiyo inayopaswa kuingilia kati na kuokoa adha wanayoipata waisilam hawa ambao wameshalipia kila kitu, akasema Sheikh Ponda.

Kama si Serikali kuingilia, nani sasa atakayewezesha mahujaji hawa kulipia gharama kubwa walizoingia kwa kukaa jijini zaidi ya wiki sasa, wakiishia kila siku kusoteshwa Airport kwa kuahidiwa safari?

Ni vyema gharama hizi zikafidiwa na wahusika wanaotoa taarifa zisizokuwa na ukweli, tena zaidi ya mara moja, wawajibishwe, akaongeza Sheikh Ponda.

Aidha, katika orodha ya mahujaji waliosoteshwa zaidi ya wiki moja sasa pale katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, inaelezwa yumo baba mkwe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Jakaya Kikwete na mashemeji zake kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ni kwamba, kama walivyo mahujaji wengine, ba`mkwe huyo mzaa chema wa Rais Kikwete aitwaye Mzee Rashid Yusuph Mkwachu, ametaabika mno na njoo kesho ya ATC.

Pia waliokumbwa na adha hiyo inayodaiwa kusababishwa na ubovu wa ndege iliyotegemewa kusafirisha mahujaji hao huku zikitolewa ahadi hewa za kila mara ni shemejie Rais Kikwete aitwaye Mwanakombo Bakari na ndugu wengine ambao ni Hassan Mohamed na Jamillah Omar.

Imedaiwa kuwa mahujaji hao walikuwa wasafirishwe wiki iliyopita na ATC, lakini wakaishia kurudishwa na kuahidiwa kila mara kuwa watasafirishwa, lakini bila ya mafanikio.

Jana usiku, imeelezwa na Sheikh Ponda kuwa taarifa walizopelekewa na Mwenyekiti wa Bodi ya ATC ni kwamba sasa, safari hiyo iliyoahirishwa tena jana, itakuwa leo jioni.

Here is the trueth
 
DSL liliotokea limetokea. Sijui ni nani aliyekosea. Concern yangu hapa ni wao "waislamu" wenzetu kuishi airport wakati Waislamu wa Dar wapo na mijumba mikubwa....migari...mipesa...

..mama,

..hili jambo si rahisi hivyo,kuna fitna kubwa kwenye hilo swala,subiri tutapata nyeti za kilichojiri!

..kuna ubabaishaji mkubwa umefanywa!by all accounts!
 
Where is the so called "Muslim brotherhood" in Dar es Salaam??Nilishangaa kuona jana kwenye luninga eti " Mahujaji wamenalala na kuswali airport! Aibu! Wako wapi Waislamu wa Dar es Salaam?
Je imeshindikana kuwasitiri hawa ndugu zetu mahujaji alau wapate sehemu decent ya kulala na kuswali?Kwa mabiashara, majumba na mipesa mliyokuwa nayo. Je imeshindikana hata mkachanga hela watu hawa wakatafutiwa guest iliyoko karibu na airport waweze kuswali na kulala vizuri??
Uko wapi umoja wa kiislam hapa???
Mimi ni Mkristo aka "mgalatia" in JF nina uwezo wa kumchukua mama mmoja aje akae kwangu hadi hapo atakapopata usafiri.
Mwenye info naomba anitumie kwenye PM.

Hapana Mzee, kuwaacha hawa watu pale airport ni muhimu na wao hawataki pia kuondoka pale na kwenda gesti, wao wametoka mikoani kote ili waende Mecca, sasa kuja kuishia gesti Darisalama itakuwa ni kitu ambacho hakieleweki.

Kubaki pale kunatoa ishara kubwa na kuwaanika vilivyo watu walioboronga katika huo mpango wa kwenda Mecca, yaani kubaki pale is more effective kuliko hata kushtaki mahakamani.

Sasa jamani waandishi wetu wa habari, tuchambulieni basi mchakato huo wa kupeleka watu kuhiji ukoje? Nani anahusika na nini? nani alitakiwa ahakikishe ndege inakuja? alijuaje hao watu ni watu waaminifu? alifuatilia kuchunguza ni ndege ngapi na huduma zipi wameshawahi kutoa? au ndio mambo yale yale ya kibongobongo kama jamaa wale waliotakiwa kutuletea umeme na kuipa kampuni kazi wakati kampuni yenyewe haijawahi kufanya kazi hizo ilimradi tu wahongane.

