Sakata la Buzwagi hatuwezi kulisahau

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Posted Date::9/29/2007
Sakata la Buzwagi hatuwezi kulisahau

Na Julius Samwel Magodi
Mwananchi

ZAMANI binadamu tulikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukumbuka mambo. Kuweka mambo kichwani ilikuwa ndio njia mama ya kutunza kumbukumbu.

Kukuliwa na washairi mahiri waliokuwa wakikariri maelfu ya mistari bila ya kusahau. Misahafu ya vitabu vya dini pamoja na ukubwa wake wote vilikaririwa na wafuasi wa dini husika bila matatizo.

Baada ya ugunduzi wa maandishi, uwezo wa binadamu kukumbuka mambo umepungua sana. Ubongo haupewi mazoezi au changamoto ya kukumbuka maana unaweza kuandika mahali unachotaka kukumbuka.

Ni kutokana na teknolojia hii ndiyo hivi sasa kuna vitu vingi mno vya kutukumbusha kitu ambacho tunataka kuvikifanya si ajabu kabisa hivi sasa unaweza kutumia mlio wa saa au simu kutukumbusha kitu unachotakiwa kukifanya.

Hata hivyo, pamoja na kupanuka kwa teknolojia hiyo Watanzania tunaonekana bado uwezo wetu wa kukumbuka unazidi kupungua mno.

Nalazimika kutoa mfano huu kuwa Watanzania hawawezi kumbukumbuka mambo yaliyopita, kama vile mjadala mkali unaoendelea hivi sasa wa mkataba wa kuchimba madini ya dhahabu katika mgodi wa Buzwagi mkoani Shinyanga.

Mkataba huu uliingiwa na serikali Februari mwaka huu jijini London na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na kampuni ya Barrick iliyokuwa ikiwakilisha kampuni yake tanzu ya Pangea Minerals.

Nakumbuka ni mwaka jana tu Rais Jakaya Kikwete aliamua kuwa mikataba yote ya madini ipitiwe upya ili iweze kuwafanya wawekezaji na Watanzania nao kuweza kufaidika.

Alisema serikali haitaingia tena mikataba mipya mpaka hapo iliyopo imepitiwa, lakini baada ya muda mfupi tunashudia serikali inaingia katika mkataba mwingine ambao hauana manufaa hata kidogo kwa nchi. Je hii kukosa kumbukumbu kuwa rais alishazuia au ni kitu gani? Nashindwa kuelewa kabisa.

Awali baada ya kubainika habari kwamba kuna mkataba mpya ambao serikali imeingia na kampuni ya Barrick kuhusu mgodi wa Buzwagi nilidhani kwamba kasoro zilizokuwa zikielezwa zilikuwa ni ndogo tu.

Lakini baada ya kuona nakala mojawapo ambayo zimemwagwa kama njugu na kambi ya upinzani kwa hakika unasikitisha.

Moja ya upungufu uliopo katika mkataba huo ni kwamba, wawekezaji hao watafanya shughuli zao kwa muda wa miaka 25 na wakimaliza wanaweza kuongezewa tena kipindi kingine kama hicho na masharti yakiwa yale yale na wanaweza tena kuongezewa kipindi kingine ambacho waziri wa madini ataona kinafaa.

Kwa hakika huu sasa sijui niute uhuni au ni kuhujumu nchini, kwa sababu haiwezekani mwekezaji apewe kipindi kirefu kama hicho kuwekeza katika mgodi huo unaolezwa ni wa muda mfupi halafu masharti yasibadilishwe.

Kwa maana nyingne ni kwamba kipengele katika mkataba huo kinachoeleza kwamba kodi zitakazolipwa na Pangea Minerals, ni pamoja na asilimia tatu ya thamani ya madini baada ya kuondoa gharama za uzalishaji kama mrahaba kwa madini yote yatakayochimbwa eneo la Buzwagi isipokuwa almasi, ambayo mrahaba wake utakuwa asilimia tano, zibaki hivyo hivyo hata kama kampuni hiyo itakaa hapo kwa miaka 100.

Hii haingii akilini hata kidogo. Pia kipengele hicho kinaonyesha kuwa mkataba wa kampuni hii na serikali sio wa kuchimba dhahabu peke bali ni wa madini yote, ndiyo maana unaonyesha kuwa kuna almasi ambayo italipiwa mrabaha wa asilimia tano.

Sasa ninajiuliza almasi hiyo wataichimbia wapi ina maana watapewa eneo lingine kuchimba madini hayo baada ya kumaliza madini ya dhahabu ambayo wanasema yapo kidogo katika eneo hilo.

Upungufu mwingine katika mkataba huo, unaeleza kwamba kampuni italipa ushuru wa stempu kama ulivyoainishwa na Sheria ya Ushuru wa Stempu Na. 20 ya Mwaka 1972 kuanzia tarehe ya kuanza kwa mkataba wa Buzwagi.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa Pangea Minerals kutolipa hata senti moja kama ushuru wa stempu, kwani kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Ushuru wa Stempu kimetoa angalizo kwamba �hakuna ushuru wowote utakaolipwa kutokana na waraka wowote uliosainiwa na, au kwa niaba au kwa taarifa ya Serikali.� Ambapo kama kifungu hiki kisingekuwapo, basi Serikali ingekuwa na wajibu wa kulipa ushuru huo kuhusiana na waraka huo.

Kwa hakika kama nilivyosema hapo awali ni kwamba kuingia mkataba kama huu kwa wakati huu ambapo tayari Rais ameshasema kuwa mikataba yote ya madini ipitiwe upya ni kumdharau na kuwatukana Watanzania.

Kwa nini tuendelee kuingia mikataba isiyokuwa na maslahi? hii inatuonyesha kwamba kuna wenzetu wachache wanafaidika na mikataba hii mibovu.

Kuna wakati Rais Kikwete alipokuwa ziarani katika nchi za Scandinavia aliwahi kulalamika kwamba tatizo la Tanzania kuingia mikataba mibovu ni kutokana na kutokuwa na watalaam ambao wanaweza kutetea maslahi ya taifa wakati wa kuingia mikataba hiyo.

Hivi ni kweli kwamba hata suala la kumpa mwekezaji wa Buzwagi muda wa miaka 50 kuwekeza kwa kufuata masharti yale yale, kunahitaji mtu uwe mtalaam kujua? Au mtu kujua kwamba huyu mwekezaji kwa kulipa mrabaha wa asilimia tatu tena baada ya kupata faida kuwa hauna maslahi ya nchi nalo linahitaji mpaka mtu uwe mtalaam wa mikataba?

Nadhani hili limefanyika kwa makusudi kwa nia ambayo wenzetu wanaijua.

Pia kasoro kubwa ambayo ipo katika mkataba huu ni kufutwa kwa mkono kipengele cha ushuru wa forodha wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Kwa nini ufutwe kwa mkono, ina maana kwamba Waziri Kamaragi alikwenda London Uingereza kuusaini mkataba huu kabla ya kuusoma, kama alikuwa ameusoma awali kwa nini asingeshauri uchapishwe upya ili kuondoa makosa kama hayo?

Kuna maswali mengi mno yaliyopo katika mkataba huo ambayo yanahitajika kujibiwa ili Watanzania wafahamu ukweli wa mambo kuhusu suala hili. Tunasubiri kuona Rais Kikwete anawawajibisha wote waliohusika katika kuingia mkataba huu ili wananchi warejeshe imani yao kwa serikali.

Kama nilivyosema awali tatizo la Watanzania tulilonalo ni kusahau mapema, tabia hii ndiyo imekuwa ikitumiwa na baadhi ya viongozi wetu kutungiza katika matatizo wakidhani kuwa Watanzania huwa hawachelewi kusahau.

Wanajua kabisa kwamba pamoja na rais kutoa tamko mwaka jana tu la kupitia mikataba upya ya madini lakini wanajua kwamba baada ya mwezi Watanzania kama kawaida yao watakuwa wamesahau na wao kuendelea kuingia mikataba mibovu.

Mwandishi wa safu hii ni mhariri wa habari maalum. Anapatikana kupitia baruapepe; juliusmagodi@yahoo.com. Simu ; 0754 304336
 
ahsante Mwananchi kwa kuendelea kutukumbusha wananchi, keep it up kwa kuongea ukweli, inawezekana pia hata hawa viongozi (including wabunge) wetu wanao huougonjwa 'wa kusahau', nahisi nalo hili ni tatizo kubwa.

Sijui huu ugonjwa umetokana na nini?
Sijui ni moshi wa mbio za mwenge au ni ule uji wa burga kwa previous generations?

Kama tumeshajua haka ka ugonjwa, na angalau dawa yake ya kupunguza makali ni kuweka alarm ili zitusaidie, basi tuzitumie hizi alarm (vyombo vya habari) ipasavyo,

lakini nahisi hata hizi alarm sometimes huwa zinaishiwa betri (ukata) na kusababisha (kutoa mlio ambao si wenyewe au kutoa taarifa muda ukishapita (distoration ya taarifa)

Na pia hao wanaozifeed hizo alarm wamesalimika na haka ka ugonjwa ka kusahau, otherwise kama na wao wanahuu ugonjwa then kumbukumbu ya wananchi ipo mashakani zaidi.
 
Dr Kikwete aliyaona hayo siku nyingi tu lakini hakuna aliyekuwa serious
 
Karamag rol modal wa lowasa yaan wezi ndo lowsa huwa anawapigia mfano wa kuigwa
 
Back
Top Bottom