Sakata la Catalan: Wazungu ni wanafiki sana, wanatulazimisha kufanya vitu ambavyo wao vinawashinda

dedon

JF-Expert Member
Jul 6, 2015
1,507
2,054
Kweli wazungu ni watu wanafki sana wanajarbu kututawala waafrika kwa kutulazimisha tufanye vitu ambavyo hata wao hawafanyi.

Katka swala la Catalan kujitoa Hispania kuna vitu vingi nimejifunza.

Kwanza democracy ni theoretical sio practical kwao bali wanaijaribu kwetu kama itafanya kazi ama lah.

Wakat sudan inataka kujigawa wao ndo walikua mstari wa mbele kulazimisha kura za maoni kwa kisingizio cha democracy na ilivyofanikiwa kujigawa Sudan Kusini na Kaskazini waliwapongeza viongoz kwa kufanya kile wananchi walikua wanahitaji.

Leo wananchi wa Catalan baada ya kupiga kura za kujitoa Spain wamepitisha sheria za direct rule kwa jimbo la Catalan kwamba litaendelea kubaki kama koloni la Hispania kitu ambacho wakifanya mataifa ya Afrika matamko yatakuwa mengi. Mfano Morroco anachokifanya kwa Western Sahara sidhani kama kina tofauti na hiki lakini angalia Morroco anavyosumbuliwa

Kila mtu anaona jinsi Catalan walivyo hawataki kubaki Spain lakin EU wametoa tamko hawatokubali kuona Catalan wakijitenga na sio EU tu bali mataifa kibao viongozi wao wametoa matamko kuwasupport Spain.

Waziri mkuu Spain kavunja serikali yote ya Catalan ikiwemo Mkuu wa polisi na wengineo kisa walikuwa wanasupport muungano but hakuna anayekemea

Ingawaje kuna kura zilipigwa illegal mara ya kwanza na legal kwa mara ya pili zote watu wamepinga muungano kwa asilimia kubwa lakini viongoz wa Ulaya hawaulizii democracy tena

Najarbu kuwaza tu haya matukio yangetokea kwa taifa la kiafrika au uarabuni tungeshuhudia vitisho ambavyo vingeambatana na kupinga.

Tunajifunza nini sisi Watanzania katika hili? Tuna muungano na Zanzibar tuwe makini sana na hawa wazungu watakapojarbu kututenganisha nao.
 
Mkuu figisu ziko dunia nzima sio africa tu tafauti kati yao na sisi ni methodology tu.pia rekekebisha hapo juu moroco wanaikalia kimabavu Jamhuri ya sahrawi na sio Saudi arabia.
 
Mkuu figisu ziko dunia nzima sio africa tu tafauti kati yao na sisi ni methodology tu.pia rekekebisha hapo juu moroco wanaikalia kimabavu Jamhuri ya sahrawi na sio Saudi arabia.
Na ili kuwasopoti tulipewa nini na mfalme wa Morocco?
Nimeikumbuka hii
 
Article 155 inatumika hapo yaani kuitumia hiyo wameifananisha na nuke bomb.
It means ni last option kabisa.
Ilitungwa mwaka 1978 na Ina maneno 84 tu lakini umebeba maneno mazito sana.
4a7d580197e98d4ed90ae6aad140d4bf.jpg
 
Wanatufanya mazwazwa hawa washenzi wa pua ndefu.
Kuanzia Britain,Spain,ulaya yote mpaka USA wote sura mbili ila sisi tunavyoitikia hicho kibwagizo cha democracy mpaka twauana.
 
Wanatufanya mazwazwa hawa washenzi wa pua ndefu.
Kuanzia Britain,Spain,ulaya yote mpaka USA wote sura mbili ila sisi tunavyoitikia hicho kibwagizo cha democracy mpaka twauana.

Ni mazwazwa kweli why watuendeshe na mambo yetu kama tuko strong. Hiyo AU wenyewe haina nguvu yoyote hata taifa LA Africa likiingiliwa wata mute tu.
 
Ni mazwazwa kweli why watuendeshe na mambo yetu kama tuko strong. Hiyo AU wenyewe haina nguvu yoyote hata taifa LA Africa likiingiliwa wata mute tu.
Liingiliwe mara ngapi mkuu wangu ,au umesahau ya Libya..!??
 
Democracy is not real!
*****!
To be precise it's not real if you oppose oppression and exploitation from european country or USA.
 
Liingiliwe mara ngapi mkuu wangu ,au umesahau ya Libya..!??

Ni kweli usinikumbushe machungu ya Libya yaani Africa wote tulinywea hakuna hata MTU aliyesimama kumtetea ghadafi. Lakini hao wazungu gusa hata mbwa wao utaona wote wanaungana na kuku attack.
 
Mkuu figisu ziko dunia nzima sio africa tu tafauti kati yao na sisi ni methodology tu.pia rekekebisha hapo juu moroco wanaikalia kimabavu Jamhuri ya sahrawi na sio Saudi arabia.
nilijichanganya shukran mkuu
 
Wanatufanya mazwazwa hawa washenzi wa pua ndefu.
Kuanzia Britain,Spain,ulaya yote mpaka USA wote sura mbili ila sisi tunavyoitikia hicho kibwagizo cha democracy mpaka twauana.
na hiko ndo kinachokera wako busy kuhubiri democracy kenya hadi watu wanauana wao wenyewe hata hawajishugulishi
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom