Sakata la Dario: Mashabiki wa Singida Big Stars, tulieni..

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
889
1,928
Watu wa Soka,

Nina salamu maalum kwa mashabiki, wapenzi na wadau wa Singida Big Stars.

Naomba niwafahamishe tu kuwa taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu Winga wetu Dario Frederico sio za kweli. Dario ni mchezaji mwenye kandarasi ya miaka 3 na klabu ya Singida Big Stars.

Tunafahamu, uwezo na ubora ambao wachezaji wetu wameanza kuuonesha katika kipindi hiki cha pre-season kupitia mechi chache za kirafiki tulizocheza, vimewapa presha washindani wetu tunaoenda kukutana nao LIGI KUU hivyo zinapikwa propaganda za kuwavunja moyo mashabiki wetu na kuzua taharuki ili kuturudisha nyuma. Tayari wameshashindwa kabla

Msiwe na wasiwasi, hakuna mchezaji ambae tumemsajili na yupo kwenye mipango yetu ya msimu ujao ataondoka. Dario ni mmoja wa wachezaji ambao uongozi unaamini amekuja kwa sababu ya Target yetu ya msimu ujao. Hivyo hauzwi na hana bei.

Vilevile tunapenda kuwakumbusha kuwa taarifa zozote kuhusu klabu zitatolewa kupitia kurasa zetu rasmi na si vinginevyo.TUKUTANE LIGI KUU!
 

Attachments

  • Dariiiio.jpg
    Dariiiio.jpg
    41.2 KB · Views: 7

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
12,296
46,864
Huyo mchezaji mlikuwa mnatoa ila mmeona aibu tu, nawashangaa sijui kwanini hamjiamini, kama mmeamua kuwa klabu ya kuinufaisha nyingine msiogope, fanyeni hivyo kwa kujiamini, sio mnapelekeshwa kama watoto wadogo.
 

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
944
1,369
Jemesari anasema manara kakataa asije yanga kwakuwa habar hii kaanza kuivukisha yeye na manara hata jemdari saidi apate credibility kitoka kwa fans.hivyo basi dario anabaki kwa walima alizeti coz manara kagoma.
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
16,931
14,903
... hakuna mchezaji ambae tumemsajili na yupo kwenye mipango yetu ya msimu ujao ataondoka. Dario ni mmoja wa wachezaji ambao uongozi unaamini amekuja kwa sababu ya Target yetu ya msimu ujao. Hivyo hauzwi na hana bei.
Utapoteza kibarua chako ukikinzana na wakubwa wako. Bora ungepiga kimya tu
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
17,325
30,405
Huyo mchezaji mlikuwa mnatoa ila mmeona aibu tu, nawashangaa sijui kwanini hamjiamini, kama mmeamua kuwa klabu ya kuinufaisha nyingine msiogope, fanyeni hivyo kwa kujiamini, sio mnapelekeshwa kama watoto wadogo.
Hivi mbona watanzania mna wivu wa kitoto? Haya maneno mbona sikukusikia ukiyaongea kwa tukio la Habib Kiyombo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Top Bottom