Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Haya maneno mazito sana mkuu Kyoma, karibu tena baada ya kupotea sana mkuu, hii yako ndio tunaita kukata mzizi wa fitina:-

Quote: Kyoma

"Je tuamini nini kati ya haya mawili

1. Ujumbe ambao Texas Medical Board walimpa Mzee Kuhani kwa njia ya simu na akaumwaga hapa JF?

Au

2. Sheria za Texas na Kanuni za Texas Medical Board walizoziweka kwenye mtandao wao?

Je katika hatua za mwanzo kati yako na wanasheria, mnatumia vigezo ambavyo Texas Medical Board walikueleza kwenye simu au mnatumia official documents ambazo Texas Medical Board imeziweka katika mtandao wake?"
 
Tuwe waangalifu kuamini robots waliowekwa kujibu simu kwenye institutions hata katika nchi zilizoendelea. Ninawaita "robots" kwa sababu mara nyingi ukiwauliza swali linalohitaji a little bit of thinking watakujibu - I HAVE NO IDEA. Wamekuwa trained kufanya kazi in a certain way, kwahiyo ukizungurusha kidogo mambo unakua umemmaliza, na kwa kuwa anajiamini ataishia kukuambia chochote mradi amalizane na wewe.

Hizi ndio dizaini za watu ambazo unaweza ziuliza kama unaweza tumia passport yako kama identification na jibu watakalokupa ni kwamba passport is not an ID, kwa kuwa wao wamezoea tumia state IDs ama drivers' license kama form of ID. This happened to me niliposimamishwa na askari polisi wiki ya mwanzoni nilipofika Marekani nikiwa sijapata bado kitambulisho cha huko na polisi akakataa kabisa kukubali passport yangu kama form of identification.

Sijasema kwamba tusiamini yaliyosemwa na mtumishi wa bodi hiyo, ila ninamaanisha kwamba inabidi tuwe waangalifu kidogo tunapo-digest information from people who might not know what they're doing.
 
Mzee Nyani Ngabu, heshima yako Mkuu!

Nakubaliana kabisa na hoja yako. Katika verification process, hatua ya kwanza kabisa ni kupata maoni ya wahusika wakuu. Nadhani Mwanakijiji anaweza kutusaidia kwa hili, kwani aliwahi kumhoji Dr. Masau. Lakini wahusika wasipopatikana, haiwezi kuzuia process yenyewe. Ila lazima tuwe waangalifu tusije tukawa tunatengeneza hypothesis, alafu tunazijengea hoja na kufikia conclusion bila supporting logic, fact and evidence.

Niliwahi kusoma bandiko lako moja nikapata picha kama vile uko Marekani (kama siyo nisamehe Mzee). Kuna chain stores katika Jimbo la Texas zinaitwa Fiesta. Hawa jamaa waliwahi kupata hasara kwa sababu program zao za Computer zilipata kizungumkuti. Fikiria mtu anatoa dola mia na amenunua kitu cha dola tano. Utamrudishiaje dola miambili?
Sales representatives (cashiers) wao walikuwa wanarudisha chenji kubwa kuliko stahiki. Computer na Calculator zimewalemaza, hivyo screen ikimwambia mteja arudishiwe dola miambili anampa, hata kama amepokea dola mia. Naamini kabisa Mzee Kuhani alipiga simu Texas Medical Board. It depends, kama alimkuta kimwana wa schedule (nadhani unanielewa), atamwambia nipe last name na first name.

Wakati mwingine unaweza kumkuta hata Dr. aliyeajiliwa na Board. Na mara nyingi waajiliwa wa Texas Medical Board ni madaktari. Lakini daktari anaweza kwenda zaidi ya kimwana, na kukuuliza kama una date of birth na social security number ya muhusika. Hata hivyo, Computer ikimwambia sioni kitu, naye atakueleza vivyo hivyo. Tena umekwisha kumwambia watu wengi wamekufa. Lo!

