Ki msingi mimi nimestushwa na Taarifa ya "kamati ya uchenjuaji" kuwa tumeibiwa mali zenye thamani ya trilioni 280. Serikali nzima hakuna aliyekuwa na taarifa wala kustuka.
hivi serikali imelala au imeamka ?
huwezi kuwa unasimamia duka na una watendaji kila siku wako dukani wanasimamia alafu mali zinazoibiwa dukani ni mara 10 ya zile zinazoingia kwenye vitabu alafu ujiseme unasimamia duka. kuna tofauti gani taifa kuwa na utajiri wa hali ya juu na umeunda chombo cha kusimamia mali hizo and then kinaibiwa mali zote hizo na uone jambo la kawaida.
ki msingi kunakuwa na tatizo kubwa sana na sio watendaji wachache.
kuna haja ya ku "overhaul" entire government system.
1. inakuwaje tunaibiwa hivyo hakuna chombo hata kimoja chenye wajibu wa kuwamonitor hawa tuliowakabidhi mali zetu wazilinde tukiamini ni nyuki watakaotumia mali hizo kututengenezea asali tule kumbe ni mchwa wanaotafuna mali hizo na kutengeneza vichuguu.
kwa nini wizi mkubwa kama huu tuubaini kwa kutumia tume? na maovu siku zote mpaka tuunde tume ndio tunabaini.
Kuna tatizo katika mfumo na utaratibu wa utendaji ndio maana
1. waziri mkuu anakuwa ni kama shati tu lipo, limekabidhiwa wajibu wa kusimamia shughuli za kila siku za serikali lakini hajui kinachotendeka katika wizara. Kuna tatizo.
2. waziri anakuwa kama bendera katika wizara, ngonjera nyingi si unajua bendera ikipulizwa na upepo inavyodansi kwa sana, mara umeme vijijini, mara tuna gesi ya kutosha miaka mingapi kumbe upepo unakotokea kuna mbwa mwitu wanatafuna kila kitu. vipofu hawaoni wako kwenye ngonjera.
3. Bunge liko wapi lenye wajibu wa kusimamia na kushauri hawa.
imekuwaje hakuna aliyekuwa akiona kinachofanyika mpaka tumeunda tume kuchunguza uchenjuaji ndio tunabaini uozo wa hali ya juu.
si swala la serikali kujikweza au bunge kupongeza bali kila aliyeko kwenye utendaji kuona aibu kuwa kwa haya alikuwa wapi kuona.
Yaani unasimamia duka na siku moja wanaleta mkaguzi kukagua inabainika fedha mara kumi ya mahesabu yako inaibiwa na huna habari na wewe unakaa kupongeza eti mkaguzi kafanya kazi nzuri.
Yawezekana kutoa huyu na kuweka yule kusilete tija maana hatujui kiini cha tatizo bali kutafuta chimbuko la tatizo ndio jambo la msingi.
Mimi nadhani tufanye yafuatayo.
1. Ni upumbavu kumlipa mtu anayeitwa mbunge fedha nyingi sana kuliko watendaji wanaokesha maofisini, wenye utaalamu wa kibobezi eti mtu kwenda bungeni kujadili mawazo yake.
tunawaita wawakilishi wa wananchi kwa kigezo cha kuchaguliwa na wananchi lakini nani anayeweza kuonyesha uwakilishi wa wananchi katika utendaji wao? mtu anatoka kwenye biashara zake anaenda bungeni kujadili fikra zake na mitizamo yake eti anawakilisha wananchi.
matokeo ya mfumo mbovu wa bunge ni kutokupata " function" ya bunge iliyokamilika ya kusimamia na kushauri serikali.
yaani mtu akienda pale akaweka neno nashauri serikali, akajdili mipango ya serikali kwa kutaja majina ya vijiji na kadhalika eti ni bunge?
Bunge kiwe ni chombo cha kukusanya takwimu, wabunge wawe wabunge wakaazi full time kwenye ofisi za wabunge wakikusanya takwimu za kila kinachoendelea katika jimbo. madiwa wote wawe chini ya wabunge na kila diwani anakusanya takwimu katika kata na majumuisho ya taarifa za madiwani ndio wajadili na yale wanayoweza kufuatilia katika jimbo au halmashauri wafuatilie.
ofisi ya jimbo iwe wazi kupokea kero za wananchi mda wote, mtu amenda hospitali hajapewa dawa anaenda kuuliza kwa bunge na mbunge anafuatilia kwa watendaji, mtu kaombwa rushwa ili ahudumiwe yeye ni kwenda kwa mbunge, anazungushwa . na yale ambayo yanashindikana kutatuliwa na watendaji katika jimbo lake ndio ayafuatilie ngazi ya taifa.
yenye utata na majumuisho ya repoti za wabunge ndio performance ya wizara na ndio iwe base ya bunge kupongeza au kukosoa au kushauri wizara. na hapo mbunge kweli anakuwa kiungo baina ya serikali na wananchi na ndio maana ya kuwawaklisha sio kulipa wazururaji wanaotoka katika biashara zao kwenda bungeni kujadili mawazo yao na serikali haisimamiwi hata kidogo.
............................