Sakata la madini: Tundu Lissu ategua kitendawili

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
541
Ifahamike kwamba mapigano makubwa kati ya serikali na upinzani juu ya sakata la madini/mirabaha/mikataba lilianzishwa siku nyingi sana bungeni, mwanzo kabisa alikua mh Mnyika akiwa waziri kivuli wa madini, Zitto kabwe na kwenye mambo ya mikataba Tundu Lisu alikua mwiba mkali sana.

Sasa hatimaye kitendawili kimeteguliwa alichokua anakipigania na matokeo ya tume ya madini vimeenda sawa.

Tazama hapa.

 
Wabunge walipewa. Kumbukumbu zenu vipi? Kamati ya mbunge walishafanya uchunguzi. Na Kuna kamati ya JK ikiwa Na ZITTO. Akuyaona ujinga huu
 
Ifahamike kwamba mapigano makubwa kati ya serikali na upinzani juu ya sakata la madini/mirabaha/mikataba lilianzishwa siku nyingi sana bungeni, mwanzo kabisa alikua mh mnyika akiwa waziri kivuli wa madini, zitto kabwe na kwenye mambo ya mikataba tundu lisu alikua mwiba mkali sana. sasa hatimae kitendawili kimeteguliwa alichokua anakipigania na matokeo ya tume ya madini vimeenda sawa. tizama hapa.


Daaaa,huyu Tundu Lissu ni mtu makini. Yale aliyoyasema huko nyuma kuhusu madini ndo yanatimia leo.
 
Majizi chadema kwa kujipendekeza hawajambo
Bila kujali mambo ya uvyama,kama Wabunge wa CCM wataanza kuwa makini,mambo mengi ya hovyo yasingetokea. Kumbuka hiyo video Clip ni ya muda mrefu,lakini leo yanatimia.Sasa mchangiaji imekuuma kuona kwamba aliyoyasema Tundu Lissu zamani leo yanatimia. Kwa ushabiki wako ukadhani Tundu Lissu aliongea leo,kumbe ni muda mrefu. Tukubali tu kuwa katika Taifa,watu kama Tundu Lissu,JPM tunatakiwa tuwe nao kama 100 hivi,tutafika mbali sana.
 
Bila kujali mambo ya uvyama,kama Wabunge wa CCM wataanza kuwa makini,mambo mengi ya hovyo yasingetokea. Kumbuka hiyo video Clip ni ya muda mrefu,lakini leo yanatimia.Sasa mchangiaji imekuuma kuona kwamba aliyoyasema Tundu Lissu zamani leo yanatimia. Kwa ushabiki wako ukadhani Tundu Lissu aliongea leo,kumbe ni muda mrefu. Tukubali tu kuwa katika Taifa,watu kama Tundu Lissu,JPM tunatakiwa tuwe nao kama 100 hivi,tutafika mbali sana.
Tunahitaji watu kama Rais John P.M na Tundulisu zaidi ya 100 mkuu. Tundu Lisu na Rais Magufuli wana nia njema na wanaona mambo mengi ambayo kama umejifungia kwenye ukada kamwe huwezi kuyaona. Na ili mambo yazidi kwenda vizuri inabidi waendelee kubaki vyama tofauti ili mmoja aendelee kuwa kama third eye kwa mwengine.
 
Majizi chadema kwa kujipendekeza hawajambo
Hapo ndipo watz tunapoonekana hatuna kitu kichwani kwa hoja mfu kama hizi ,hao chadema wanaingiaje hapa ?na ukizungumzia majizi nadhani utafahamu nani wahalifu katika jambo hili,ni wakati wa kuweka mshikamano kama watz na kumuunga mkono Rais wetu katika kukabiliana na tishio hili kuu la uchumi wetu ,tupunguze comment za kipumbavu za kunyooshea vidole wasio husika ,tubadilike katika matumizi ya akili zetu!
 
Tutaweza kutoka hapa tulipo na kufaidika na rasilimali zetu tu endapo bunge litasimama kama mhimili na kuachana na siasa za vyama vyao. Bila bunge imara hakuna kipya zaidi ya mipango mingi isiyo na utekelezaji

WabunGe hawa ambao wakati wa kampeni wanahonga wanaenda kwa waganga nk. We una utani sana
 
Ni kweli kuwa maamuzi mengi ya serikali ni ya zimamoto! Katika mambo ya kitaalamu wabunge wangekuwa wanapewa muda wa kutosha kufanya consultation kwa wataalamu wa masuala husika!
Kwa wabunge wenyewe hawa wa ccm wachumia tumbo, wao kila kitu ndioooo,
Kwa unafiki wao hapo wanampongeza rais wakati maazimio mabovu wanayapitisha wao bungeni.
 
Back
Top Bottom