My point ni kwamba ni vizuri kufanya utafiti wako kwanza ili uweze kuhodhi kitu unachouliza. Unaweza kujaribu hata hiyo namba aliyoitoa Mzee Kuhani utapata haya niliyokueleza. Lakini ukijibiwa uliza maswali kidogo tu kwamba, mbona sheria namba fulani inasema hivi na hivi, alafu wewe unanieleza vingine. Utasikia tone inabadilika na anaweza hata kukuweka on hold.

Vitu vingine tunamhitaji Dr. Cooley na Dr. Masau kutia neno, lakini mambo mengine inabidi tutafiti na kusoma wenyewe kwa sababu yako wazi. Sasa Dr. Masau na Cooley wakikwambia kuwa alifanya upasuaji na hakuwa na Physician-In-Training Permit, kwani hakupashwa kuwa nayo, utarudi tena Texas Medical Board kufanya verification ya statements zao?

Ndiyo maana official documents zimewekwa wazi ili watu wazisome. Kama umekwisha ziperuzi na ukaamua kuwavaa wahusika wote, utakuwa na mashiko yasiyo legevu kama asemavyo Mzee Masatu. Ama sivyo watakupigisha danadana, na unajua wamarekani hawakawiagi kutoa majibu ya mkato hasa wakigundua hujuhi undani wa kitu unachododosa. Na lazima tuelewe kuwa wamarekani wengi mambo ya msingi yanawapiga chenga kwa sababu yakupenda spoon feeding.

Piza, programs za TV nakadhalika ni simu tu, yaani wanaweka reciever sikioni wakisubili jibu la mwisho kutoka upande wa pili. Angalia inavyowagharimu katika chaguzi za Rais kwa sababu ya kuacha vyombo vya habari vifanye utafiti na vifikiri kwa niaba yao. Wanakuwa kama vibogoyo wa akili wakingoja kumeza tu.

Hata hivyo wadau wengi wa JF ni watafutaji ndiyo maana nampongeza Mzee Kuhani kwa hatua aliyofikia. Ushauri ni kwamba asitegemee wao kumtafunia kila kitu. Hawatafanya.

Mzee wewe nakuaminia sana. Na wala hujakosea. Mimi nipo hapa Marekani. Umenifurahisha sana kwa jinsi ulivyofuatilia jambo hili na jinsi ulivyoshusha hoja zako hapa zikiambatana na vidhibiti vya vifungu vya sheria na timeline ya masomo ya Dk. Masau chronologically. Hivi ndivyo watu (bloggers, waandishi, wachunguzi, n.k.) wanavyotakiwa kufanya kabla hawajatoa tuhuma nzito kama hizi. Na kwa nyepesi nyepesi nilizopenyezewa najua wewe huhitaji kupiga simu katika kufuatilia suala hili. Ni kiasi cha kuweka appointment ya ana kwa ana tu na mhusika/ wahusika....Lol.
 
Tuwe waangalifu kuamini robots waliowekwa kujibu simu kwenye institutions hata katika nchi zilizoendelea. Ninawaita "robots" kwa sababu mara nyingi ukiwauliza swali linalohitaji a little bit of thinking watakujibu - I HAVE NO IDEA. Wamekuwa trained kufanya kazi in a certain way, kwahiyo ukizungurusha kidogo mambo unakua umemmaliza, na kwa kuwa anajiamini ataishia kukuambia chochote mradi amalizane na wewe.

Hizi ndio dizaini za watu ambazo unaweza ziuliza kama unaweza tumia passport yako kama identification na jibu watakalokupa ni kwamba passport is not an ID, kwa kuwa wao wamezoea tumia state IDs ama drivers' license kama form of ID. This happened to me niliposimamishwa na askari polisi wiki ya mwanzoni nilipofika Marekani nikiwa sijapata bado kitambulisho cha huko na polisi akakataa kabisa kukubali passport yangu kama form of identification.

Sijasema kwamba tusiamini yaliyosemwa na mtumishi wa bodi hiyo, ila ninamaanisha kwamba inabidi tuwe waangalifu kidogo tunapo-digest information from people who might not know what they're doing.

