Sakata la Dr Ulimboka,kama Saed Kubenea anaweza kutoa data polisi, usalama wa taifa wanafanya nini?

Status
Not open for further replies.

Seif al Islam

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
2,156
638
Nilishangazwa sana na uwezo wa mwandishi mwandamizi wa gazeti la mwanahalisi bwsaed kubenea kupata, kuharir na hata kutoa bila woga wowote taarifa nyeti za mawasiliano ya watuanaodai wanahusika na kupigwa kwa dr ulimboka. Nilishindwa kuelewa namna anavyoweza kunasa mawasiliano yale na kuyapanga vyema vile.

Nilishindwa pia kujua namna anavyoweza kujipenyeza ndani ya idara ya usalama wa taifa na kupata taarifa muhimu ambazo jeshi la polisi na usalama wa taifa wanashindwa kuzipata na kuishia kutoa maigizo ya kitoto kwenye tv.sasa najiuliza kama kweli taasisi hizi za serikali zinashindwa kupata taarifa ambazo mtu binafsi anaweza je ikitokea serikali nyingine ya nje ikapanga jambo baya juu ya taifa ketu hawa usalama na polisi wanaweza kugundua?

Na je kama ndo wachovu hivyo nchi yetu muda huu ipo hatarini kwa kiwango gani?
 
Jamani mwenye huo uzi wa Kubenea aumwage hadharani. Nimejaribu kutembelea wavuti ya mwanahalisi ili nijisomee mwenyewe kwa macho yangu nikakumbana na ujumbe kuwa iko kwenye matengezo!
 
Tanzania hakuna usalama wa Taifa, kuna usalama wa CCM na serikali ambao ndio hao TISS
 
KUBENEA jasiri sana... Go on Kubenea and God be with all the way...
 
Status
Not open for further replies.
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom