Sakata la kujivua gamba CCM Zitto adai Serikali imejitia kitanzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la kujivua gamba CCM Zitto adai Serikali imejitia kitanzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  *Zitto adai Serikali imejitia kitanzi

  NA Waandishi Wetu, jijini Habari Leo

  MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema kitendo kinachofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa watendaji wake
  kutakiwa kujivua gamba kinaweza kuathiri utendaji wa Serikali.

  Zitto amesema CHADEMA haioni kuwa kitendo hicho kinaweza kukisaidia chama hicho kuwa na wanachama wasafi.

  “Sidhani kama huo utaratibu unaweza kuwaondoa mafisadi bali kunaweza kuathiri utendaji wa Serikali kwa kuwaondoa viongozi wasio na makosa,” amesema Zitto.

  Amesema kwa kuwa wapinzani wakubwa wa CHADEMA ni CCM, wamedhamiria kukaa pembeni na kuangalia ni kitu gani kitafuatia.

  Zitto amesema suala la ufisadi ni jukumu la mtu binafsi kuamua kuachana na suala hilo na si la kushinikizwa.

  “Hivi sasa CHADEMA inaangalia mechi hiyo ili kuweza kufahamu itakwishaje na ndio maana tumekaa pembeni kuwaangalia hawa wapinzani wetu wakubwa,” amesema Zitto.

  Zitto amesema chama chake kitaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kuhakikisha kuwa suala la ufisadi linakomeshwa nchini.

  Amesema bado suala hilo linahitaji nguvu zaidi kwa kuwa baadhi ya maeneo kumejengeka mizizi ambayo inahitaji kung'olewa.

  “Hii mizizi inahitaji kung'olewa hivyo kama wananchi wataamua kufanya hivyo itawalazimu kwanza kukubaliana na CHADEMA kwa kukipa nguvu zaidi katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu,” amesema Zitto.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hii mechi itakuwa kama ile ya Real Madrid na Barcelona. There will be plenty of divers lakini hawataonyeshwa red card.
   
 3. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I couldn't Agree more Zitto..............

  Either way, CCM inajimaliza yenyewe as time pass by...........
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mizizi imetanda hawawezi kuikata kiusalama; CC na NEC yote ina matajiri Uchwara
   
 5. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unafiki mtupu
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  we shetani mwekundu nini?
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  chuki tupu
   
 8. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nani mnafiki?
   
 9. M

  Magamba Member

  #9
  May 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unafiki Upi?
   
 10. m

  mkulimamwema Senior Member

  #10
  May 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna chama cha wababaishaji kama ccm ilikuwa siku 90 sasa wamesema chama kimekuwa imara baada ya kuvua MAGAMBA ngoja wajimalize wenyewe kwa kucheza na uozo
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MHESHIMIWA ZITTO NAKUOMBEA KWA MUNGU AKUJALIE TENA ULE UJASIRI WA ZAMANI WA KUNYOOSHA KAULI JUU YA MASUALA NYETI NA YENYE MASLAHI YA UMMA KITAIFA

  Zitto Zuberi Kabwe,

  Naomba sana tukubaliane kutofautiana kidogo katika baadhi ya kauli ulizozitoa humu.

  Kwanza, endapo kilichoandikwa ni maneno yako kweli basi nikatae hapa kwamba JANGA LA UFISADI (kauli ya kwanza hapo chini) si suala la Mtu binafsi na kwamba akaachwe tu kule kujipima mwenyewe na kuhiari njia gani akajipitie.

  Sababu yangu kuamini hivyo ni kwamba kodi zinazosadikiwa kukwapuliwa na watuhumiwa wa UFISADI ulikua ni mali ya Umma kwa ujumla wetu hivyo kufanya suala zima hapa kuwa na Maslahi ya Jamii nzima ya Tanzania.

  Hivyo watuhumiwa wa ndani ya CCM na serikali yake wakimaliza KUBEMBELEZANA KUJIUZULU huko katika kifindi cha siku 90 basi sisi Nguvu ya Umma tutalazimika kuchukua hiyo kesi kuja kwenye mahakama yetu ili kama waathirika wa janga hilo, ukwapwaji wa kila mara ya kodi zetu na kudidimiziwa maendeleo, ili tukalitolee maamuzi sahihi na ya kudumu.

  Pili, kwa kuzingatia ukweli kwamba zao 'Pamba' kamwe haiwezi kufifia hata kidogo ueupe wake endapo wakati wote halikukutana na uchafu wowote popote pale, basi hata watumishi wetu serikalini uliowataja kama 'Wasio na Makosa' nao kamwe hawawezi kupigwa dhoruba yoyote ile ya fagio la chuma kuondoa ufisadi kwenye mfumo wetu kama hawakuwahi kushiriki UFISADI au kusaidia jambo hilo kutokea.

  Kwa msingi huo, aheri tubaki na watumishi wawili waaminifu katika kila idadi 1000 ili nafasi hizo 998 zikatangazwe kwa utaratibu mpya, kuzingatia miiko ya uongozi ndani ya Azimio la Arusha na sheria na vyombo vya usimamizi kuimarishwa maradufu kuzuia kabisa hali hiyo. Endapo mtapenda kujua 'njia zipi zitumike mara baada ya hapo' basi mkatuulize hapa JF - tutatoa mkakati kiboko ambayo hakuna atakayeamini wengine tumeikalia tu kimya hapa kwa kuwa hata siku moja hatupewi nafasi tu.

  Tatu, yeyote atakayekua amesoma na kutafakari vema kauli yako namba moja na mbili bila shaka atakua amebaki ameduazwa bila kuelewa kama aliyetoa na kauli ya tatu na ya nne bado ni mtu yule yule AU NI NAFSI YA KUTOKEA wakati zile kauli mbili za mwazo zilitoka kwa NAFSI YA KUSHINDIA ndani mwake mtu yule yule mmoja.

  Hiyo hali ya mkanganyiko unatokana na ukweli kwamba tayari umetoa Judgment kwamba Mtanzania yeyote ni ruksa tu kuwaibia wenzake ilmradi tu kipenyo kinapatikana kwaki kama kiongozi wa ngazi fulani hivi ila pale suala la kuwajibika kubeba mshahara wa dhambi hiyo basi sasa Wa-Tanzania wenye kuibiwa kamwe hawana nafasi kumtaka MKWAPWAJI YEYOTE kubeba msalaba wake mpaka jambazi huyo tu akiamka vizuri ndio akajionelee kama ni vema akaturejeshee kilichoibwa au ajiuzulu au asijishughulishe kabisa na lolote lile.

  Mhe Zitto, hili nalipinga hata kama Mwalimu Nyerere ninayemuamini saana ndio ngekua ametoa kuli kama hii. Ingawaje utakua umesaidia sana kuwafariji wahusika kiaina ila kiama cha mfumo mzima wa kifisadi uko pale pale hivyo hata kama kiongozi wangu wa CHADEMA (wewe mwenyewe ukiwemo) atathibitika kuwa ni sehemu ya ukwapaji huo basi itakua ndio hivyo tena ...!!!

  Mwisho, kama kuna kitu kinachonifanya siku zote kuwapenda viongozi weengi sana ndani ya CHADEMA basi ni kule kuwa na ujasiri wa kutoa KAULI NYOOFU usiopinda pinda kiasi cha kuweza kuzalisha maana zaidi ya moja juu ya mada ile ile au kule kutafuta kufurahisha pande zote tatu za sarafu.

   
 12. J

  Joblube JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni uchambuzi makini (Great thinker)
   
 13. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
   
Loading...