Sio pasipoti hawakuikubali, bali walitaka uwape kitu chenye kuthibitisha address yako kama bank statement au Driving Licence, kama hawakuibali pasipoti yako kama form of of ID mbona ulipita AIRPORT kwa pasipoti hiyo hiyo? au ulienda kwa Meli?

hata kama ni Robot lakini wanajua kuwa Masau hawaku mwanafunzi wao.
 
kituko cha TANZANIA DAIMA wikiendi hii:

Ok inawezekana ikawa mara moja ni bahati mbaya...lakini huyu mwandishi wa gazeti la Mbowe akakisha likaendelea kuonyesha ujinga na uvivu wa kufikiri na kufanya research kwa kudai hivi:

UKWELI WA NANI MWENYEKITI WA BODI YA NSSF HUU HAPA:

http://www.nssf.or.tz/board_of_trustees.php

Jamani tuache ushabiki halafu tuangalie hili gazeti FREEMAN MBOWE LINAVYOOAJIRI makanjanja

hivi huyu kweli ndio Dr MUSSA HASSAN au kajibadilisha?
b_nyoni.gif

Mrs. Blandina Nyoni
Board Chairperson
National Social Security Fund
Dar es salaam

hivi wanashindwa kuingia JAMII FORUMS kutafuta referencing kama KUBENEA na MWANAHALISI?

What a shame!
Mwanakijiji anakesha hapa JF na kaleta habari yenye utata mkubwa kuwa Professor Mtulia ndiyo Board memba wa NSSF,Tusiwalaumu Tanzania Daima wala KlhNews kwa vile wako kwenye MKAKATI Maalum wa kupotosha na wanatusisitizia kuwa 'MKIMKOROFISHA MASAU ATAAMUA KUFUNGA TAASISI YAKE NA KURUDI MAREKANI KWANI WABONGO HAWANA MPANGO WALA SHUKRANI'
swali atarudi vipi Marekani wakati hana kibali cha kuishi MAREKANI?
 
Mkuu, kweli una nia ya kujenga hoja au unaandika kufurahisha baraza? Sithani kama kuna daktari wa "Moyo" mwenye reference ya Dr Masau atakayepata shida kuingia na kufanya kazi USA iwapo atakuwa na nia hiyo.
 
Muungwana Kyoma,

Hayo mabandiko yako ndo tunayaita critical analysis! Watu hapa wanakuja na data za kupika pika..simply because wako against initiatives za mtu.

Dr. MASAU anaweza kuwa hajalipia pango la NSSF..lakini sikubaliani na hii njia ya kumtuhumu as if alifanya kosa la jinai kuanzisha ile taasisi. Eti jamaa hana qualifications? hicho kibali cha upasuaji na kuanzisha taasisi alipewa na nani?

Mkuu mengi umenyaongea sina haja ya kuyarudia, naomba ni kushukuru kwa uchambuzi makini na wa kiutu uzima!

Its a shame watu wanapoishiwa hoja kuanza kuattack personality za watu.
 
b_nyoni.gif

Swali langu liko pale pale, mnakubali kama mnavoambiwa na gazeti la TANZANIA DAIMA kuwa huyu ndiye chairman wa bodi ya NSSF bwana DR MUSSA HASSAN?

Hivi kweli huyu anafanana na nani?
 
Sio pasipoti hawakuikubali, bali walitaka uwape kitu chenye kuthibitisha address yako kama bank statement au Driving Licence, kama hawakuibali pasipoti yako kama form of of ID mbona ulipita AIRPORT kwa pasipoti hiyo hiyo? au ulienda kwa Meli?

hata kama ni Robot lakini wanajua kuwa Masau hawaku mwanafunzi wao.

You didn't get me right mtaalam. Proof ya address wanaihitaji for what in a city like New York ambako kuna watalii mamilioni kila siku? Nilikua naingia kwenye subway siku ambayo threat level ilikuwa orange, so kulikuwa na random check-up kwa wasafiri. Huyo polisi alikua hajawahi kuona kitu kinachoitwa passpoti, na aliponi-refer kwa mwenzie huyo mwenzake akacheka tu baada ya kujua mwenzie alivyobofoa. I hope you got me right now...
 