Sasa Emirates inajulikana kuwa ni shirika mahiri na la uhakika na linatoa hizi huduma tangu miaka nenda rudi bila uzembe, ni kigezo gani alichukua huyu mtu kuipa kazi shirika ambalo halina reputation? Hao ATC kutaka kukodi ndege kwa sijui kishirika gani huko saudia ambacho hata hakina jina manake nini? ndio mambo hayo hayo ya mishen town kupeana peana tu tenda kiholela, si ajabu mtu aliyepewa jukumu la kutoa tenda alipigiana simu na mshirika wake wakaambiana aise kuna dili apa wakapeana bila kujali kuwa cha muhimu si ushirika, bali uwezo wa ku-deliver.
 
Just another "Richmondinization" of serious and important business,watu tayari wameshajinyima hicho kidogo walichokuwa nacho iliu waende kutimiza nguzo ya imani yao,then some "smart" dumbasses come along and promise them "kuwaunganishia usafiri" a kwenda kuhiji Makka on the pretext kwamba "aliyetuomba tusafiri na ATC ni Mustapha Nyang'anyi ambaye ni Muislamu mwenzetu!" (kulingana na TanzaniaDaima la jana)yaani kwa Nyang'anyi kuwa Muislamu ni kigezo tosha cha waandaaji wa safari kutowapa tender hiyo Emirates ambao ni more than reliable!!

Really tanzania has a long way to go...fananisha hii na ile tender ya ujenzi wa barabara ya Sam Nujoma (kilometa 4 inayojemgwa kwa miaka 2 sasa),barabara za Dodoma-Manyoni,Singida-Shelui,huko kusini na baba lao RICHMOND...ni usanii tu mpaka kwenye imani,mtaona keshokutwa mtu ananyanyua kigorofs chake Mbezi au Masaki na kuagiza Vogue na kupeleka watoto "Saint Ramadhani" kusoma...
 
Hapa mwenye kubeba jukumu la kuwahudumia na kuwafidia hasara zote ni kampuni inayohusika na kuwasafirisha, na si waislamu wenzao. Sijui kilichotokea huko ATC hadi wakashindwa hii kazi, lakini hiyo ATC ndiyo tabia yao ya miaka mingi, kumbe hawajabadilika. Zamani tuliwaita "Any Time Cancelled", maana walikuwa na tabia ya kufuta safari dakika za mwisho wakati abiria wamesha-check in na kuagana na wasindikizaji! Ndipo wakaandaa kipindi cha redio kama mnakumbuka, cha kuwataarifu abiria usiku unaotangulia siku ya safari kama ndege itakuwapo au la, hata hivyo waliendelea kuwa "ATC". Hii hasara na gharama zote zinapaswa kufidiwa na ATC, na wala si na sympathisers wa mahujaji, na si hivyo tu, wanawajibika kuwasafirisha hadi Mecca kama walivyokubaliana katika tiketi walizonazo. Kuna sheria ya kimataifa inayozungumzia suala hili kinagaubaga (Warsaw Convention 1929 na Montreal Convention 1999) kuhusu haki na wajibu wa wasafirishaji na abiria kwa ndege.
 
DSL liliotokea limetokea. Sijui ni nani aliyekosea. Concern yangu hapa ni wao "waislamu" wenzetu kuishi airport wakati Waislamu wa Dar wapo na mijumba mikubwa....migari...mipesa...

Kwa maoni yangu wenye wajibu wa kwanza kuwasaidia wasafiri hawa ni ATC na siyo Waislam. Ninavyofahamu mimi Waislamu wengi kama walivyo Watanzania wengi hali zao kifedha si nzuri, ukiondoa waislamu wahindi ambao baadhi yao wana hali nzuri. Wengi wanaishi katika maisha ya dhiki hivyo kuongeza hata mmoja itakuwa ni mzigo mkubwa sana. Hivyo wa kulaumiwa hapa si Waislam wa Dar, bali ni ATC.
 
Uongozi wa hii nchi yetu kweli umeoza...yaani kwani hawa mahujaji walikuwa wanaenda bure?? Si wamelipia hawa; tena ni wengi zaidi ya 900..!!!

Nashangaa hakuna kiongozi yoyote wa ATC au Wizara ya Usafiri aliyekuja kuomba rathi Watanzania. Raia wenzetu zaidi ya 900 wanalala Uwanja wa Ndege kwa zaidi ya wiki na hakuna mtu anayeulizwa maswali ya msingi mbele ya wananchi.

Ningekuwa mimi ni mmoja wao kama nina uwezo tiketi ya kurudi ningebadilisha maana hawa ATC hawakawii kukuacha Macca.

Waislam wasipoandamana hata kwa hili; basi mimi nitajiuliza maswali magumu sana..!!

Kalaghabaho
 
Hivi lile dege alilonunua Chez Nkapa (hadi tukaambiwa ikibidi kula nyasi tutakula, shurti dege linunuliwe) haliwezi kuwawahisha hao mahujaji huko Mecca na kuwaondolea hii adha? Maana kodi yao pia ilitumika kununua dege hilo. Mlio karibu na JK hebu mshaurini alitoe hilo dege lifanye angao jambo moja la kheri, pengine italiondolea nuksi inayotokana na malalamiko yaliyogubika ununuzi wake. Mawazo yangu tu.
 
Ile ndege inachukua watu 19, ATC walitakiwa wawafanyie Arraengements za safari au sehemu ya kukaa lakini kama kawaida yetu Tanzania mashirika mengi hayajali wateja.
 
Ile ndege inachukua watu 19, ATC walitakiwa wawafanyie Arraengements za safari au sehemu ya kukaa lakini kama kawaida yetu Tanzania mashirika mengi hayajali wateja.

Sasa iliyobaki ni sisi wateja kuwafundisha haya makampuni jinsi ya kutujali. Yaani kuanzia leo mtu akisafiri inatakiwa achukue ndege nyingine zote isipokuwa ATC.

Nchi zilizoendelea ukizembea tu hakuna mteja atakayekubali kuburuzwa hapo your competitors ujue washachukua wateja, hii inasaidia sana kuyafanya makampuni yaboreshe huduma zao, sasa kama wateja tutaendelea kusafiri na ATC that would mean tuna-reward uzembe kwa hiyo wala tusilaumu viongozi wazembe wasipofukuzwa.

ATC ikafilie mbali hapendwi mtu wala shirika ni huduma ndio inapendwa.
 
Ila ATC wamezidi nao wanapenda kutreat wateja kama wanasafiri bure. Ila hiki kitendo kinasikitisha sana hawa mahujaji hawakuchelewa? Hivi ATC haina ushirikiano na mashirika mengine? maana najua kama shirika moja likishindwa kukusafirisha wanakuweka kwenye next available flight(wao wanalipia the difference).
 
Sio ATC tu yani system nzima kuanzia juu hadi unyayoni CHOKA CHOKA CHOKA CHOKAMBAYA.

kwa maana nyingine ni FISADI FISADI kwenda mbele, ndio maana hata JK anapatwa na kigugumizi kubadilisha safu Lake maana aliyopo ni fisadi afadhali kuliko ajae.

Hii naifananisha na jamaa mmjoja kule kijijini kwetu baada ya MAMASUP kumtupa(kumtosa) akaonelea ni vyema ajitoe uhai wake na kwa kutekeleza hilo alichukua kamba yake iliyosokotwa kwa nyuzi za mkonge na kuelekea porini ili aitekeleze adhima yake.

Na alipokuwa pori kwa pori mara vapu JOKA HILO KOBOKO ana kwa ana na marehem tarajiwa. duuuuu!!!! jamaa badala ya kumvaa yule koboko ili adhima yake itekelezwe na koboko lile ,yeye alichokifanya ni kutimua mbio kujiepusha na balaa la koboko yule.

Watu wakabaki mdomo wazi na ikabidi wamhoji mwezetu kulikoni tena?? naye akajibu VIFO VINGINE VINATISHA.
 
Hapa mwenye kubeba jukumu la kuwahudumia na kuwafidia hasara zote ni kampuni inayohusika na kuwasafirisha, na si waislamu wenzao. Sijui kilichotokea huko ATC hadi wakashindwa hii kazi, lakini hiyo ATC ndiyo tabia yao ya miaka mingi, kumbe hawajabadilika. Zamani tuliwaita "Any Time Cancelled", maana walikuwa na tabia ya kufuta safari dakika za mwisho wakati abiria wamesha-check in na kuagana na wasindikizaji! Ndipo wakaandaa kipindi cha redio kama mnakumbuka, cha kuwataarifu abiria usiku unaotangulia siku ya safari kama ndege itakuwapo au la, hata hivyo waliendelea kuwa "ATC"

Nadhani nitakubaliana na wewe kwenye hili la "hatujui kilichotekea ATC" kutoweza kukamilisha safari kama ilivyopangwa awali. Lakini hili la tabia yao, naona kidogo tunakwenda above ourselves. Cancellation zinatokea na saa nyingine ni reasons ambazo ziko beyond their capabilities. Inaweza kuwa kweli ndege imeharibika and what not; mbona mambo ya kawaida sana haya, the whole world does this, all the time! Ndio maana mnaambiwa contact your airline before hujaenda airport. Lakini kama kawaida binaadamu tunachukua risk ya kwenda airport. Tuwape ATC benefit of doubt! In fact kama cancellation imetokea ambayo sio fault ya shirika la ndege, as a customer, it is your responsibility to come up with plan B.
 
Back
Top Bottom