Sakata La Kutorosha Wanyama Hai: Serikali Ya CCM Yawafutia Mashtaka Watuhimiwa Watatu

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), amewafutia mashtaka watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutorosha isivyo halali wanyamapori hai kwenda Doha, nchini Qatar. Wanyama hao wakiwamo twiga wanne, wenye thamani ya Dola 113,715 za Marekani walisafirishwa Novemba 26 mwaka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Ombi la kuwafutia mashtaka watuhumiwa hao liliwasilishwa mahakamani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo. Liliwasilishwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Araffa Msafiri, Evetha Mushi na Pius Hilla.Waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Jane Mbogo, raia wa Kenya ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Equity Aviation Services na maofisa usalama wawili wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Authority (Kadco).

Maofisa hao ni Veronica Benno na Locken Kimaro ambao jopo la mawakili wa Serikali walisema DPP ameamua kuwafutia mashtaka na kuiomba mahakama iwaachie huru, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna haja ya kufanya hivyo.


Katika hatua nyingine, upande wa mashtaka umebadilisha hati ya mashtaka, kusoma hati mpya na kumwongeza mshitakiwa. Mshtakiwa huyo ni Michael Mrutu ambaye ni Ofisa Usalama wa Kadco na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa waliobakia katika kesi hiyo kuwa wanne.


Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande hadi Desemba 4 mwaka huu na kutakiwa kuwasilisha maombi yake ya dhamana katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, yenye uwezo wa kusikiliza mashtaka ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kamran Ahamed ambaye ni raia wa Pakistan, Hawa Mang’unyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders na Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary).


Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi likiwamo la kusafirisha wanyama kwenda Doha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh170.5 milioni.Mshtakiwa Ahmed na Hawa wanakabiliwa na mashtaka mengine yakiwamo ya kula njama na kufadhili utoroshwaji wa wanyama hao, kufanya biashara ya wanyamapori bila leseni na kumiliki nyara za Serikali isivyo halali.


Kwa upande wao, Kimath na Mrutu wanakabiliwa na mashtaka ya kuwezesha kufanikisha mpango wa kuwatorosha wanyama hao, kushindwa kuzuia kosa na pia kushindwa kutoa taarifa za tukio hilo. Hata hivyo, washtakiwa walikanusha mashtaka dhidi yao. Jopo la mawakili wanaoendesha kesi hiyo waliiambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kwamba jana walikuwa tayari kuanza usikilizaji wa awali.

Hata hivyo washtakiwa waliiomba mahakama iahirishe kuendelea na usikilizaji huo wa awali, kwa maelezo kuwa wanatarajia kukodi mawakili wa kuwatetea na hasa ikizingatiwa kuwa wao hawajui sheria zinazohusu kosa linalowakabili. Hakimu Kobelo alilikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 4 mwaka huu na kuwataka washtakiwa wahakikishe siku hiyo wanakwenda na mawakili wao, ili mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa awali.


Dhamana ya washtakiwa watatu awali inaendelea isipokuwa mshtakiwa wa nne ambaye ametakiwa kuwasilisha maombi yake ya dhamana katika Mahakama Kuu ya Tanzania Tayari vigogo watatu wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii wamefukuzwa kazi kutokana na utoroshaji wa wanyama hao huku kigogo mwingine akishushwa cheo kwa kushindwa kuchukua hatua kudhibiti utoroshaji huo.
 
Tunamalizia uchunguzi alafu tunampandisha kizimbani katibu mkuu wa ccm kosa la kuua tembo na kusafirisha pembe za ndovu kwa meli yake.

HATARI:
Weka mbali na Tembo.
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Kinana aongezwe hapo wawe watano.
 
Kale kamchezo ka kucheza na akili za watu ili kufutika mambo kwa kutumia akili ya kubai/ kucheza na muda kanaendelea

Kama kwa epa, kama kwa rada na kama kwa richmond nk hakika bila kuitoa serikali ya ccm madarakani tutaendelea kuibiwa daima.
 
Wanaserikali wa CHUKUA CHAKO MAPEMA ndiyo wauzaji maliasili zetu (twiga, pembe za ndovu n.k)
 
Hii ni katika kumnusuru katibu mkuu wa magamba kwani yeye ndiye mfadhili wa majangiri na watorosha wanyama hai.
 
Usanii mtupu, serikali yenyewe inahusika. Suala la Loliondo tangu Raisi Mstaafu Mwinyi hadi leo bado lipo.
 
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kamran Ahamed ambaye ni raia wa Pakistan, Hawa Mang’unyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders na Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary).

Mkuu, ndiyo sababu tunasema waandishi wetu ni uchwara. Zoosanitary ni kitengo cha serikali (Wizara ya mifugo) kinachohusika na udhibiti wa usafirishaji wa wanyama na mazao ya wanyama kutoka eneo moja la kijiografia kwenda lingine (Sio shamba la wanyama). Wako kwenye vituo vyote ambapo wanyama hupitishwa kisheria (Border posts) kama mipakani (Namanga, Tunduma, Kasumulu, Holili, etc), Bandarini na viwanja vya ndege. Kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanyama wanaotolewa nje ni halali - hawako kwenye orodha ya wasioruhusiwa, kuhakikisha kuwa wana afya nzuri,au wapepata chanjo zinazohitajika na wana vibali vya wizara ya mifugo kusafirishwa kwenda nje. Pia wanahakikisha kuwa wanyama na mazao yao yanayoingizwa nchini hayataathiri afya za wanyama wetu na binadamu humu ndani na yanavibali husika vya kuruhusiwa kuingizwa.

Kwa sababu ya unyeti wa kazi yenyewe, wahusika wanatakiwa kuwa na elimu na vifaa vya kutosha na wawe chini ya usimamizi wa daktari wa mifugo anayeweza kutambua magonjwa ya wanyama, namna ya kuyatambua, uelewa wa sheria za kimataifa za usafirishaji wa wanyama na mazao yake pamoja na sheria zilizopo nchini mwake za kudhibiti mazao hayo. Hawahusili kabisa na utozaji wa kodi yoyote, hilo ni suala la TRA. Kwa wale waliosafiri kwenda nchi za wenzetu wanaojali maliasili hai nchini mwao mnawaona hawa watu kwenye airports wakiuliza maswali kama " umebeba chochote kimachohusiana na wanyama au ulishawahi kuwasiliana/unahusika na wanyama wa aina yoyote ulikotoka?" etc.

Kwa nchi yetu, kwa kuwa huko kuna ulaji, wengi waliowekwa ni vilaza na wanapendelewa kupewa hizo nafasi wa udhibiti airports. Aidha, hawana vifaa vya aina yoyote ya kutambua magonjwa wala kukagulia vibali kama ni halali au la. Hiyo ndiyo hali ya kwetu.
 
ni vigumu sana kuamini kuwa haya mambo yanafanyika bila serikali yenye uwakilishi kila kona msituni mpaka airport kuyafahamu; masuali ni mengi kuzidi majibu hapo.
 
Back
Top Bottom