Sakata la Korosho: Kabudi anatakiwa ajiuzulu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Profesa Kabudi azushiwa jambo, Dk Mwakyembe asema uamuzi ulikuwa wa mawaziri wote
Friday May 17 2019
pic+kabudi.jpg

By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
Dodoma. Kutajwa kwa jina la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi kumezua utata na mabishano bungeni, huku Serikali ikisema asilaumiwe peke yake.
Akizungumza katika chombo hicho cha kutunga sheria leo Ijumaa Mei 17, 2019, mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alimtaka Profesa Kabudi kujiuzulu au kuwajibishwa kwa maelezo kuwa alishauri kampuni ya Indo Power ya Kenya inunue korosho nchini wakati haikuwa na uwezo.
"Tunampongeza Rais (John Magufuli) kwa kuchagua wasomi, lakini tuliamini Profesa (Kabudi) angeweza kuwa na uelewa mpana wa kumshauri Rais na Taifa lakini ametuingiza chaka, lazima aachie ngazi," amesema Msigwa.
Kaimu kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, Dk Harrison Mwakyembe alimtetea waziri huyo kwamba uamuzi huo (wa kampuni hiyo kukubaliwa kununua korosho) haukuwa wake peke yake, akisisitiza kuwa ulikuwa wa mawaziri wote
Dk Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema mawaziri wanawajibika pamoja hivyo jambo lolote linalotendeka ni kwa mashirikiano ya pamoja.
"Mheshimiwa mwenyekiti (wa Bunge), sisi tunafanya kazi kwa pamoja lakini wenzetu wanapiga kelele pamoja, siyo sahihi kumlaumu mtu kwani hakusimama mezani na kuamua peke yake," amesema Mwakyembe.
Baada ya kauli hiyo ilizuka kelele kwa wabunge wa pande zote na naibu Waziri wa Viwanda, Stella Manyanya alisimama na kusema Serikali inazo taarifa kuwa baadhi ya wabunge walikuwa wanaomba rushwa kutoka kwa kampuni na wanazifanyia kazi ili wakati mwingine wawataje.
"Humu ndani Serikali inazo taarifa kuwa baadhi ya wenzetu huko (anaonyesha kidole upande walioketi wabunge wa upinzani) walikuwa wanaomba rushwa kwa kampuni tunachunguza na tutawataja," amesema Manyanya.
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amewatuliza wabunge kwa kutishia kuwatoa wengine nje baada ya wabunge wa upinzani kutaka Manyanya afute kauli yake hiyo.
 
Sijawahi ona boga kama huyo mama stela manyanyi nakumbuka sakata la Ulimboka bungeni aliwahi sema kua Chadema ndo walimteka ulimboka, yaani huyu ni kiazi kwelikweli
 
Huyu Paramagamba ni mtu asiye na mafanikio, kila afanyalo linakufa kabla halijazaa matunda.
Yako wapi mazungumzo ya makinikia na kishika uchumba cha Noah mpya kwa kila Mtanzania?
Ziko wapi korosho za kununuliwa na Wakenya?
Huyu sidhani hata Mahakamani kisha wahi shinda kesi yoyote, bila shaka ndio wale mawakili wanaoenda Mahakamani kwa ajili tu yakuahirisha kesi
 
Profesa Kabudi azushiwa jambo, Dk Mwakyembe asema uamuzi ulikuwa wa mawaziri wote
Friday May 17 2019
pic+kabudi.jpg

By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
Dodoma. Kutajwa kwa jina la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi kumezua utata na mabishano bungeni, huku Serikali ikisema asilaumiwe peke yake.
Akizungumza katika chombo hicho cha kutunga sheria leo Ijumaa Mei 17, 2019, mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alimtaka Profesa Kabudi kujiuzulu au kuwajibishwa kwa maelezo kuwa alishauri kampuni ya Indo Power ya Kenya inunue korosho nchini wakati haikuwa na uwezo.
"Tunampongeza Rais (John Magufuli) kwa kuchagua wasomi, lakini tuliamini Profesa (Kabudi) angeweza kuwa na uelewa mpana wa kumshauri Rais na Taifa lakini ametuingiza chaka, lazima aachie ngazi," amesema Msigwa.
Kaimu kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, Dk Harrison Mwakyembe alimtetea waziri huyo kwamba uamuzi huo (wa kampuni hiyo kukubaliwa kununua korosho) haukuwa wake peke yake, akisisitiza kuwa ulikuwa wa mawaziri wote
Dk Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema mawaziri wanawajibika pamoja hivyo jambo lolote linalotendeka ni kwa mashirikiano ya pamoja.
"Mheshimiwa mwenyekiti (wa Bunge), sisi tunafanya kazi kwa pamoja lakini wenzetu wanapiga kelele pamoja, siyo sahihi kumlaumu mtu kwani hakusimama mezani na kuamua peke yake," amesema Mwakyembe.
Baada ya kauli hiyo ilizuka kelele kwa wabunge wa pande zote na naibu Waziri wa Viwanda, Stella Manyanya alisimama na kusema Serikali inazo taarifa kuwa baadhi ya wabunge walikuwa wanaomba rushwa kutoka kwa kampuni na wanazifanyia kazi ili wakati mwingine wawataje.
"Humu ndani Serikali inazo taarifa kuwa baadhi ya wenzetu huko (anaonyesha kidole upande walioketi wabunge wa upinzani) walikuwa wanaomba rushwa kwa kampuni tunachunguza na tutawataja," amesema Manyanya.
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amewatuliza wabunge kwa kutishia kuwatoa wengine nje baada ya wabunge wa upinzani kutaka Manyanya afute kauli yake hiyo.
Prof. Kabudi kama watu wanakomaa atolewe ni sawa na kum-implicate kwa makosa ambayo yalikuwa facilitated na balozi wa Kenya nchini Tanzania.
Balozi Dan Kazungu kumshika mkono huyo mkikuyu mwenzake who knows hakuwa na hela. By the way, ilikuwa ni provisional MoU; sioni kama ni busara sana kwa Mch, Msigwa kukomalia sana swali hili.

Tukirejea 2015, EL aliwapa ahadi wana CDM kuwa atakuja na wabunge zaidi ya 100 toka CCM na nusu ya Wenyeviti wa mikoa. Dr. Slaa akasubiri kuona hao wenyeviti na wabunge; hawakutokea.
Mbona hawakumfukuza EL au kumtaka Freeman ajiuzuru?

It is high time akina Mch. Msigwa na Mbunge Mwambe wajiangalie kwa kutoa boriti ndani ya macho yao kabla ya vibanzi kwenye macho ya wenzao
 
Acha niamini unaota.

Humu ndani Serikali inazo taarifa kuwa baadhi ya wenzetu huko (anaonyesha kidole upande walioketi wabunge wa upinzani) walikuwa wanaomba rushwa kwa kampuni tunachunguza na tutawataja," amesema Manyanya.
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amewatuliza wabunge kwa kutishia kuwatoa wengine nje baada ya wabunge wa upinzani kutaka Manyanya afute kauli yake hiyo.
Hili tosha kuonyesha ubaguzi unavyo shamiri unaposema mbuge wa upinzani kuomba rushwa wakati ukijua atakaye pitisha ni Mawaziri wa chama tawala na wapo wengi bungeni haiingi akilini aibu kwa Waziri Jenista
 
30 Jan 2019
Bodi ya Nafaka na mazao imetia saini na Kampuni ya Indo Power Solution ya kwa ajili ya Ununuzi wa Korosho Tani laki moja ambapo viongozi mbalimbali wameshuhudia mkataba huo akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi ,Waziri wa Viwanda na biashara, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mkoani Arusha.
 
Mpuuzi huyo sijui alikuwa anamaanisha nini kufanya kazi za ovyo.

Huyo Kabudi ndiye aliyewaambia diaspora German sijui wapi kule 'eti na mimi nilikuwa kama ninyi nimefanya kazi za ovyo' Kabudi ulifanya kazi za ovyo na wewe umekuwa wa ovyo.
Serikali yote ijiuzulu tuanze upya
 
Katika hili jambo la korosho , Baraza la mawaziri linaonekana kushawishiwa na hoja ya waziri (mikataba / sheria). Hivyo Palamagamba Kabudi kuwa kinara mbele kabisa kushawishi Indo Power Kenya ipewe tenda, lawama zote ni kwake.

Video hapo juu inaonesha uhusika mkuu wa Palamagamba hadharani kabisa kwa kupitia simulizi zake za kumpamba kwa kupitiliza Brian Mtembei bosi wa Indo Power Kenya aliyekuja na chartered private jet.
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽 Dah! Kuja na ndege yake huyo mnunuzi FAKE, basi kabugi akaona mzigo umeshanunuliwa! 🙉

30 Jan 2019
Bodi ya Nafaka na mazao imetia saini na Kampuni ya Indo Power Solution ya kwa ajili ya Ununuzi wa Korosho Tani laki moja ambapo viongozi mbalimbali wameshuhudia mkataba huo akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi ,Waziri wa Viwanda na biashara, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mkoani Arusha.
 
Ukitaka kuja ni kwa nini Msigwa ni asset muhimu bungeni ni hapo anapoongea bila kumung'unya maneno
 
Back
Top Bottom