Mzee Kuhani, heshima yako Mkuu!

Kwanza hongera sana kwa juhudi unazozionyesha za kupeleleza, kuchokonoa na kutafuta ukweli kuhusu uhalali wa utaalamu wa Dr. Masau. Pili, post # 995 uliandika:

“I spoke again with the Texas Medical Board (512) 305 7010). Masau never obtained a physician-in-Training permit. He is nowhere to be found in Texas Board computers. Meaning, he probably had no business being at the Texas school. So, as I said, it's now potentially a legal matter pointing at Texas Heart Institute”

HISTORIA YA PHYSICIAN-IN-TRAINING PERMIT

Mwaka 1996, Federation of State Medical Boards of the United States, ilitoa wito kwa majimbo yote kuanzisha utaratibu wa kuwadhibiti na kuwawajibisha wanafunzi na madaktari wanaojifunza kwa matendo (Residents and Fellows). Mpaka mwaka 2004, Texas haikuwa na utaratibu wa Physician-In-Training Permit.

Badala yake ilikuwa na mpango wa Institutional Permit, ambapo Texas Medical Board ilitoa Permit kwa chuo tu, na si kwa Residents and Fellows. Computer za Texas Medical Board zilikuwa na majina ya vyuo na si majina ya Residents and Fellows. (Refer to pdf attachment # 1: pages 1, 2, 6 and 5 – evidence highlighted in Yellow).

Mwaka 2001, Bunge la Texas liliridhia maombi ya Texas Medical Board na kutunga sheria Texas Occupations Code, iliyoifanyia marekebisho Texas Medical Practice Act-1999. Ibara ya 155 fasihi ya 105 kifungu kidogo (a), ya sheria hiyo iliipa mamlaka Texas Medical Board kubadilisha kanuni zake kwa kuanzisha rasmi Physician-In-Training Permit. (Refer to pdf attachment # 2: page 11 – evidence highlighted in yellow). Hii sheria inapatikana katika mtandao wa Texas Medical Board, chini ya Texas Statutes - Texas Occupation code. Tafuta chapter 155 - License to practice medicine. http://www.tmb.state.tx.us/rules/codes/mpa.php

Kutokana na maagizo ya sheria ya Texas Occupational Code 155.105, iliyotungwa na Bunge la Texas mwaka 2001, Mwaka 2004 Texas Medical Board ilitunga kanuni ya 171 fasihi1 (Chapter 171.1) kuanzisha rasmi Physician-In-Training Permit,. Halikadhalika ibara ya 171.5 ilibadilisha utaratibu wa Institutional Permit kwenda Physician-In-Training Permit.

Kanuni ya 171.1 na 171.5 zinatamka bayana kwamba “The provisions of this 171.1 & 171.5 adopted to be effective November 7, 2004. (Refer to pdf attachment # 3: pages 1 & 6 – evidence highlighted in yellow). Kanuni hii inapatikana katika mtandao wa Texas Medical Board, chini ya Board Rules and guidelines. Kwenye mtandao kanuni hii iko katika kurasa za 58-62. Ni jumla ya kurasa 243, lakini mimi nimenyofoa zinazohusu mada hii tu. http://www.tmb.state.tx.us/rules/rules/bdrules.php

Dr. Masau alianza Fellowship Program in Cardiovascular Surgery chini ya Sponsorship ya University of Texas Health Science Center-Houston mwaka 1997 mpaka Juni 2000.

Swali: Texas Medical Board wameka wazi kwenye mtandao wao sheria za Texas (Texas Statutes) na kanuni za bodi (Board Rules) – Visit website or pdf attachment #s 2 & 3. Sheria hizi zinaonyesha mambo makuu mawili.

