Sakata la mahindi litaondoka na serikali?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Kumekuwa na kelele sana juu ya anguko la bei ya mahindi kote nchini. Kiasi ambacho imebidi CCM iingilie kati. Nimewaona wabunge wote hasa wa CCM wakionyesha kutorodhishwa kwao jinsi NFRA inavyonunua mahindi toka kwa wakulima.

Ongezekeo hili la wingi wa mahindi ni mwitikio wa wakulima kwani wakati wa CORONA wakulima waliambiwa walime kwa wingi kwani baadhi ya mataifa yanaweza kukumbwa na baa la njaa kwani kujifungia kwao ndani wengi wao walishindwa kulima kwa wakati na kwa ufasaha.

Kwa kuwa CCM ni chama na Wakulima na wafanyakazi hakiwezi kujisikia furaha kwa kuwaona wakulima wakipata taabu.

Je, ni kutokana na ukaribu huo wa CCM na wakulima serikali inaweza undwa upya?

Ni jambo la kusubiri kuona mambo yataendaje ikizingatiwa kuwa mikoa inayolima mahindi kwa wingi kama Ruvuma, Iringa, Njombe na Katavi ndiko waliko wana CCM wasiobadilika hivyo wana mchango sana kwa CCM kuendelea kuwa madarakani.
 
Mbolea laki moja halafu mahindi gunia elfu 25

Eka moja inatoa gunia 8 na eka moja inalimwa kwa kutumia mbolea kg 100 ambazoni laki mbili.

Hii maana yake ili uweze kulima eka lazima uuze gunia 8 kwa laki 2

Bado pesa ya kukodi shamba elfu 50.

Bado kulima na kupalilia Kama laki na nusu hivi.

Inaelekea kumaliza kulima eka moja ni Kama laki tano.

Hapa tumepigwa .
 
Wakati mamlaka ya hali ya hewa wana project hali mbaya ya hewa iliyo na upungufu mkubwa wa mvua ambayo itapelekea uhaba mkubwa wa mavuno, serikali haitoi pesa ya kununua na kuhifadhi mahindi kutoka kwa wakulima ili wanunue mafuta ya VIIEITE.....hili linawezekana bongoland tu.
 
Kumekuwa na kelele sana juu ya anguko la bei ya mahindi kote nchini. Kiasi ambacho imebidi CCM iingilie kati. Nimewaona wabunge wote hasa wa CCM wakionyesha kutorodhishwa kwao jinsi NFRA inavyonunua mahindi toka kwa wakulima...
Rais wa Kenya mh.Uhuru Kenyatta ametangaza JANGA la njaa kaunti za Isiolo ,Garisa na kwengineko linalowakumba wananchi takribani milioni 2 na ushee.

Hayati JPM alituambia TULIME VYEMA KIPINDI CHA CORONA ili tuje KUWAUZIA MAZAO WENGINE.

Ndicho kipindi chenyewe hiki.

RIP Hayati Rais Magufuli ,amen🙏

#SerikaliYaCCMNiMakini
#SiempreChifuHangaya
#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
Kumekuwa na kelele sana juu ya anguko la bei ya mahindi kote nchini. Kiasi ambacho imebidi CCM iingilie kati. Nimewaona wabunge wote hasa wa CCM wakionyesha kutorodhishwa kwao jinsi NFRA inavyonunua mahindi toka kwa wakulima...
Wasomi wetu tupeni mawazo tufanyeje na mahindi yetu.

Tusisukumie serikari kununua tu mahindi.

Njooni na majibu tuyafanyeje hayo mahindi yasiharibike na wakulima waendelee kuyazalisha
 
Mbolea laki moja halafu mahindi gunia elfu 25

Eka moja inatoa gunia 8 na eka moja inalimwa kwa kutumia mbolea kg 100 ambazoni laki mbili
Kilimo chetu cha kijamaa hakitatufikisha popote. Kitatutia umaskini na nchi ipo siku itaanguka kwenye njaa. Wanaolisha nchi ni wazee vijijini. Matajiri wakubwa na vijana hawataki kulima, kwanini?

Sababu kilimo hakilipi. Kwanini hakilipi? Sababu serikali inafunga mipaka inapojisikia, inawapangia watu kwa kuuza mazao yao! Matokeo yake bei inakuwa si rafiki, hairudishi hata gharama. Hakuna atakayelima kwa mazingira hayo.

Tunakoenda kwa bei hizo hakuna atakayelima ili kuuza. Watu watalima kiduchu tu ya kula. Nchi itaingia kwenye njaa.

Cha kufanya, serikali iruhusu mtu auze mahindi yake popote anapotaka. Itungwe sheria kuwa serikali hairuhusiwi kumzuia mtu kuuza mazao yake atakako. Mtu alime akiwa na uhakika wa soko zuri South Sudan, Congo nk. Hapo ndipo mkulima atachomoka na uwekezaji mkubwa utafanyika kwenye kilimo.
 
Mbolea laki moja halafu mahindi gunia elfu 25

Eka moja inatoa gunia 8 na eka moja inalimwa kwa kutumia mbolea kg 100 ambazoni laki mbili...
Nakushauri, mtembelee sumry akuambie anapataje faida,
 
Wakati mamlaka ya hali ya hewa wana project hali mbaya ya hewa iliyo na upungufu mkubwa wa mvua ambayo itapelekea uhaba mkubwa wa mavuno, serikali haitoi pesa ya kununua na kuhifadhi mahindi kutoka kwa wakulima ili wanunue mafuta ya VIIEITE.....hili linawezekana bongoland tu.
Pesa zinatumika kushuti filamu ya mamaa jamaa, tuwe wapole nchi inabrandiwa ili wazungu watuletee pesaa
 
Mchi jirani wanalia na ukame huko hebu tupite nduki na hiyo fursa.
 
Tatizo la soko la mazao ya wakulima hapa Tanzania,ni kubwa na Serikali haiwezi kukwepa lawama.Pawe na uratibu Kati ya wizara za kilimo na viwanda na Biashara,hizi wizara zinategemeana.

Hizi wizara zinaongozwa Maprofesa ambao wamebobea kwenye nadharia Sana, lakini hawana uzoefu wa kinachoendelea huko kwenye field,kwa kufanya wao wenyewe binafsi.

Bodi ya Biashara za nje IPO kama haipo, watendaji wake wanafanya kazi kisiasa na wanawekwa kwa kujuana. Wahusika wajitafakari wakulima wanavunjika moyo,wanapojitahidi kuongeza uzalishaji wa mazao, lakini wanakosa masoko na hawana maghala ya kuhifadhia mazao yao.
 
Back
Top Bottom