Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,888
- 143,985
Japo inadaiwa kuwa kampuni husika imetupiga hela nyingi (bilion 5 mpaka 7 kwa mwezi) lakini ukweli ni kuwa walikuwa wanatupiga kupitia mikataba tuliyoingia nayo wenyewe huku tukiwa na akili zetu timamu (hizo hela hawajatupora kwa mtupu wa bunduki)
Kwahiyo, kama tumevunja mkataba kinyume na makubaliano, basi upo uwezekano wa hawa mabwana kutushita, wakatushinda na tukalazimika kuwalipa mabilioni ya hela kama fidia kwa kuvunja mkataba.
Vile vile ilikuwa busara watanzania tukaelezwa mkataba husika ulikuwa umebakiza muda gani kumalizika kwani wanasiasa wetu hawa huwa wanafanya maamuzi pengine bila hata kuwa na taarifa za kutosha kuhusu jambo husika.
Tusishangile ushindi wa uwanjani wakati huenda kanuni za mchezo zimekiukwa kwani wenzetu hawa wanaweza kuja kupata point za mezani.
Time will tell.