Sakata la boss wa TIC: Hivi Kibonde yuko sahihi kuwaita watanzania wehu?

vantz

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
1,107
570
Nikiwa narudi kazini leo mida ya saa 11:26 hivi nikiwa nimefungulia Radio Clouds zaidi ya mara mbili nimemsikia mtangazaji huyo akisema watanzania ni WEHU.

Wakati huo alikuwa anazungumzia ishu ya kusimamishwa kwa Kairuki ameshindwa kuzuia hisia zake na kuzungumza maneno ya kipashukuna sana kiasi cha kusema Rais anasema anaowatumbua ni wezi wakati hana ushahidi watanzania walivyo wehu wanashangilia tu!

Mwenzie Gadner nae anasema watu wanameza kete za dawa za kulevya halafu wanaenda kunya zinatoka hewani?

Sio bure hawa watu wana matatizo..
 
Kwani ni uongo?? Na neno gani la kipashkuna ambalo we huwezi andika hapo??
 
Kibonde ni ProJK na anasahau kwamba ENZI zimeshapita. Itam cost
 
Mmh..
ngojea tuone" kinyantindinya" , na' " yule " akimwachia basi kibonde kwao'" kilingeni "
 
Nilisikia huyu kibonde alikua msomaji wa magazeti ikulu kipindi cha jk ila kwa kipindi hiki magu kamwambia nyang'au wee kaaa mbali hakuna hela za mchezo kula urefu wa kama tena kusoma magazeti sii kazi hata mtoto wangu anaweza kusoma
 
Kibonde ana njaa kuliko Ruge, halafu hajui kujenga hoja,anajipendekeza mpaka basi..
 
kibonde amesoma chuo gani cha uandishi wa habari? ana elimu gani? Nadhani imefika wakati wizara ya habari kufanya uhakiki wa waandishi na watangazaji kama wana sifa ya kazi hizo
 
Sasa unashangaa nini? Hawa ni watangazaji wa Clouds Radio na kila mtanzania anajuwa kuwa watangazaji wa Clouds hawana weledi. Clouds kuna mtangazaji mzuri pale? Si unaona matangazo yao ni ya kitoto.
Mnakosea. Hawa si ndiyo walipongezwa na rais au nimesahau?
 
Back
Top Bottom