Sakata la kuuawa kwa Faru John lachukua sura mpya. Watumishi watano watiwa mbaroni

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Maofisa watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wanaotuhumiwa kushiriki kumwondoa faru John kutoka katika Creta hiyo walikamatwa juzi kwa mahojiano ili kujua ukweli kuhusu mazingira ya kupotea kwake.

Hatua ya maofisa hao kukamatwa imekuja siku tatu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuituhumu menejimenti, wafanyakazi wa NCAA na Baraza la Wafugaji (NPC) kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la faru John ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh200 milioni kwenye Hoteli ya Grumet iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh100 milioni.

Waziri Mkuu alisema anataka kumwona faru huyo, nyaraka za kumhamisha na kama amekufa basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisisitiza kuwa ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.

Habari za uhakika kutoka Ngorongoro, ambazo zimethibitishwa na Jeshi la Polisi zinasema kuwa maofisa hao watano wanashikiliwa katika kituo chao cha Ngorongoro kutokana na ushiriki wao kwa njia moja au nyingine.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Israel Naman ambaye alikuwa Kaimu mkuu wa idara ya uhifadhi wakati faru huyo akiondolewa.

Wengine ni Cuthbert Lemanya, ambaye alikuwa Mkuu wa Kanda ya Creta, Dk Athanas Nyaki ambaye anadaiwa kumdunga sindano ya usingizi ili aweze kubebwa.

Maofisa wengine waliokamatwa ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Kuya Sayaleli na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ikolojia, Patrice Mattey.

Ofisa mmoja wa NCAA, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake jana alisema maofisa hao walikamatwa juzi jioni na jana walikuwa wanaendelea kuhojiwa.

“Tuiache serikali ifanye kazi kwani ni muhimu sana kujulikana ukweli wa tukio hili,” alisema ofisa huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakupatikana jana kuelezea tukio la kukamatwa maofisa hao, baada ya simu yake kupokelewa na msaidizi wake ambaye alieleza yupo kwenye kikao.

Lakini, ofisa wa mmoja wa polisi, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina kwa kuwa si msemaji alikiri kukamatwa maofisa hao kwa mahojiano.

Chanzo cha sakata
Akiwa katika ziara ya kikazi Ngorongoro, Waziri Majaliwa aliibua sakata la kuhamishwa kinyemela faru huyo na kudaiwa kupelekwa Grumet.

Waziri mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa John aliyeondolewa Creta na kupelekwa Grumet na kudaiwa kufa huku taarifa za kifo hicho zikifanywa siri.

Waziri Mkuu alitaka kupewa nyaraka zote zilizotumika kujadili kumuondoa faru na kuamua kumpeleka Grumet.

Waziri Mkuu alitoa hadi Desemba 8 (jana) awe amepata taarifa zote, ikiwamo ya daktari inayothibitisha kifo hicho na kwamba pembe za faru huyo zifikishwe ofisini kwake. Pia, Majaliwa alisema ikibainika wapo waliokiuka taratibu watawajibika.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawa hawawezi kumpeleka faru bila kuelekezwa na uongozi wa hifadhi Na Wizara husika. Naamini wapo waliotelekeza jukumu hili kwa makusudi hao ndo wawajibishwe. Hawa ni kuwaonea kwanza hawana itifaki ya kuongea na tajiri anayemiliki grumeti game reserve.
 
Watu hao wasingeweza kufanya jambo/tukio hilo sensitive pasipo maelekezo kutoka juu....

Waziri wa wakati huo na pia Katibu Mkuu wa wakati huo na hata wakurugenzi wa idara husika wizarani lazima wanafahamu sakata Zima...

Nchi hii ifike mahala tuheshimiane na kunyooka...haiwezekani washikwe watu wa chini tu....hao wengine nao wakamatwe na wahojiwe...justice doesn't 'look' into faces....justice should be seen by all to be fair...

Key words here: justice, fair, all
 
Hawa hawawezi kumpeleka faru bila kuelekezwa na uongozi wa hifadhi Na Wizara husika. Naamini wapo waliotelekeza jukumu hili kwa makusudi hao ndo wawajibishwe. Hawa ni kuwaonea kwanza hawana itifaki ya kuongea na tajiri anayemiliki grumeti game reserve.
yule aliyehojiwa na waziri mkuu alitaka kufafanua akakatishwa,huu mziki unaanzia makao makuu ya wizara,japo inasemwa taratibu zilifatwa,tena zote,sasa ukianza kuhoji wanyama wanavyokufa porini,kuna mtu huwa anakesha nao huko vichakani
 
how is it possible kifaru ambae anatambulika kwa jina kabisa anaondololewa kwenye crater anapelekwa sehem nyengine then taarifa haipo wizarani.
Ina maana wazir husika either wa awamu iliyopita na leo hawajaliona hilo swala mpka wazir mkuu aje kuona hapo kuna tatzo juu ya uhamishwaji wake.
Siamin sana hao watumish wa chin wana uwezo na nguvu kubwa kias hcho cha kufanya hayo maamuzi ya kumuhamisha / kufa kwa faru john then wayafanye bila boss wao asijue lolote.
 
Kumbe! Basi we tega tuu sikio utalisikia jina lake huyo "raia wa Marekani"[/QUOTE)

Nasikia hotel yake analeta VIPS tu na celebrities duniani hata opra na Bill gate na mtot wao walikaa mwaka jana August, anatoa US 300,000 kila mwaka kama hunting fees lakini hawindi ngoja zinakuja nyingine usiondoke
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Nasikia hotel yake analeta VIPS tu na celebrities duniani hata opra na Bill gate na mtoto wao walikaa mwaka jana August, anatoa US 300,000 kila mwaka kama hunting fees lakini hawindi ngoja zinakuja cha kujiuliza nini kwann alitaka Faru apelekwe pale kwake?????????????????????????????????????????????????????????
 
Back
Top Bottom