Sakata la Kagera: Simba SC tutatumia Dola Elfu 15 kuipeleka barua FIFA

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,768
7,258
Rais wa Simba, Evans Aveva anasema wanakamilisha taratibu za mwisho ikiwemo kupata barua kutoka bodi ya ligi ya kupokwa point 3 za Kagera sugar ili wakwee pipa kuelekea Zurich, Uswizi kunako makao makuu ya FIFA kukata rufaa ambapo itawagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 15,000.

Nini maoni yako kuhusiana na sakata hili?

=====

Baada ya Kamati ya maadili na hadhi za wachezaji kuipoka klabu ya Simba SC alama tatu ilizopewa na kamati ya saa 72, rais wa klabu ya hiyo, Evans Aveva amezungumza na waandishi wa habari hii leo na kuelezea maamuzi ya klabu hiyo.

Aveva amesema Simba SC wanaonewa katika hilo na kamwe hawawezi kulikalia kimya swala hilo, na kwa sasa wanangoja barua ya maandishi kutoka kwenye bodi ya shirikiso la soka nchini, TFF, ili kulipeleka swala hilo kwenye shirikisho la soka duniani, FIFA pamoja na kulipeleka suala hilo katika mahakama ya michezo CAS.

Kuhusiana na maamuzi hayo yaliyotolewa na TFF kupitia kwa katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa, TFF walishasema Simba haiwezi kukata rufaa tena.

Wao kama Simba Sc wanaona alama tatu ni mali yao, na hivyo kuna mkanganyiko kati ya Bodi na kamati ya haki na hadhi za wachezaji, na kwao wanajua kadi tatu zilikuwepo kwa kuwa hakuna kamati hata moja inayopinga suala hilo.

Swala lingine ambalo Rais Aveva amelizungumzia ni juu ya mchezo wao wa fainali kati ya Simba Sc dhidi ya klabu ya Mbao Fc, na kusema kuwa wanaomba waendeshaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini wake kupewa heshima inayoambatana na mashindano kwa kuwa ni makubwa na yanatoa mshiriki wa kimataifa na hivyo kuna umuhimu wa kutoa ratiba ya mapema na sio kuchelewa kutoa ratiba ya Viwanja.

Amesema hawana tatizo na Dodoma na watatungulia huko mapema kwani wanaiheshimu sana Mbao Fc ila kamwe hawaiogopi na wapo tayari kucheza hata wangepangiwa kiwanja chochote.

Chanzo: Bongo 5
 
Kanuni zilizowekwa kuongoza ligi lazima zifuatwe vinginevyo haki lazima itafutwe kwenye vyombo vya juu vya mchezo wa soka.
 
Acha waende tu.

Wao walimtumia mchezaji mwenye kadi tatu Kombe la FA dhidi ya Polisi

Rufaa ya Polisi ilitupwa kwa kuwa nje ya muda na haikulipiwa! Sababu hizo hizo zilitumika kurejesha point za Kagera

Polisi washauriwe kwenda FIFA maana mashauri yao yanafanana. Simba haikustahili kuendelea Kombe la FA kwa maana hiyo!
 
Acha waende tu.

Wao walimtumia mchezaji mwenye kadi tatu Kombe la FA dhidi ya Polisi

Rufaa ya Polisi ilitupwa kwa kuwa nje ya muda na haikulipiwa! Sababu hizo hizo zilitumika kurejesha point za Kagera

Polisi washauriwe kwenda FIFA maana mashauri yao yanafanana. Simba haikustahili kuendelea Kombe la FA kwa maana hiyo!
Polisi nao waende FIFA
 
Sasa kama mnatumia fedha nyingi kwenye ligi alafu kuna timu ya kupewa ubingwa si bora haki itafutwe kwingine.
 
Yule mwesigwa ndio alichemka kabisa. Alikiri mchezaji Fakhi alikuwa na kadi tatu na akaamuru akakosa mchezo unaofuata wa Kagera hahahhaa tanzania kuna mapicha picha ya kifala sana.
 
Acha waende tu.

Wao walimtumia mchezaji mwenye kadi tatu Kombe la FA dhidi ya Polisi

Rufaa ya Polisi ilitupwa kwa kuwa nje ya muda na haikulipiwa! Sababu hizo hizo zilitumika kurejesha point za Kagera

Polisi washauriwe kwenda FIFA maana mashauri yao yanafanana. Simba haikustahili kuendelea Kombe la FA kwa maana hiyo!
Hili nalo neon, tabu labda hizo dola 15,000/=
 
Aveva anza kufunga virago , hatutakubali kudanganywa kishamba namna hiyo , huyo Julio anakuingiza kingi akulie hela zako tu , muulize Kajumulo .
 
Wangetumia dola hizo kwenye mazoezi si wangeshinda mechi zote? Hana jipya nae huyo Aveva.
 
Wanasema mfa maji hakosi kutapatapa kwa hiyo tusishangae sana ......
 
Hili jambo litaidhalilisha sana TFF huko mbele.
Hakuna atakaye dhalilika kwenye hili suala.

FIFA wakipata barua ya simba, wataomba maelezo kutoka TFF ya namna suala lilivyoshughuliliwa na TFF.

TFF wakisema kuwa kuna kanuni imevunywa kwenye uwasilishaji wa Rufaa, hapo simba hawana chao tena!
 
Back
Top Bottom