Sakata la Kibiti: Mwigulu Nchemba ni wakati wa kujitafakari na kujiuzulu ateuliwe Adadi Rajab

mleta mada amesema kinyume huyu Adadi ana vikundi vyake vya ujambazi vilivyokuwa vinafanya kazi wakati akiwa DCI. ni vema arudishwe tena Zimbabwe vinginevyo hayo mauaji hayawezi kwisha. Apelekwe zimbabwe halafu awekewe ulinzi.
 
Hiyo ni chuki binafsi kwa Mwigulu

Hivi kwann watu hatupendani, akijiuzulu wewe utapata nn kwa mfano...
Husna mbaya sana siwaelewi yaani viumbe wengine, yaani badala ya kushauri nini kifanyike wanaona kujiuzuru ndo solutions
 
Mwiguluuuu Leo yamekugeukia kweli CCM kiboko,

Ndio mazala ya siasa za CCM haya..mmateuana kwa kuangalia ukada leo mnalalamikia mazara..

Waziri wa mambo ya ndani anatakiwa na uzoefu wa maswala ya ulinzi na usalama, wako wazee kibao jeshini huko na usalama wa Taifa.
Waziri wa ulinzi Lazima mkongwe kutoka JWTZ na si vinginevyo.. Ukada usiwe sehemu ya uteuzi.

Brilliant
 
Likitokea tukio lingine basi Mwigulu aachie ngazi kulinda weledi na heshima
 
Mwiguluuuu Leo yamekugeukia kweli CCM kiboko,

Ndio mazala ya siasa za CCM haya..mmateuana kwa kuangalia ukada leo mnalalamikia mazara..

Waziri wa mambo ya ndani anatakiwa na uzoefu wa maswala ya ulinzi na usalama, wako wazee kibao jeshini huko na usalama wa Taifa.
Waziri wa ulinzi Lazima mkongwe kutoka JWTZ na si vinginevyo.. Ukada usiwe sehemu ya uteuzi.
Mazala - madhara! Uwiiiiii duh!
 
Hiyo ni chuki binafsi kwa Mwigulu

Hivi kwann watu hatupendani, akijiuzulu wewe utapata nn kwa mfano...
Akiendelea kubaki wewe unapata nini? Kwani kujiuzulu ni dhambi? Hilo ni tendo la kiungwana na huonyesha mhusika anajali. Anaomba kukaa pembeni ili wengine waje na maarifa tofauti! Lengo hapa ni kutafuta suruhisho sahihi! Inawezekana hana uwezo wa kuendana na hiyo wizara!

Kauli yake kuwa hayo mauaji ni siasa inaonyesha alivyo gizani! Unawezaje kutoa kauli hiyo ikiwa hujui nani anafanya mauaji yenyewe? Unawezaje kutoa kauli hiyo ikiwa wauaji wako kimya na hawajatamka chochote?

Huyu ni waziri aliyewahi kutamka kwamba anawafahamu waliolipua mabomu kule Arusha, lkn mpaka leo hajawahi kutamka hata jina moja, pamoja na kwamba yeye ndo msimamizi mkuu wa usalama wa raia na mali zao...unamhitaji mtu wa aina hii kuongoza wizara nyeti km hiyo ili iweje?

Bahati mbaya viongozi wetu wengi huwaza ulaji, ndo sababu huwa ngumu sana kwao kuwajibika! Hata pale inapoonekana wazi kwamba wameshindwa kazi!
 
IMG_20170611_090327.jpg
 
Back
Top Bottom