Sakata la kutekwa Mo Dewji: IGP Sirro na Waziri Lugola mnangoja nini kujiuzulu?

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
IGP Sirro(Ziro) na Waziri wake wa Internal Affairs juzi wamevuliwa nguo na kuachwa uchi wa nyama. Kitendo cha Rais Magufuli kuliponda na kulishambulia Jeshi la Polisi kwa kushindwa KUWAKAMATA WALIOMTEKA Mohamed Dewji(Mo) kinatosha kuonesha kwamba IGP Ziro na Kangi Lugola hawatakiwa kuwepo kwenye nyadhifa hizo..!!!

''Watanzania siyo wajinga...'' haya ni maneno mazito ya Rais Magufuli aliposema mbele ya hadhira wakti wa kuapishwa kwa Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje Palamagamba Kabudi.

Ukiunganisha hili tukio la kutekwa kwa MO Dewji na Kushambuliwa kwa Mhe.Tundu Lissu mchana kweupe tena ndani ya Viunga vya Bunge la JMT pale Area 'D' unaweza kugundua kuwa Tanzania haina Jeshi la Polisi isiokuwa tuna mijitu inavaa sare za Kipolisi na kula Mishahara ya bure.

IGP Ziro atuambie sasa hao WAZUNGU kutona nchi jirani waliomteka Mo wako wapi mpaka leo? Ilikuwaje kweli wakakaa na Mo wiki nzima bila ya IGP Ziro na makamanda wake kubaini Mo yuko wapi. Halafu watekaji wanatokea Usiku kwenye nyumba fulani wakiwa na Mo na kumtelekeza barabarani na silaha zao huku Ziro na Makamanda wake wakiwa usingizini wanakoroma....!!

Matukio haya 2 ya Mo na Lissu yanatosha kabisa kuwafanya Afande Ziro na Waziri Kangi Lugola KUJIUZULU kwa KOSA LA UZEMBE NA KUTOWAJIBIKA. Kama la hawawezi kujiuzulu basi Rais John Joseph Pombe Magufuli AWAFUKUZE KAZI kwa kuwafanya WATANZANIA KUWA NI WAJINGA. Watanzania tumechoka kufanya wajinga na mandondocha lazima watu wawajibike. Haiwezekani Raia wa Kitanzania wasio na hatia wawe wana TEKWA, KUPOTEZWA na KUSHAMBULIWA mchana kweupe huku Jeshi la Polisi likiwadanganya Watanzania kuwa ni wanaofanya vitendo hivo ni WATU WASIOJULIKANA...Sasa ifike mwisho.

Wasalaam.
 
..hata ktk suala la TL nimemsikia Waziri Lugola akitoa kauli ambazo naamini zinaichafua serekali, na iko siku zitamgharimu.
 
Akili za kuambiwa nawewe ongeza na za kwako! Sio kila anachoongea jiwe usichukue kama kilivyo, anataka kujisafisha kwa wananchi wavivu wa kufikiri, lakini sio kwa mtu mwelevu. Huwezi kujitekenya na kucheka mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi nimeongeza akili zangu mara dufu baada ya kusikia kauli ya Jiwe.
Tunataka kama ni kweli Jiwe ametamka toka moyoni basi AWAFUKUZE HAWA JAMAA WAWILI vinginevo na yeye tutamuunganisha Jiwe na hao wateule wake kwa kuendelea kuwafanya WATZ KUWA WAJINGA. Mimi nasubiri Rais Magufuli atoe tangazo kutoka Ikulu ya kwamba IGP Ziro na Kangi Lugola wametumbuliwa kwa UZEMBE na UONGO na hasa baada ya Waziri Lugola kuwadanganya Watanzania kuwa SIKU YA SHAMBULI LA TUNDU LISSU HAKUKUWA NA CCTV CAMERA...!!!!
 
..hata ktk suala la TL nimemsikia Waziri Lugola akitoa kauli ambazo naamini zinaichafua serekali, na iko siku zitamgharimu.
Naaamini Magufuli anafahamu vizuri matukio hayo hata kabla ya kutokea, naona anajikosha tu.
 
Naaamini Magufuli anafahamu vizuri matukio hayo hata kabla ya kutokea, naona anajikosha tu.

..hata mimi nimeshangaa kwanini ulianza kuzungumzia suala la Mo Dewji pale Ikulu.

..utakumbuka alisema alikuwa na mkutano na Waziri Lugola na IGP Sirro. Sasa kwanini hakuwasilisha madukuduku yake ktk kikao hicho ili hatua zichukuliwe?

..Au hata pale Ikulu kwanini hakueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa badala yake analaumu na kuliacha suala hilo hewani?
 
..hata mimi nimeshangaa kwanini ulianza kuzungumzia suala la Mo Dewji pale Ikulu.

..utakumbuka alisema alikuwa na mkutano na Waziri Lugola na IGP Sirro. Sasa kwanini hakuwasilisha madukuduku yake ktk kikao hicho ili hatua zichukuliwe?

..Au hata pale Ikulu kwanini hakueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa badala yake analaumu na kuliacha suala hilo hewani?
Ni kutaka aonekane mwema...........
 
propaganda ni taaluma. tatizo ukiwa ccm unajiona una akili kubwa wakati uhalisia sio
 
Alichofanya Mh.Rais ni kuwapa muda polisi ili watimuize majukumu yao, sio kama mijitu mingine inavyoshauri kuwa Mh.Rais awafukuze baadhi ya watendaji wa polisi . Magufuli nsi mkatili kiasi hicho kwani anajua makosa ni kwa binaadamu na kama wakipewa maagizo/maelezo wanaweza kujirekebisha na kutimiza wajibu wao,na hivyo ndivyo alivyofanya Mh.Rais.
 
Back
Top Bottom