Sakata La Kugombea Eneo La Mafuta Sudan:Mahakama ya Kimataifa Yakata Mzizi wa Fitina.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
t.gif
_44658796_sud_bahr_al_ghazal_226map.gif

Mpaka mpya wa Abyei
Sudan ya kusini na kaskazini zimesema kua zimekubali uamuzi wa Ma Jaji wa Mahakama ya Kimataifa juu ya mipaka.
Chini ya uamuzi huo wa Mahakama ya upatanishi eneo lenye visima vya mafuta la huko Abyei sasa limekabidhiwa mamlaka ya kaskazini.
Uamuzi huo umeweka mipaka mipya ya jimbo la Abyei ambalo katika kipindi kizima cha mgogoro wa miaka 22 lilikua kiini cha mvutano baina ya kaskazini na kusini.
Mipaka iliyopendekezwa baada ya mpango wa amani wa mwaka 2005 ilipingwa na viongozi wa kaskazini na hivyo ma jaji wa mahakama waliipuuza katika uamuzi wa sasa.
Hata hivyo waliamua kua sehemu kadhaa vikiwemo visima vya mafuta vya Heglig si sehemu ya Abyei.
Wadadisi wanasema kua ingawa jukumu la Mahakama ya The Hague lilikua juu ya mipaka ya Abyei na sio nani mmiliki wa ardhi hio, uamuzi huo utasaidia nani atamiliki visima vya mafuta.

SOURCE:BBC SWAHILI SERVICE
 
Junius,

..pande zote mbili Kusini na Kaskazini wamesema wameridhika na hukumu hiyo.

..manasema kila upande ulikuwa right or wrong on something.

..eneo lenye visima vya mafuta lilikuwa linatawaliwa jointly na North and South Sudan. hukumu imeamua kuipa North mamlaka ya visima hivyo.

..pamoja na hayo ifikapo 2011 jimbo la Abyei watapiga kura ya maoni kuamua kama wanataka kuwa chini ya North au South administration.

..vilevile nasikia bado kuna visima vingine vya mafuta ambavyo viko eneo la Southern Sudan.
 
Joka Kuu,
Fikra zangu ni kuwa Salva Kiir anavuta pumzi anajuwa kuwa kilichoamuliwa ni kuwa eneo hilo litakuwa chini ya mamlaka ya North, nani atakuwa dhamana wa rasilimali hizo ambazo wakaazi wake wengi ni mchanganyiko, halijaafikiwa vizuri.
 
Junius,

..uelewa wangu ni kwamba kesi ilihusu eneo lenye visima vya mafuta.

..sasa miliki ya visima hivyo imehamishiwa North.

..kuna visima vingine viko maeneo ya South Sudan na hivyo havikuwa na mgogoro.

..pia kuna kura ya maoni inakuja 2011 ambayo itaamua Abiey inakuwa chini ya mamlaka ya North au South.

..kwa uelewa wangu hiyo kura ya maoni haitabadilisha uamuzi huu wa mahakama ya kimataifa kwasababu visima hivyo tayari viko North.

..kura ya maoni pia itaamua kama kutakuwa na nchi mbili, au Sudan moja.

..inasemekana Salva Kiir anapendelea South Sudan wajitenge.

NB:

..rasilimali ktk eneo hilo ni zaidi ya mafuta. kuna masuala ya MAJI na maeneo ya malisho ya mifugo.
 
Back
Top Bottom