mkulu senkondo
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,857
- 3,561
Hatimaye lile sakata la faru john limefikia patamu baada ya kamati iliyokuwa imeundwa na waziri mkuu Ndugu majaliwa kassim majaliwa kumaliza uchunguzi wake na kuweka matokeo mujarabu kuhusu sakata la mnyama huyo adimu! Taarifa ya kamati inaeleza kuwa baada ya kufanyika uchunguzi wa sampuli za vinasaba vya faru huyo huko afrika ya kusini, inebainika kuwa ni kweli faru John ndie aliyekufa na sio faru hadija ambaye ni shemeji wa faru john kama ambavyo ilidaiwa hapo awali. Pia kamati hiyo imetoa mapendekezo kadhaa kuhusu sakata hilo na rungu hilo linaonekana kuwaangukia maofisa wa tanapa sambamba na viongozi wa wizara husika.