Kumbukumbu za bunge zinaonesha kuwa hoja ya Mh Sendeka kuhusu kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza sakata la Jairo iliungwa mkono baada ya kutolewa lakini haikuafikiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge!
Licha ya Naibu Spika kurejea kuisoma kanuni kabla ya kuamua,hakuwahoji wabunge ili hoja iafikiwe au la, kama kanuni inavyotaka mara baada ya hoja kutolewa na kuungwa mkono.inawezekana alipitiwa kutokana na jazba au ni usanii,lakini vyovyote iwavyo kamati teule iliyoundwa si halali kwakuwa haikuridhiwa na bunge.kwa maana hiyo serikali inaweza ikaikataa repoti ya kamati hiyo endapo itagundua mapungufu yanayoidhalilisha.
Licha ya upungufu huo wa kikanuni vile vile kamati teule pia inakwenda kwenye uchunguzi ikiwa inajua aliyewatuma (bunge) anataka nini, hivyo basi kwa kuwa wao pia ni sehemu ya bunge watakuwa kama mshtaki,muendesha mashata na jaji.
Tafakari!!!!!!