Sakata la Escrow: Hawa wawe makini na usalama wao

Hata wewe pangupakavu ulianzisha uzi huu upo hatarini kwa kuwa uchinguzi wewe umewapa tahadhari walengwa. Angalia nyendo zako na ikiwezekena linda sana kucha na meno yako.
 
mtu alouza roho hapa ni kafulila zito na mengi wana sekiurit ya kutosha mkono hakulishwa sumu alitoa hizi habari ili kuendelea kulitia chumvi hili jiishu
 
Hakna lolote ukweli ndio adui yao mkubwa,usigope mkuu....tupo nyuma yao tutawatetea,watamuua mmoja hawawezi kuwaua wote,na huyo mmoja hadi sasa wamechelewa sawa
 
pangupakavu, Umejiunga JF tarehe 25/11/2014 kwa maneno mengine umeiunga baada ya sakata
la ESCROW kushika kasi. Maswali yangu kwako...

1. Nini malengo yako mkuu?
2. Wewe ni nani anayekutumia??
3. Sakata la Escrow likiisha utaendelea kuwepo hapa JF???
 
Mkuu yaani unadata kweli; ila umesahau kujitaja na wewe mwenyewe uko hatarini.unajilinda vipi? Kama una vaa buret proof wape wenzako pia mkuu
 
Zitto Kabwe
PAC inawahakikishiaWatanzania kuweka ukweli wote kuhusu uchunguzi wa akaunti ya ‪#‎ TegetaEscrow‬. Tutawasilisha ripoti yetu Bungeni kesho mara baada ya kipindi cha maswali.
Narudia, tutatenda Haki. Aliyemo hatutamtoa na asiyekuwemo hatutamwingiza.Mola atuongoze katika kutenda Haki, kusema kweli na kweli tupu
1 hr·
 
Wakuu,

Katika kuhakikisha tunapambana na ufisadi unaolitafuna taifa, kuna wengine hugeuka mbuzi wa kafara.

Ningependa kuwapa hadhari kubwa hawa wafuatao kwakuwa wapo kwenye hatari zaidi. Hatari hii itapungua (haitaisha) baada ya ripoti kusomwa Bungeni lakini baada ya hapo kuna watakaoendelea kutaka kulipiza kisasi.

1. Nimrod Mkono (hata baada ya kunusurika bado anasakwa, wao wanaamini ni kinara dhidi ya kinachoendelea sasa)
2. David Kafulila (Wanaamini huyu anatumiwa na Zitto, Mengi na Mkono katika kufikia malengo)
3. Zitto Kabwe (Wanaamini bila nguvu ya ziada ya huyu mtu sakata hili lingepotelea hewani, wameshafanya mashambulizi ya kimkakati kwake na watajwa hapo juu bila ufanisi mkubwa)
4. Reginald Mengi (Huyu pamoja na kuwa wengi wanadhani ni vita yake dhidi ya Muhongo kama ambavyo propaganda zimekuwa zikieleza; bado hadi namba moja anaamini jamaa anahusika kuiangusha serikali yake kwa kutumia vyombo vyake vya habari na wanasiasa)
5. Mhariri wa The Citizen (Hawa wamekuwa mwiba mkali katika sakata hili, wao wanasema hawa watu ni tatizo na ni vyema wapunguzwe makali. Lolote linaweza kufanywa, umakini kwa mhariri ni muhimu sana kwa wakati huu)
6. Mhariri mkuu (admin) wa JamiiForums (Inadaiwa hapa JF zimekuwa zinaanzishwa thread zinapigwa pini wakati zilikuwa zikilenga kupoza nguvu ya sakata hili. Wao wanaamini JF inasomwa sana na kitu kikianzia JF kinakuwa viral; kuzuiliwa kwa mijadala yao kunaonekana kuwakera na tahadhari ni muhimu kwa mhusika).

Ifahamike kuwa, mashambulizi yao hayatakuwa ya moja kwa moja kama wengi wanavyodhania. Mashambulizi ya kibaiolojia huenda yakatumika.

Nimetoa tahadhari hii mapema na niwashauri wahusika kutopaniki sana bali kuwa makini zaidi katika kipindi hiki.

Taarifa hizi ni za ndani na atakayezipuuza asilaumu kwa matokeo mabaya kwake. Tulimwonya mara 3 Nimrod hadi tukamfata Airport kumjulisha kuwa tahadhari yetu ni ya kweli, aliyaona matokeo. Na aliyemfanyia hivyo anamjua vema.

Pangu pakavu

======
UPDATES:

acha kuwatishia wapambanaji hakuna wa kuwazuru,uoga wako ndio umasikini wako
 
Back
Top Bottom