Sakata la Dangote: Kama ni kuondoka na aondoke tuu

The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
9,303
20,319
Hii ni too much, kwa madai ya serikali hatuwezi ku deal na mfanyabiashara huyu

Nitashangaa sana kama serikali itakubaliana na matakwa ya dangote cement, itakuwa ni kuua moja kwa moja viwanda vingine vya cement hapa nchini vilivyofanya uwekezaji wa kutisha na ku struggle kwa miaka mingi mpaka kukua.

Hii iwe fair game, fair competition siyo kuwafunga wengine kwa ma kodi na yozo za kutosha kidha kumpendelea mwekezaji mmoja, yani tuue viwanda vitano kwa ajili ya kumtajirisha dangote...hii haiwezekani

Mazingira, kodi na incentives zote ziwe fair kwa wazalishaji wote wa cement la sivyo tutaua viwanda vyetu vya wazawa na kukuza cha mgeni ambaye halipi kodi na kila kitu anataka kiwe bure
 
Serikali ilikubalije kumpa Dangote vibali vyote vya kujenga hicho kiwanda kabla ya kumwekea masharti kwamba lazima atumie mkaa wa mawe wa hapa Tanzania badala ya kuagiza? Na mbona waziri alishasema Dangote wamefunga kwa sababu ya ukarabati tu lakini sasa maelezo yamekuwa mengine? Je, Dangote akiagiza makaa ya mawe nje ya nchi lakini pia akiuza sementi yake nje ya nchi kuna shida gani? Hivi kweli kama tunataka nchi ya viwanda tukimfanyia mizengwe Dangote ambaye ni tajiri mkubwa Africa kuna wawekezaji wengine watakaopenda kuja?
 
Maslahi ya nchi kwanza hayo mazagazaga mengine baadae..kwani akiondoka cement itakua hamna?? Mbona watu wamejenga hata kabla ya Dangote?? Akwendree analeta un9ja hapa kujiona wao wako juu.
 
Serikali ilikubalije kumpa Dangote vibali vyote vya kujenga hicho kiwanda kabla ya kumwekea masharti kwamba lazima atumie mkaa wa mawe wa hapa Tanzania badala ya kuagiza? Na mbona waziri alishasema Dangote wamefunga kwa sababu ya ukarabati tu lakini sasa maelezo yamekuwa mengine? Je, Dangote akiagiza makaa ya mawe nje ya nchi lakini pia akiuza sementi yake nje ya nchi kuna shida gani? Hivi kweli kama tunataka nchi ya viwanda tukimfanyia mizengwe Dangote ambaye ni tajiri mkubwa Africa kuna wawekezaji wengine watakaopenda kuja?
Wasije kabisa!!! Nchi yetu ni tajiri kuliko Dangote! Tena mwambieni huyo dangote wenu hatumtaki na awaambie na wawekezaji wengine wote kuwa hatuwataki!! Tumeshaagiza nchi hii iwe ya viwanda na tutavijenga wenyewe! Ala!! [HASHTAG]#teamkunimbichi[/HASHTAG]
 
kusema mengi bila ya kujua mkataba na makubiliano ya kuja Tanzania yalikuwaje ni kupoteza muda, tuwe wakweli kwa kusikiliza pande zote mbili, sasa unasema aondoke tu, kwa kuwa wewe haikuathari moja kwa moja, tuwe na uwezo wa kufikiri kabla ya kuandika.
 
JK amemuingiza Dangote kwenye hasara kwa ahadi zisizotekelezeka walizompa kumvutia kuwekeza Tanzania.

Hii ndiyo Tanzania ya viwanda janja-janja.
 
mh!hapa hujaekeweka!kwani jamaa anataka gesi ya bure?au iwe bei rahisi kuliko viwanda vingne?cha msingi tuzingatie makubaliano yetu na huyu mwekezaji,tusije tukawa tunajikaanga wenyewe kwa kufukuz wawekezaji!

Tukimfukuza DANGOTE tajiri wa AFRICA ni sawasawa na kuwafukuza wawekezaji wa kiafrika wote wengine.
 
Yani kweli nimeamini mwenye shibe hamjui mwenye njaa .kabla ya Dangote cement ilikua bei juu baada ya dangote ukaonekana ushindani wa kibiashara cement ikashuka bei hata nyumba bora zikaongezeka kwa maskini. sasa imewauma kununua cement kwa bei poa yani uhalisia wa kumsaidia mtanzania katika maisha bora hayapo ni unafiki tu.
 
Aliyeenda kumkokota huko na ahadi ya special treatment ndiye kamtia hasara.

Yawezekana hata aliahidiwa kujengewa reli ya SG na serikali from Mtwara to DSM maanake tayari kaanza kulalamika soko kubwa la saruji liko mbali tofauti na alivyoelezwa.

BTW:Aliahidiwa tu au waliingia mkataba na serikali wenye hizo terms?

Kama ni mkataba si aende mahakamani!
 
mh!hapa hujaekeweka!kwani jamaa anataka gesi ya bure?au iwe bei rahisi kuliko viwanda vingne?cha msingi tuzingatie makubaliano yetu na huyu mwekezaji,tusije tukawa tunajikaanga wenyewe kwa kufukuz wawekezaji!

Tukimfukuza DANGOTE tajiri wa AFRICA ni sawasawa na kuwafukuza wawekezaji wa kiafrika wote wengine.
Hatuwezi kukumbatia wanyonyaji
 
Back
Top Bottom