SAKATA LA ARVs FAKE NANI AFUNGWE KENGERE SHINGONI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SAKATA LA ARVs FAKE NANI AFUNGWE KENGERE SHINGONI?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miwatamu, Oct 12, 2012.

 1. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133


  Kwa muda wa majuma kadhaa hapa kwetu tumejikuta tukisahau kila kitu na kurukia mjadala ambao uko hot kwa sasa wa sakata la dawa fake za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi. Katika sakata hili ambalo limehusisha kiwanda cha TPI, MSD,TFDA,TBS na kwa upande mwingine SIASA, mbali ya kuwa mjadala lakini pia sakata hilo limeleta hofu kubwa katika jamii na haswa wale wanaotumia dawa hizo.

  Sasa sakata hili linakuja kuwa kubwa baada ya ufafanuzi uliotolewa na mama Madabida ambaye ni mmoja wa wamiliki wa kiwanda hiki wakati akihojiwa katika kipindi cha kupaka rangi cha Magic FM. Mama huyu amelaumiwa na watu wengi nikiwemo mimi kwa kuamini kuwa huu ni ule mkakati wa watu wa CCM kuzoe kupata hela haramu ikibidi hata kwa kutoa roho ya mtu. Tofauti na fikla hizo, sasa imegundulika kuwa dawa hizo hazijatoka TPI na wala wao hawajasambaza dawa hizo kwa kipindi cha miezi 16 iliyopita! Swali la kujiuliza, Je, zimetoka wapi? Na kwa lengo gani?

  Ikumbukwe kuwa MSD ni idara ambayo imekuwa ikilalamikiwa kila kukicha kwa kuingiza nchini dawa zilizoisha muda wake au ambazo hazihusiani na magonjwa sugu yanayotukabili hapa kwetu. Ilifikia hatua ya wabunge wetu kuongea hadi kutoa udenda juu ya utendaji mbovu wa idara hii, hata hivyo hakuna hatua za dhati ambazo ziliwahi kuchukuliwa na wenye nchi pamoja na wadau wengi kulalama sana lakini selikari iliweka pamba masikioni.

  Je, sasa linapojitokeza sakata hili tutegemee nini kutoka kwa selikari kama kiwanda ambacho kilikuwa kikilalamikiwa kimekanusha kweupe kuwa hakihusiki na huku Mkurugenzi wa MSD kuonekana kama anayebebwa kila kukicha?
  Tulijadili wana jamvi.
   
Loading...