  • Kipindi cha 1997 – 2000, ambapo Dr. Masau alikuwa Trained, ni University of Texas ilivyopashwa kuwa na Institutional Permit kutoka Texas Medical Board.
  • Kipindi cha 1997 – 2000, Dr. Masau hakupashwa kuwa na Physician –In-Training Permit, kwani hakikuwepo na kitu kama hicho. Na kama angekuwa nayo ingekuwa ni kinyume cha sheria za Texas na kanuni za Texas Medical Board zilizokuwepo.
Je tuamini nini kati ya haya mawili

  • Ujumbe ambao Texas Medical Board walimpa Mzee Kuhani kwa njia ya simu na akaumwaga hapa JF? Au
  • Sheria za Texas na Kanuni za Texas Medical Board walizoziweka kwenye mtandao wao?
Je katika hatua za mwanzo kati yako na wanasheria, mnatumia vigezo ambavyo Texas Medical Board walikueleza kwenye simu au mnatumia official documents ambazo Texas Medical Board imeziweka katika mtandao wake?

Kwa ufupi, Mwaka 1984 mpaka 1989, Dr. Masau alisoma Faculty of Medicine of the University of Dar-es-Salaam - Muhimbili, siku hizi inaitwa Muhimbili University and Allied Health Sciences (MUHAS). Mwaka 1992 – 1995 alisoma Master of Medicine in Thoracic and Cardiovascular Surgery katika Hubei Medical University, mjini Wuhan na Residency ya upasuaji katika First Affiliated Hospital of Hubei Medical University. Sponsor wa China alikuwa Ministry of Science, Technology and Higher Education of Tanzania.

Alirudi Tanzania na kuajiliwa na Wizara ya Afya katika Hospitali ya Muhimbili. Baada ya mwaka mmoja wa kazi, yaani 1997, alipata Sponsorship kutoka University of Texas Health Science Center – Houston chini ya J-1 viza kwa ajili ya Cardiovascular Surgery Fellowship. Hiyo Fellowship ilifanyika kwa affiliate wa University of Texas ambaye ni Texas Heart Institute and Texas Children’s Hospital, ndani ya St. Luke's Episcopal Hopsital, chini ya uangalizi wa Dr. Denton A. Cooley.

Kuna tofauti kati ya Hospitali na shule. Texas Heart Institute siyo shule ni hospitali. Kama ilivyo kwa Chuo Kikuu cha Muhimbili na Hospitali ya Muhimbili. Kuna vyuo vina Hospitali zake na kuna vingine havina lakini vinatumia hospitali kubwa ku-train Residents and Fellows. Vyuo vikuu ndivyo vinawajibika kwa hizo programs. Hospitali kazi yao ni kutoa Madaktari bingwa kusimamia Residents and Fellows. Kwa ufupi, Residency and Fellowship maana yake ni kufanya matendo. Hakuna kitu kinaitwa kuangalia katika Residency and Fellowship.

Texas kuna taasisi sita za afya zisizoingilika kirahisi. Siyo rahisi hata kidogo kwa daktari yeyote kutoka popote pale duniani (hata ndani Marekani yenyewe) kupata Residency au Fellowship chini ya Sponsorship ya mojawapo kati ya University of Texas, Baylor College of Medicine au Texas A&M. Kadhalika kwa daktari yeyote kutoka popote duniani kupata ajira katika Texas Heart Institute and Children’s hospital, MD Anderson Cancer Center au Methodist hospital. Mgonjwa anayetibiwa katika hizi taasisi anakuwa na ngekewa kwa sababu anahudumiwa na mabingwa na gharama zake ni kubwa mno.

Nanukuu hotuba moja ya Rais Bush akieleza mambo aliyowahi kufanya Dr. Denton Cooley "(1). In 1955 he perfected the heart-lung Machine. (2). In 1956 he perfomed the first open-heart operation in the Southern United State. (3). In 1960 he introduced bloodless heart surgery. (4). In 1968 he perfomed the first successful heart transplant in the US. (5). In 1969 he implanted the first totally artificial heart in human"

Hakuna Mvumbuzi, Mwandishi wa vitabu, Bingwa wa upasuaji, Tajiri, na Rais wa Taasisi kubwa kama Texas Heart Institute and Children's Hospital Dr. Denton Cooley, anayeweza kudhamini na kuweka jina lake katika taasisi ya upasuaji iliyoanzishwa na mtu ambaye hajawahi kumuona anafanya upasuaji. Hizi taasisi nilizozitaja juu, siyo za vichochoroni na hazina njia ya mkato ya kuwaingiza watu kinyemela. Kuna watanzania wengi wana vipaji na wakipewa nafasi na mazingira mazuri ya kazi pamoja na vitendea kazi wataokoa maisha ya watu. Naamini Dr. Masau ni mmojawapo.

Tatizo analolipata Dr. Masau Tanzania ni ushindani wa kibiashara kati ya asasi ya Medical Tourism ya India, Lions Club na waandamizi wa Serikali ya Tanzania. Serikali ya Tanzania inapeleka wastani wa wagonjwa 100 kwa mwaka nchini India. Inawezekana gharama ya upasuaji wa Moyo India ni ndogo lakini asasi ya Medical Tourism (middleman), inaitoza Serikali ya Tanzania $ 11,000. kwa kila mgonjwa. Gharama za Dr. Masau ni $ 5000-6500 kwa mgonjwa.

Nadhani Dr. Masau tatizo lake siyo la kitaaluma bali ni uendeshaji wa kampuni. Hata Dr. Denton Cooley hakuanza kirahisi kama anavyoonekana. Aliwahi kufilisika na ku-faili bankruptcy. Hata Dr. Kairuki alivyorudi kutoka Ujerumani alipambana na upinzani na mazingira magumu ya bongo. Aliambiwa alikuwa anafanya utaperi Ujerumani na mambo mengine yasiyo na kichwa wala miguu. Kama Mungu angemfufua leo, angetabasamu kuwa kumbe kejeli zote alizokuwa anapata zimegeuka kuwa baraka kwa wengine. Ajabu, kuna Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu alichoanzisha au wanaotibiwa katika Hospitali aliyoanzisha, hawajuhi karaha alizokumbana nazo, au wengine wamesahau.

Dr. Masau anaweza asione matunda ya juhudi zake leo. Pia inawezekana asiwe hai wakati Taasisi yake inatimiza lengo alilokusudia. Ushauri wangu kwake asife moyo. Roma haikujengwa kwa siku moja.

Nimeambatanisha list ya Residency & Fellowship programs zinazoratibiwa na University of Texas Health Science Center-Houston. Coordinator wa sasa wa Program iliyomdhamini Dr. Masau anaitwa Dr. Doug Heidemann. (Refer to attachment # 4 –evidence highlighted).

Umeipeleka kwa KUHANI lakini iwafikie wengi waliounga mkono kwa jasho lao lote bila kuongeza juhudi za ushahidi.

Naomba tupitishe uamuzi kwamba wanaojitahidi kupindisha uhalali wa mtu kwa kutaka walipwe madeni ya nyumba humu JF, sasa wajiondoe kwa muda. Au wabadili hizo pseudonym maana wengine tutahitaji muda mrefu kuamini yoote watakayotoa mbele yetu baada ya hapa. Ni sifa mbaya kwa JF.

Kwa ujumla Ugomvi wa Dr Masau wengi mumeingizwa mjini bila kufahamu ulikoanzia. Tatizo ni la miaka mingi. Tangu Kontena la kwanza la vifaa vyake lilipoingia pale bandarini. Ilibidi hadithi ifike ikulu. Kibaya zaidi Wizara haina popote ilipowahi kutoa msaada.

Naona wekeni nguvu kwenye NSSF.
 
....hata huko NSSF........bado hiyo ripoti wanayoibandika haina credibility....mchezo wa kubandika bandika figures...huko ktk mashirika tumeuona sana tu unakumbuka........Postal Bank
 
Kyoma.

