Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #41
duh.. Dr. Khamisi umenifanya nishikwe na donge la uchungu!
zile links hazijajibu maswali ndio maana nikahitaji maelezo zidi
Kwa kweli wewe unamjua hasa Dr Masau kwani yote unayoyasema ni ya kweli kuna wafanyakazi hata mshahara hawalipi.Kuna kipindi serikali ilimuidhinishia documents fulani ambazo taasisi moja ya nje ilitaka imsaidie Fedha Lakini ilibidi serikali kupitia wizara ya afya iidhinishe aliidhinishiwa na kama kumbukumbu zangu ni nzuri alipewa Dola 350,000 ili awasaidie watanzania kuwapatia matibabu hayo ya moyo,Je anaweza kuwaeleza Umma wa Watanzania alizitumiaje hizo fedha?Na kama kuna watanzania waliofaidika na hizo fedha ikiwemo kupatiwa matibabu bure kwenye hiyo taasisi ni wangapi na awainishe hadharani?Kuna matembezi ya mshikamano yaliyofanywa na taasisi yake na kupatikana kiasi cha fedha za kitanzania milioni 169 je hizi nazo alizitumiaje au watanzania ambao ni wagonjwa walifaidika vipi na fedha hiyo?Hivi kama ameshindwa kutoa mchanganyuo wa fedha ya kwanza ambayo wizara ilimsainia ili taasisi fulani ulaya impe kwanini atake tena wizara ifanye kitu kile kile bila ya kutoa mchanganuo wa awali?Unajua unapoanzisha kitu kama hiki ni muhimu ukawa na watu "credible" kusaidia taasisi. Kwa mfano uliiona safu ya board of directors ya Haki Elimu? Did u see how they dealt with the goverment?
Sasa Bodi ya THI imefanya nini?Imesaidiaje katika hili. Zaidi sana tunachokiona ni Dr Masau analumbana na Wizara ya Afya kwa kutumia vyombo vya habari etc...lobbying skills zinahitajika hapa.....Sasa huyo dada anasaidiaje hapa...? Si ndio anayefanya admin ya THI....watu wanakopwa mishahara , ukabila , upendeleo etc.Nina contacts na watu kadhaa waliowahi kufanya kazi na taasisi hii wanasema it run like a "personal property"!Na wengi wameondoka
Unafikiri wanaompinga wanachukuliaje hili? Ukiamua kupambana usiachie loopholes kama hizi.Isitoshe kuna tetesi kuwa success rate ya operesheni zake ni ndogo(sina data!)
I am a big suppoter of Dr Masau lakini asafishe nyumba yake kwanza.Mimi nafikiri inawezekana kabisa watanzania kuchangia hili annually ....Hapo anapojaribu kupagusa pa eti badala ya India wagonjwa waje kwake.....ni pagumu....(Rupia zimeshatembea).
Atafute njia nyingine ya ku raise funds to prove skeptics his skeptics wrong .
Upande wa pili upi?sasa hizi hoja nzuri... nani anayeweza kunipa habari za upande wa pili wa suala hili? Natarajia kuzungumza na Dr. Masau Jumamosi.. na nitambana kwa haya maswali..
Kwa vile inaonekana kuna ugumu fulani wa kusoma kilichoandikwa (labda sababu ya wingi wa maandishi na kutokupangiliwa vizuri) nimerudi kwenye ukurasa wa kwanza na kuhighlite ni nini kinazungumziwa. Natumaini itawasaidia. Vinginevyo sina jinsi nyingine.
KNKCU, si hayo mnayomwaga hapa. Inabidi Moderator aongeze "alama ya kuuliza" kwenye heading ya hii post maana ilivyo sasa inaonekana kama kauli ya uhakika.
sasa hizi hoja nzuri... nani anayeweza kunipa habari za upande wa pili wa suala hili? Natarajia kuzungumza na Dr. Masau Jumamosi.. na nitambana kwa haya maswali..