Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Nakumbuka ajira za watendaji wa vijiji /mitaa zilipoanzishwa(kama sikosei mwaka 2006) ndio zilifuta utaratibu wa wenyeviti wa mitaa kumiliki mihuri na badala yake watendaji wa mitaa ndio walitakiwa kukaa na mihuri wakiwa ndio watendaji wakuu wa shughuli katika ofis ya serika ya mtaa
Nakumbuka pia Watendaji wa mitaa/vijii walikabidhiwa mihuri na baada ya wao kukabidhiwa ndio wenyeviti waliagizwa warudishe mihuri jambo ambalo utekelezaji wake ulikuwa mgumu kutokana na upinzani uliojitokeza.
Swala hili la kuwapa mihuri watendaji wa vijiji na mitaa na kuwanyang'anya wenyeviti wa mitaa mihuri lilisababisha baadhi ya wenyeviti wa mitaa kukataa kuwapokea watendaji wa mitaa katika ofiso zao/nyumba zao zilizokuwa zikitumika kama ofisi za serikali ya mtaa maana watendaji wa mitaa zilikuwa ni ajira mpya na hawakuwa na ofisi.
Kwahiyo hapa tatizo bila shaka itakuwa ni sheria iloyotungwa kutambua/kuanzisha ajira za watendaji wa mitaa/vijiji maana mihuri yao ndio inatambulika kisheria ingawa jambo hili limekuwa halizingatiwa hata na serikali yenyewe.
Kwa mfano, form za bodi ya mikopo bado zinawatambua wenyeviti wa mitaa na si watendaji wa mitaa hivyo katika hili hata serikali yenyewe ni ya kulaumiwa.