DR.Kairuki hakupata upinzani wowote na alikuwa na blessing kubwa ya Serikali na alitumia jina la Kanisa kama ndio wanaomiliki Hospital mwanzoni alificha sana kama ni mali yake aliisajiri kwa jina la MIKOCHENI MISSION HOSPITAL iliposimama vizuri ndio ikabadilika jina na kuwa KAIRUKI.

DR.HUSSIEN MWINYI amefanya kazi pale KAIRUKI kama daktari na Mwalimu hadi anapata unaibu waziri wa Afya,viongozi na familia zao walikuwa wakienda kutibiwa. kifupi Kairuki alipata timu nzuri ya kumshauri na alitumia vizuri neno MISSION.

Kyoma kama DR.Cooley ni tajiri basi amkopeshe mwanafunzi wake (Masau)ili alipe deni lake la pango kuliko kwenda kunyea debe Ukonga?

hujui historia ya mkocheni hospital,alichosema kyoma ni sahihi kabisa.baada ya kukataliwa ndio hakahamua kutumia kanisa ilikuanzisha hiyo hospitali
 
hujui historia ya mkocheni hospital,alichosema kyoma ni sahihi kabisa.baada ya kukataliwa ndio hakahamua kutumia kanisa ilikuanzisha hiyo hospitali
Alitumia jina la Kanisa ili apate misaada toka kwa wafadhili na kukwepa kodi hiyo ndio ilikuwa ujanja aliutumia Kairuki.
 
Mkuu, kweli una nia ya kujenga hoja au unaandika kufurahisha baraza? Sithani kama kuna daktari wa "Moyo" mwenye reference ya Dr Masau atakayepata shida kuingia na kufanya kazi USA iwapo atakuwa na nia hiyo.

Yebo yebo acha kupendelea kitu kwa vile ni kabila moja hata mimi natoka mkoa wa DR.Masau, kama ana uwezo wa kurudi Marekani angekwenda haraka kuliko kushinda kwenye press conference kuomba kusaidiwa Pango, unajua kuwa kuomba ni jambo la aibu labda uwe huna njia nyingine.

Naona wazi na dhahiri kuwa DR.Masau hana njia nyingine zaidi ya kuwekeza karata zake Tanzania,Marekani kuna wataalam wengi na vigumu kuweza kusettle na kama una ACT unprofessional vigumu kupata kazi hata kama una hizo sifa.
 
Umeipeleka kwa KUHANI lakini iwafikie wengi waliounga mkono kwa jasho lao lote bila kuongeza juhudi za ushahidi.

Naomba tupitishe uamuzi kwamba wanaojitahidi kupindisha uhalali wa mtu kwa kutaka walipwe madeni ya nyumba humu JF, sasa wajiondoe kwa muda. Au wabadili hizo pseudonym maana wengine tutahitaji muda mrefu kuamini yoote watakayotoa mbele yetu baada ya hapa. Ni sifa mbaya kwa JF.

Kwa ujumla Ugomvi wa Dr Masau wengi mumeingizwa mjini bila kufahamu ulikoanzia. Tatizo ni la miaka mingi. Tangu Kontena la kwanza la vifaa vyake lilipoingia pale bandarini. Ilibidi hadithi ifike ikulu. Kibaya zaidi Wizara haina popote ilipowahi kutoa msaada.

Naona wekeni nguvu kwenye NSSF.
Ina maana hata kontena alitaka asilipe Ushuru na kwenda kwa rais? basi yeye ni mtu wa vya bure, tumlipie na pango lake.
 
Naona wawakilishi wa Dk. Masau wanajibu mashambulizi na kuleta data zao. Ni vizuri, kwani ukipata upande mmoja tu unakuwa huelewi.

Where Kuhani @?

Mimi nilishatoka kwenye the nitty gritties nikauliza kuhusu madai ya utapeli ya Dk. Masau, kuwa ana tabia ya kutolipa kodi ya pango, mnaweza kuelezea hii wawakilishi wake?

Kwamba hapa NSSF siyo mwanzo, kuna pattern kutoka Mikocheni alimzima Muarabu, kuna ukweli hapo?
 
Back
Top Bottom