Sakata la Escrow: Hawa wawe makini na usalama wao

pangupakavu

New Member
Nov 25, 2014
2
0
Wakuu,

Katika kuhakikisha tunapambana na ufisadi unaolitafuna taifa, kuna wengine hugeuka mbuzi wa kafara.

Ningependa kuwapa hadhari kubwa hawa wafuatao kwakuwa wapo kwenye hatari zaidi. Hatari hii itapungua (haitaisha) baada ya ripoti kusomwa Bungeni lakini baada ya hapo kuna watakaoendelea kutaka kulipiza kisasi.

1. Nimrod Mkono (hata baada ya kunusurika bado anasakwa, wao wanaamini ni kinara dhidi ya kinachoendelea sasa)
2. David Kafulila (Wanaamini huyu anatumiwa na Zitto, Mengi na Mkono katika kufikia malengo)
3. Zitto Kabwe (Wanaamini bila nguvu ya ziada ya huyu mtu sakata hili lingepotelea hewani, wameshafanya mashambulizi ya kimkakati kwake na watajwa hapo juu bila ufanisi mkubwa)
4. Reginald Mengi (Huyu pamoja na kuwa wengi wanadhani ni vita yake dhidi ya Muhongo kama ambavyo propaganda zimekuwa zikieleza; bado hadi namba moja anaamini jamaa anahusika kuiangusha serikali yake kwa kutumia vyombo vyake vya habari na wanasiasa)
5. Mhariri wa The Citizen (Hawa wamekuwa mwiba mkali katika sakata hili, wao wanasema hawa watu ni tatizo na ni vyema wapunguzwe makali. Lolote linaweza kufanywa, umakini kwa mhariri ni muhimu sana kwa wakati huu)
6. Mhariri mkuu (admin) wa JamiiForums (Inadaiwa hapa JF zimekuwa zinaanzishwa thread zinapigwa pini wakati zilikuwa zikilenga kupoza nguvu ya sakata hili. Wao wanaamini JF inasomwa sana na kitu kikianzia JF kinakuwa viral; kuzuiliwa kwa mijadala yao kunaonekana kuwakera na tahadhari ni muhimu kwa mhusika).

Ifahamike kuwa, mashambulizi yao hayatakuwa ya moja kwa moja kama wengi wanavyodhania. Mashambulizi ya kibaiolojia huenda yakatumika.

Nimetoa tahadhari hii mapema na niwashauri wahusika kutopaniki sana bali kuwa makini zaidi katika kipindi hiki.

Taarifa hizi ni za ndani na atakayezipuuza asilaumu kwa matokeo mabaya kwake. Tulimwonya mara 3 Nimrod hadi tukamfata Airport kumjulisha kuwa tahadhari yetu ni ya kweli, aliyaona matokeo. Na aliyemfanyia hivyo anamjua vema.

Pangu pakavu

======
UPDATES:
Habari MPASUKO
Wanajamvi saa dkk hii nipo makao Makuu Polisi dodoma tukiwa na Mh Kafulila na Mh Mnyaa na Mh machali
Kilichopo Mh Kafulila ametumiwa ujumbe ambao ameambiwa sifa zake hizo bila kujuwa uwezo wa anaopambana nao mwisho wa uhai wake ni leo Kesho ataongea kaburini
Hali inatisha!!
Ndg zangu tuombeeni duwa hali no ngumu sana.
Nipo hapa kutimiza jukumu kama naibu w/kivuli mambo ya Ndani
Nimepewa jukumu hili na huyu bw Ndio namuendesha kwenye GARI langu binafsi
Jamani ndg zangu duwa zenu ni muhimu kuliko chochote kwa huu.

Mh Khatib a.k.a Obama Mbunge wa Konde
 
Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
hahahhhahahahaha...watanzania bana...sasa inawezekana vipi mtu yule yule ajidhuru yeye? Think Outside the box...
 
MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,788
1,500
Kwa wenye akili huwa wanaweka maneno yote akilini maana hujui ukweli ni upi. Uki unganisha nukta unaona kuna haja.
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,920
2,000
Wakuu,
Katika kuhakikisha tunapambana na ufisadi unaolitafuna taifa, kuna wengine hugeuka mbuzi wa kafara.
Ningependa kuwapa hadhari kubwa hawa wafuatao kwakuwa wapo kwenye hatari zaidi. Hatari hii itapungua (haitaisha) baada ya ripoti kusomwa Bungeni lakini baada ya hapo kuna watakaoendelea kutaka kulipiza kisasi.
1. Nimrod Mkono (hata baada ya kunusurika bado anasakwa, wao wanaamini ni kinara dhidi ya kinachoendelea sasa)
2. David Kafulila (Wanaamini huyu anatumiwa na Zitto, Mengi na Mkono katika kufikia malengo)
3. Zitto Kabwe (Wanaamini bila nguvu ya ziada ya huyu mtu sakata hili lingepotelea hewani, wameshafanya mashambulizi ya kimkakati kwake na watajwa hapo juu bila ufanisi mkubwa)
4. Reginald Mengi (Huyu pamoja na kuwa wengi wanadhani ni vita yake dhidi ya Muhongo kama ambavyo propaganda zimekuwa zikieleza; bado hadi namba moja anaamini jamaa anahusika kuiangusha serikali yake kwa kutumia vyombo vyake vya habari na wanasiasa)
5. Mhariri wa The Citizen (Hawa wamekuwa mwiba mkali katika sakata hili, wao wanasema hawa watu ni tatizo na ni vyema wapunguzwe makali. Lolote linaweza kufanywa, umakini kwa mhariri ni muhimu sana kwa wakati huu)
6. Mhariri mkuu (admin) wa JamiiForums (Inadaiwa hapa JF zimekuwa zinaanzishwa thread zinapigwa pini wakati zilikuwa zikilenga kupoza nguvu ya sakata hili. Wao wanaamini JF inasomwa sana na kitu kikianzia JF kinakuwa viral; kuzuiliwa kwa mijadala yao kunaonekana kuwakera na tahadhari ni muhimu kwa mhusika).
Ifahamike kuwa, mashambulizi yao hayatakuwa ya moja kwa moja kama wengi wanavyodhania. Mashambulizi ya kibaiolojia huenda yakatumika.
Nimetoa tahadhari hii mapema na niwashauri wahusika kutopaniki sana bali kuwa makini zaidi katika kipindi hiki.

Taarifa hizi ni za ndani na atakayezipuuza asilaumu kwa matokeo mabaya kwake. Tulimwonya mara 3 Nimrod hadi tukamfata Airport kumjulisha kuwa tahadhari yetu ni ya kweli,&! aliyaona matokeo. Na aliyemfanyia hivyo anamjua vema.

Pangu pakavu
Na wewe uwe makini hatukawii kusikia umejidumbukiza kisimani.
 
rpg

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
3,512
2,000
Kweli kwako pakavu, tahadhari ni muhimu sana. Hii ni vita kubwa dhidi ya wanaofikiri wao ndio wenye nchi.
 
majorbuyoya

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,830
1,225
......Hao wote wawadhuru lakini wakimduru Moderator Mkuu wa JF, kwa kweli tutamchuna mtu ngozi!!
 
MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,788
1,500
Namba 6 sikubliani nayo.

Anyway sijui unatumia criteria gani kutoamini, ila nilisikia mkono aliambiwa awe makini, kuna watu walimtonya. Sasa kwa nini isiwe kwa jf? Angalia ni issue ngapi nzito zilizotikisa nchi zilianzishiwa hapa jf? Ndipo tunasema, sikiliza, chunguza na ikiwezekana fata ushauri.
 
Noel france

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
910
1,000
......Hao wote wawadhuru lakini wakimduru Moderator Mkuu wa JF, kwa kweli tutamchuna mtu ngozi!!
kwani moderator wa jf unamfahamu? je ukiambia moderator wa jf ni job ndugai ama bi kiroboto ama la le mutz mtoto wa malecela! je utakubali kuyaramba matapishi yako
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Mafisadi ni maharamia, na mafia, wanatumia kila aina ya silaha kuangamiza au kuua sio kazi kwao!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom