Sakata la Airtel na TTCL: TTCL wasema wana ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa kampuni ya Airtel ni mali yao 100%

MJUE MSANII WAKO

Kwanza niwape pole na mjukumu ya kilasiku, na bila kupoteza muda nianze na kusema hamjambo???

leo nataka nikukaribishe umjue msanii wetu!!! Msanii matata, msanii wa kuigwa, msanii pendwa na mwenye nyimbo nzuri za kupendeza!!!

Katika harakati zake za kuitengene ulbum yake ya WANYONGE msanii wetu alianza na single kali, single ya kutisha iliyo tengenezwa studio maarufu nchini tozamalia, Na single ikiitwa "VIWANDA". Single ilisumbua sana na ikashika chati mbali mbali ikitarajiwa kutoa ajira kwa wacheza shoo, kila presenter wa redio allipiga single hii,

Single ika hit ikaaminika itatupelekeka kimataifa, mara ghafla ikaonekana single ni feki, single imekopiwa mahala, ghafla ikapotea, na hata tuzo haikupata matokeo yake wacheza shoo wakalalamika sana wakidai single ilikosa midundo mizuri ivyo msanii wetu akashtuka akaja na single ingine;

Single ya vyeti vya ukweli; single hii ilikuja na moto wake. Msanii wetu akadai produza alie tengeneza mdundo wa single ya VIWANDA alikua na vyeti si vya kweli, ndio maana single ile haikupata tuzo.

Basi msanii akaipromoti single yake hii mpya, kwenye media zote watu wakaisikiliza jamaa akimponda produza wake wa zamani kuwa alikua navyeti tata toka call me J, kwakua single ya viwanda ilibuma, watu wakapenda maneno lakini wakagundua kuwa single haikua na style ya kuchezwa vizuri, wakaisahau nayo ikabuma msanii akabaha akaaamua kuja na single ingine;


Simgle akaiintroduce kwa jina la "wafanyakazi pumzi"; hii single bwana ilikua ina wahusu wacheza shoo wa msanii, Kwamba walikua hawana pumzi , hawajui kubuni stail za kucheza kwenye midundo yake, akawaimba kua amewafukuza wote na aakandaa tamasha kuonesha kua amekuja na kundi jipya la wacheza shoo ili kuibeba single yake ipae lakini akaonabora atoe na ya pili papo hapo,

Ghafla msanii wetu akatoa single ingine inaitwa "MAKINI MKIA WA NGOMBE" ikafanyiwa promotion vituo vya redio zote, single ng'ombe. Single ikabamba, nchi ikasimama kila mtu makini mkia wa ng'ombe, ikasemekana single itauza bilioni 700 watu wakatarajia msanii atawajengea familia yake mjengo wa maana na kupata noha moja moja mwisho wasiku naskia wanunuzi wa single ya makini mkia wakaingia mitini single ikafa ikafifia, jamaa ikabidi arudi studio;


Akatafakari sana akaona kama single zote zinahiti muda mfupi afu zinapotea; ndipo msanii akarudi studio na kuja na single ingine inaitwa "OKOTA MALI" ndani ya single hii msanii akaonyesha jinsi alivyo okota vichwa vya basii kule gambia na magari meeeengi akiwa visiwa vya komoro, single iliwashangaza wengi lakini ilibidi waipokee, tatizo koras yake ikawa haina melody nzuri msanii akaona akaribishe wasanii wenzake ili watoe single moja kali itakayo mpeleka sasa kimataifa!!


Ndipo msanii akaja na single inaitwa "HAMAHAMA" umondani akawashilikisha wasanii mbali mbali, inasemekana wengine aliwalipa ili watie mistari yao kuifanya single ifike kimataifa, bahati mbaya mixing ya sauti kule studio kutokana na kuwashirikisha wasanii wengi ikawahaina quality, single ikapigwa sanaaaaaaaana but nayo ika chuja, maana wasanii alio washirikisha wengi washa zoeleka!!

Sasa msanii kaja na single mpya inaitwa "WHERE IS MY PHONE"kaitambulisha juzi wakati anatangaza kuamia nyumba mpya Stay tune tujue ita leta mafanikio??


Kama single hii nayo itabuma basi ulbum ya wanyonge itakosa market na faida ila kwa kuwa wacheza shoo wao nikucheza tuuuuuu kama wasipo inunua wataicheza tuu!!!


Alamsiki!!!
 
TIMIZA wananidai nisubiri haya mambo yakae sawa nije kumlipa mmiliki mpya!!
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkurugenzi mkuu wa Tanzania telecommunication limited (TTCL) alidai kuwa kampuni hiyo ina nyaraka zote zinazoonyesha kuwa Airtel ni mali ya TTCL.

Licha ya hivyo mkurugenzi huyoamekiri kuwa mchakato wakuichukua aitel ni vita kubwa kutokana na mchakato wa kuihamisha kampuni hiyo ulivyokwenda.

Akihojiwa na waandishi wa habari aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa airtel bw. Joseph Warioba kuhusu swala hili alisema yeye hawezi kuzungumzia swala hili kwani wahusika wakuu ni serikali na ndio wenye mikataba ya kampuni hii.

Pia bodi ya sasa ya airtel inadai kwamba alifuata taratibu zote za kisheria kabla ya kupewa leseni na serikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkurugenzi mkuu wa Tanzania telecommunication limited (TTCL) alidai kuwa kampuni hiyo ina nyaraka zote zinazoonyesha kuwa Airtel ni mali ya TTCL.

Licha ya hivyo mkurugenzi huyoamekiri kuwa mchakato wakuichukua aitel ni vita kubwa kutokana na mchakato wa kuihamisha kampuni hiyo ulivyokwenda.

Akihojiwa na waandishi wa habari aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa airtel bw. Joseph Warioba kuhusu swala hili alisema yeye hawezi kuzungumzia swala hili kwani wahusika wakuu ni serikali na ndio wenye mikataba ya kampuni hii.

Pia bodi ya sasa ya airtel inadai kwamba alifuata taratibu zote za kisheria kabla ya kupewa leseni na serikali.

Chanzo: Mwananchi
Yani mimi nashindwa kuelewa hawa viongozi wetu uwa wanafanya nini wakiwa kwenye nafasi zao za kazi.

Hivi inakuaje miaka yote hiyo zaidi ta 15 leo hii amekuja Rais mwingine ndyo wanajua kuwa Airtel/Zain ni mali ya serikali? Ina maana muda wote huo mkurugenzi mtendaji wa TTCL alikua hajui nini kinaendelea ndani ya shirika analoliongoza?anaamka asbh anafika ofisini hasomi documents za shirika?

Kweli we have a long way to go. Badala ya kwenda mbele tunazidi kurudi nyuma. Kabla hili halijaisha, linaibuka jingine. Albert Einstein
 
Jaman mnauliza ccm ilikua wap,namm niwaulize mnataka punda au mnataka mlio?ccm nilisanam la jina ss tunataka mtu anaethubutu namtu huyo ni magufuliiiiiiiiii,mbona wakat nyerere anafanya mlisema anafanya mwalim?hamkusema ccm?ninyi kizaz chanyoka mnaotafuta ishara sinawauliza?sininyinyi mlimkataa yesu ninyi?mkasema huyu mwana wa seremala,,,,,!!!
 
Nimesoma makala hii nimegundua kuwa wasiojulikana wanamiliki kampuni kubwa nawana pesa ile mbaya,kumbe walianza nzamani

IKIWA imepita siku moja tangu Rais John Magufuli amwagize Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kuchunguza undani wa suala la umiliki wa kampuni ya simu ya Airtel, siri zaidi kuhusiana na kile kilichofanyika katika ‘dili’ za mauziano zimeanza kuanikwa.

Akizungumza mjini Dodoma juzi, Rais Magufuli alimtaka Dk. Mpango kuchunguza undani wa kampuni ya Airtel baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kampuni hiyo inapaswa kuwa chini ya umiliki wa Kampuni ya Simu (TTCL), ambayo ni ya serikali. Pia Rais Magufuli alieleza wazi kuwa kuna ‘mchezo mchafu’ uliofanywa na baadhi ya watu katika suala hilo.

Kutokana na agizo hilo la Rais Magufuli, jana, TTCL, kupitia kwa mwenyekiti wake wa sasa wa bodi ya wakurugenzi, Omar Nundu, na Ofisa Mtendaji Mkuu, Waziri Kindamba, iliibuka na kuanika undani wa mambo kadhaa kuhusiana na kampuni hiyo, mojawapo ikiwa namna vigogo watano walivyoketi kwa siku moja na kufanya uamuzi unaoibua maswali mengi kwa sasa kuhusiana na umiliki wa kampuni ya Airtel. Kimahesabu, siku moja ina saa 24.

Alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo linaloambatana na madai kwamba TTCL ndiyo inayoimiliki Airtel Tanzania, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackoson Mbando, alisema jambo hilo hawawezi kulizungumzia kama watendaji bali wamiliki wa hisa walio nje ya nchi ndio wenye wajibu huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema chanzo cha yote kilianzia Agosti 5, 2005, wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi za TTCL na Celtel wakati huo na wajumbe watano ambao majina yao hakuwa tayari kuyataja, walipokutana siku hiyo moja na kubariki uamuzi mzito uliofikisha jambo hilo lilipo sasa.

Nundu alisema bodi hiyo ilikuwa na watu tisa, lakini siku hiyo moja waliketi watano kati yao na kufanya uamuzi huo mazito huku wakiongozwa na mwenyekiti ambaye wakati huo alikuwa amekabidhiwa asilimia moja ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na ‘mtu asiyejulikana’.

Nundu alisema Celnet ilianzishwa na TTCL Mei 7, 2001 kwa mtaji wa Sh. bilioni moja na thamani ya hisa ikiwa Sh. milioni moja.

Alibainisha kuwa TTCL ilikuwa ikimiliki hisa moja huku thamani ya hisa ilikuwa Sh. 1,000 na mtu asiyejulikana alikuwa akimiliki hisa moja yenye thamani pia ya Sh. 1,000, kuanza baishara kwa jina la Celtel.

Hata hivyo, Nundu alisema hisa moja ya mtu asiyejulikana ikashikiliwa na raia wa kigeni na kwamba baadaye, TTCL ilitoa bilioni tano kwa ajili ya mtaji ili kampuni ianze kufanya kazi.

"Ilianzishwa kampuni inaitwa Celnet…imeanzishwa na TTCL,…ikapewa masafa megawati 900. Ilipofika wakati wa kufanya kazi, ikabadilishwa na kuwa Celtel, kampuni hii ilianzishwa na TTCL Mei 7, 2007 mtaji wake ukiwa Sh. bilioni moja, maana yake hisa milioni moja na kila hisa ina thamani Sh. 1,000,” alisema Nundu.

“Lakini wanahisa wakawa wawili, TTCL yenyewe ikachukua hisa moja, mtu asiyejulikana akachukua hisa moja, lakini akaishika raia wa kigeni. Kwa maana hiyo, kampuni ikaanzishwa kwa fedha Sh. 2,000," alisema Nundu.

Aidha, Nundu alisema TTCL ilitoa pia fedha zaidi ya Sh. bilioni 82 kwa ajili ya biashara huku cha kushangaza, mtu asiyejulikana akiwa hajatoa kitu chochote.

"Kama si TTCL kutoa Sh. bilioni tano, hakuna ambacho kingefanyika. Hakukuwa na uhitaji wa mwekezaji…. isitoshe TTCL iliweka Sh. bilioni 82 na ushee kuikopesha Celtel…sasa hapo unaona ni kampuni ya TTCL," alisema Nundu.

Alisema baadaye, raia wa kigeni aliyekuwa akishikilia hisa moja ya mtu asiyejulikana aliikabidhi kwa Mtanzania ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na pia Celtel.

“Siku ya kikao hicho, mwenyekiti wa bodi (ambaye ndiye aliyekabidhiwa hisa hiyo moja ya mtu asiyejulikana) na wajumbe wengine watano walifanya maamuzi (uamuzi) magumu (mgumu) ya kuirudisha hisa hiyo moja na kuikabidhi TTCL, hivyo TTCL ikawa inamiliki Celtel kwa hisa zote kwa asilimia 100,” alisema.

Akieleza zaidi kuhusiana na ‘mchezo’ uliofanyika, Nundu alisema thamani ya hisa asilimia 100 za TTCL ilikuwa Sh. bilioni moja, lakini wakakubaliana siku hiyo kuongeza thamani ya hisa hizo hadi kufikia Sh. bilioni 50 katika kampuni ya Celtel.

Alisema mpaka Mei 7, 2001, hisa 999,998 zisizo na mtu ilipewa TTCL kwa sababu ilishaweka Sh. bilioni tano, hivyo kuwa na jumla ya hisa 999,999 huku mtu asiyejulikana akiwa bado anamiliki hisa moja.

Nundu alisema ilipofika Novemba 27, 2001, raia wa kigeni aliyeshikilia hisa ya mtu asiyejulikana alimpa mtu mwingine ashikilie ambaye ni Mtanzania, na mtu huyo aliyepewa ashikilie ndiye aliyekuwa mwenyeki wa bodi ya TTCL na Celtel.

Nundu aliongeza kuwa baada ya hapo, zilichukuliwa Sh. bilioni 40 za TTCL na kuwekwa katika mfuko wa Celtel kama mtaji wake, hivyo kuifanya kumilikiwa kwa asilimia 100 kwa mtaji wa Sh. bilioni 41, huku Sh. bilioni tisa zikiwa hazina mmiliki.

“Siku hiyo hiyo moja, baada ya muda TTCL ikanyang’anywa hisa zake zote na hapo ndipo tunapojiuliza uhalali wa Celtel,” alisema Nundu.

Nundu alisema kama hiyo haitoshi, hisa hizo zilianza kugawanywa kwa watu ambao hawapo katika mlolongo wa Celtel kutokana na ukweli kuwa wakati huo, waliokuwa wakitambulika ni wawili tu, yaani TTCL na ‘mtu asiyejulikana’.

Aidha, alisema ilikubaliwa kuwa serikali ipewe asilimia 65 na ‘mtu asiyejulikana’ apewe asimilia 35.Alisema kwa hesabu za kawaida, haikupaswa watu wengine kugaiwa hisa kwa sababu hawakuwa na hisa tangu awali lakini wakapewa hisa zote.

Alisema kama haitoshi, siku hiyo hiyo ya kikao cha bodi yenye watu watano, serikali ikapewa hisa milioni 26.650, ikiwa ni uwiano wa asilimia 65 ya umiliki na mwingine (mtu asiyejulikana) alipewa hisa milioni 14.350, sawa na asilimia 35.

Baada ya hapo, alisema serikali ilichukua tena hisa milioni 10 zingine na kumpa mwekezaji, hivyo kumfanya afikishe milioni 24.350 na kuifanya serikali kubakiwa na hisa milioni 16.650.

Alisema uwiano huo ndio unaoendelea hadi leo na kwamba umiliki wa Celtel upo mikononi mwa Airtel ‘kimagumashi’ (kijanjaujanja).

Kadhalika, Nundu alisema jambo la kushangaza ni kwamba ilipofika Juni 23, mwaka jana, Airtel ilitangaza kujitoa kwenye umiliki wa TTCL ambao walikuwa wamiliki na wameshajitoa.

Nundu alisema baada ya kufanyika ‘mchezo’ huo, TTCL ilikopeshwa dola za Marekani milioni 28 na kuwekewa riba ya asilimia 18 na kusababisha deni kukua hadi kufikia Sh. bilioni 76.6.

“Mimi na wenzangu baada ya kuja TTCL, ndiyo tukaanza kuchimba chimba ili kujua mbivu na mbichi kwa sababu kuna mambo mazito zaidi,” alisema.

Bosi TTCL Ajilipua
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, alisema wanachotaka kutoka kwa Airtel ni kampuni yao.

Alisema wanaamini na kutarajia kuwa watarejeshewa kampuni yao bila kukwaruzana na wamikili wa kampuni ya Airtel na kwamba wamejipanga kwa ushahidi wa asilimia 100.

“Tumeamua kujitoa sadaka za nafsi na miili yetu kwa ajili ya kutetea wanyonge katika vita hii kubwa ya uchumi inayoongozwa na Rais Magufuli,” alisema Kindamba.

Pia alisema wanatarajia kufanya biashara ya huduma za simu kwa gharama nafuu zaidi watakaporejeshewa kampuni yao na pia kuiwezesha kulipa kodi zaidi serikalini
 
New details have emerged of the controversial transfer of Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL) shares to Celtel Tanzania (now Airtel Tanzania) as the board of the state-run telecoms dug in at a press conference yesterday, vowing war to recover the “lost shares”.

The spotlight turned on a board meeting, which is being accused of sealing an eyebrow-raising deal that President John Magufuli said was marred by underhand dealing.

TTCL board chairman Omar Nundu and CEO Waziri Kindamba said yesterday the company had officially embarked on a “war to recover the firm’s lost shares”.

“We understand that it will not be an easy ride but we believe we have all the facts and evidence to support our claims,” said Mr Nundu.

The big names in the share transfer saga came to light yesterday, though neither Mr Nundu nor Mr Kindamba could reveal them. These are some of the key players who were in the TTCL board when the shares were transferred, The Citizen understands. They include Mr Omar Issa, who was Judge Joseph Warioba’s proxy, and chair of the fateful meeting.

Also in attendance was the then-Treasury Registrar Agnes Bukuku, Yona Killagane, Moez Daya (who also represented Tito Alai), Edward Mwakyembe (who was also proxy for Felix Mrema), Gilder Kibola, who was the company secretary and the then TTCL chief executive officer George Mbowe. Warner Ruessel participated via teleconference.

The board is on the spotlight for approving the transfer of TTCL’s 10.25 million shares to an investor Mobile Systems International (MSI), which boosted its share to 60 per cent against 40 per cent of the government.

Reached for comment yesterday, Judge (rtd) Joseph Warioba said the board was simply implementing the requirements of a contract that was signed between Celtel and the government.

“The contract was between the government and Celtel, so it would be better if you talked to them,” he said.

And yesterday, Bharti Airtel said it had not received any official communication from the government over the issue.

“Whilst in the absence of any notice or communication from the government of Tanzania we cannot comment on the basis of the news reports, we would like to clarify that the mentioned transaction of 2005 was well before the acquisition of the 60 per cent shareholding in Celtel Tanzania Limited from Zain to a Bharti Airtel group entity in June 2010,” it said in a statement.

“In addition, we would like to highlight that our acquisition of the said 60 per cent shareholding in June 2010 was in full compliance with and following all approvals from the Government of Tanzania,” Bharti Airtel said in a statement yesterday.

The company said it would work closely with the government and take all steps necessary to resolve any doubts or concerns to the satisfaction of all of the stakeholders.

However, the TTCL board chairman said the company was seeking to retain its ownership lost in 2005 in a fresh bid to compete in the lucrative cellular mobile market.

According to latest figures from the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), TTCL currently commands a mere one per cent subscription share in a market where seven operators scramble for 40 million active subscriber identification module (Sim) cards.

Source: The Citizen
 
unamaanisha maamuzi yaliyofanywa na serikali ya CCM kwenye awamu zilizopita ni sawa na kucheza na akili za watanzania ?
vipi hili mkuu linatofauti na lile la kuuza nyumba za serikali kiholela hadi mpwa anapata ?
je swala la viongozi haohao wa CCM kutununulia kivuko kibovu cha mwaka 78 kwa bilioni 6.8 huoni kwamba ni mafisadi yaleyale ndani ya CCM yanayonyea akili za watanzania ?
 


Kufuatia kauli ya Rais Magufuli kutaka kuchunguzwa kwa kampuni ya simu ya Airtel kuwa ni mali ya kampuni ya simu ya TTCL, kampuni hiyo ya TTCL leo inatoa ufafanuzi juu ya swala hilo.

====
Mwenyekiti wa bodi ya TTCL mh Omary Nundu;

=>Kwanza niwashukuru kwa kufika hapa, tumewaalika kwa matukio yaliyotokea jana.
Jana magazeti mawili yaliandika habari kuhusu airtel. Walisema wamepata vyanzo kutoka serikali kwamba TTCL itadai airtel irudishwe kwao. Na kwamba wana vielelezo vya kudai irudishwe kwao. Na walisema walitutafuta na hatukupatikana, ndiyo maana tukaona tulitolee ufafanuzi.

Ni kitu gani kilitufanya tuanze kuongelea airtel?

=>Ili tutoe huduma kwa pamoja kuna wajibu wa sisi kufanya kazi kwa karibu sana.

=>Tulijitahidi kufanya hivo japo ilikuwa inatupa ugumu sana. Tukaangalia ni nani yuko karibu na sisi?

=>Sisi kama tunavyojua mpaka tar 23 Juni mwaka jana. Tukaangalia pia kwenye airtel tukakuta wanamilikiwa na serikali na mbia.

=>Sisi hatumiliki chochote, wamiliki ni serikali na mbia.

=>Ni kipi tulichogundua?Baada ya kuona airtel ni ndugu yetu. Tukaenda makampuni yanaposajiliwa tukapata taarifa na hapa ndani pia.

=>Sisi kama TTCL kabla ya kuanza kuwa kampuni. Mwaka 1993 Desemba 31, TTCL ilianzishwa. Ilianzishwa kwa mtaji wa shilingi bilioni 200.

=>Ilipofika mwaka tarehe 21 July 1999 thamani ya hisa za TTCL zikapanda kutoka bilioni 200 hadi 600 na mpaka leo thamani ya hisa za TTCL ni bilioni 200 hazijabadilika.

=>Ilipofika tarehe 23 Feb 2001, likaja wazo la kuibinafsisha TTCL. Akajitokeza mtu anayeitwa MSCI-Mobile Service Cellular Investment. Huyu alikuja kuwekeza kwenye TTCL ila mlolongo wake ni simu za mkononi.

=>Walitoa dola za kimarekani milioni 120 ili wapatiwe hisa 102,852,615. Sasa ukichukua hisa hizi ni asilimia 17 tuu na siyo asilimia. Hata hivyo hawakulipa dola milioni 120 badala yake walitoa dola milioni 65. Lakini walipewa hisa 35%.

=>Ilianzisha kampuni inaitwa Celnet mwaka 1998, ikawa kampuni ya TTCL. Ilipofikia kampuni ianze kufanya kazi ikawa siyo Celnet tena bali ikaitwa Celtel lakini vitu vyote walivyopewa kwa kuwa ni kampuni ya TTCL. Kampuni hii ilianzishwa na board members wa TTCL.

Ilifika mwaka 7 Mei 2001 wakasema mradi wake utakuwa ni bilioni 1. Maana yake hisa milioni 1 na kila hisa 1000. TTCL wakachukua hisa moja na mtu asiyejulikana akapewa hisa moja na hisa ile ikawa imeshikiliwa na David Banson kwa niaba ya mtu ambaye hajulikani. Kampuni ikawa inaanzishwa kwa mtaji wa sh 2000.

=>TTCL ikatia hela zake sh bilioni 5 ili kampuni ianze kufanya kazi. Kama kusingekuwa na hizo bilioni 5 Celtel isingefanya kazi. Pia TTCL ikatoa dola milioni 82 kwa kuiposha Celtel kwasababu ni kampuni yao. Tuliambiwa kulikuwa na riba lakini suala la riba hazikusemwa.

=>Ilipofika tarehe 7 Mei ikawa na hisa 999,999 sawa na milioni 1 kasoro moja. ilipofika tar 27 Nov 2001 yule David akamkabidhi mtanzania huyo alikuwa kwenye bodi ya TTCL na bodi ya Celtel.

=>Tarehe 05/08/2005 huyu aliyekabidhiwa hisa moja akawa mwenyekiti wa bodi yenye wajumbe wanne.

=>Mwenyekiti akachukua ile hisa moja akaikabidhi TTCL, TTCL ikawa inamiliki hisa zote za Celtel kwa hisa zote, lakini thamani ya bilioni 1 na bodi ikasema iongeze thamani ya hisa hadi bilioni 50.

=>Ikachukuliwa milioni 40 zikatiwa Celtel kama mtaji. Celtel ikawa inamilikiwa na TTCL kwa hisa bilioni 41. Sasa bilion 9 zikawa hazina mmiliki. Siku hiyo baada ya masaa TTCL akanyang'anywa hisa zake. Hisa hizi zikagawanywa kwa watu ambao hawakuwepo kwenye umiliki wa celtel.

=>Zikagawanywa kwa uwiano wa 65 serikali na Celtel 35. Serikali pamoja na yule mtu mwingine ukijumlisha hazifiki 50%. Kwahiyo serikali ikachukua hisa 26,650,000 na yule mwekezaji hisa 14,350,000 hapo serikali TR alikuwa ndiye majority shareholder.

Akachukua hisa nyingine 10,250,000 akampa mwekezaji mwekezaji akawa na hisa 24,600,000 yote haya yalifanyika siku moja tarehe 5/08/2005.

Ikaja ikawa inaitwa Zain, baadae airtel.

=>Mwaka jana 23 Juni , tulialikwa Bart ili wajitoe kutoka airtel. Lakini siku hiyohiyo walichukua dola milioni 40 na wakawakopesha tena dola milioni 28.

TTCL leo inadaiwa dola bilioni 76.

=>Sisi tunaomba serikali ilichukue kwa uzito jambo hili na ikiwezekana ile kampuni ya celtel irudishwe kwetu. Hata TTCL pesa imeanzishwa ushiriki wetu katika soko ni 0.85% tangu alipoingia Kindamba mwaka jana.

=>Sisi hatuna ubaya na mtu, tunatafuta haki hatuna haja ya kumdhulumu mtu.

Naomba niishie hapo.

=========

Mkurugenzi mkuu wa TTCL;

=>Habari za mchana, kwa majina naitwa Waziri Kindamba ni afisa mtendaji mkuu TTCL.

=>Sina mengi, ila sisi kama mgt tunaiunga mkono bodi yetu chini ya Mwenyekiti mzee Omary Nundu kuhakikisha dhulma, wizi na gilba hii iliyofanywa inawekwa wazi mbele ya macho ya watanzania. Kama rais alivyosema jana, sisi tuko tayari kutoa ushirikiano kwa asilimia mia moja. Ilianza kama celnet, ikawa celtel, zain na sasa airtel.

=>Sisi tunaona tunalo deni kwa mh rais ambaye ametuamini la kusema kweli kweli tupu.

=>Kwenye quarter 2017 ni 5 bilion, tumetengeneza faida kabla ya kodi 2.66 bilioni na faida baada ya kodi 1.8 na kodi tuliyolipa ni 786 kwa quarter inayoshia 2017.

Sisi tutahakikisha faida hii tunapeleka hazina. Tunaye mh rais ambaye ameonyesha nia ya vita ya kichumi na sisi tunamuunga mkono.

Najua moja kati ya swali litakuwa miaka yote mlikuwa wapi?

Lakini sisi tunasema, Aliyekutwa na ngozi ndiye mwizi wa ng'ombe. Tumejipanga kwa mapambano

Maswali

Swali:
Ni kina nani waliofanya mambo haya?

Kama tunavyosema hii vita ni kubwa na tusingependa wakipita barabarani kila mtanzania awanyooshee kidole wote waliofanya haya wanajitambua.

Swali: Mnataka muwe na gawio au muichukue airtel?

Sisi tunataka ufanywe mchakato uliopo turudishiwe airtel yetu.

Swali: Meseji gani mnataka iende kwa watanzania?

Tumewaitwa kwa sababu kulikuwa na sintofahamu. Tunataka mfahamu sisi kama TTCL hatuna hisa kwenye kampuni ya airtel. Hisa zilizopo ni za serikali na mwekezaji. Kwa takwimu na taarifa tulizo nazo airtel ni mali ya TTCL. Tukirudishiwa kampuni yetu tutakuwa na market share kubwa.

Lengo letu hawa mabwana waturudhishie kampuni yetu bila mkwaruzano kwasababu namna ilivyopatikana ni haramu na namna inavyojiendesha ni haramu.

Hatukuwahi kupata profit kwa miaka 15 lakini katika quarter hii tunadeclare profit.

Mwisho

Mkorogo karibia kama ule wa EPA. Kuna watu wanaitafuna hii nchi kwa raha zao! Michezo ya kitapeli tapeli na ya kijinga jinga machoni pa watu, yani utadhani mchezo wa karata tatu, lakini wanapiga mabilioni.

Eti mara sijui “Benson akapewa hisa moja kwa niaba ya mtu asiyejulikana”. Kumbe wasiojulikana huwa wanapiga madili vilevile?
 
Kumbe serikali yenyewe ndio ilipitisha kuuzwa kwa hisa hizo sasa mwekezaji wana tatizo gani hapa, ni kujitafutia matatizo mengine kwa kuwa hili la makinikia hatujamaliza tunaanza lingine au zilikamati zilipata msiko mzuri ndiyo zinataka iwepo nyingine ili watengeneze fedha kwa kuwa kwenye hili tutashindwa tu ni hasara kwa nchi hii
Kamata wahusika funga acha biashara ziendelee, kama mashirika yaliyouzwa kijanja janja yako mengi sana kuna kiwila coal mine na nyumba za serikali
 
Mimi nachukia kwanini hawatajwi majina semeni tu mwaka huo kulikuwa na hawa watu na signature ni mtu fulani, tunaficha nini au kalengwa mtu mmoja kisiasa tu halafu issue ifungwe. mwageni kila kitu sio mpaka tuende google tu search kina nani walikuwa mtu fulani sijui nani. wekeni kina nani walikuwa wanaongoza TTCL na Goverment wakati huko ambao walihusika na mchakato.
Mkuu, nchi hii imegeuzwa kuwa ya mazoba wa kutupwa. Kabla ya yote, subiri kama utaona kashfa yoyote ya ufisadi ikihitimishwa kisheria. Mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuamsha hamasa za "wajinga" na kisha kupotezea taratibu. Sio kwenye umeme (IPTL), madini (makinikia ya Acacia), n.k. Sijui ndio mtindo wa "amsha popo" halafu ziiii!

Kwa uozo uliofanyika TTCL ikiuzwa na kuanzishwa kwa Airtel tusubiri kusikia kama kweli kuna mwenye jeuri ya kuwagusa mafisadi wenyewe waliohusika. Hatuna muda na hizi talalila za kijinga zinazoendelea. Watu wanaitisha "press conference" halafu wanaongea huku nyuso zimejaa "haya". Wao wathubutu tu kumtaja even one of the key deal makers badala ya kushia kulalamika kuhusu "dhulma iliyofanyika".
 
Wakuu nimeisoma hii link na MZEE warioba anasema hakuna mjadala hapo wao kama bodi walitekeleza maelekezo toka serikalini. kama kuna issue yoyote hapo waulizwe serikali. sasa ninachokiona mimi ni kuwa tusipende kulaumu watu wenye hadhi na heshima zao tuwe makini na wenye busara. tuiche serikali ifanye kazi yake.
 
Hata ikitokea nimekufa kesho ntaenda kutoa ushuhuda huko peponi nitakapokua kwamba mungu kamtuma mtu Tanzania.Go Magufuli go... waspokuelewa sasa wataelewa tu miaka 100 inayokuja
Njoo sasa hivi nikusaidie kukutanguliza huko unakotaka kwenda kumuunga nkono magu.
 
Kila sentensi. Mtu asiyejulikana natamani nione anapigwa shaba huyo invisible maana sijui hakimu atatoa hukumu kwa nani au nae atamfunga "mtu asiyejulikana"
I hate this word to be honest
 
Wakuu nimeisoma hii link na MZEE warioba anasema hakuna mjadala hapo wao kama bodi walitekeleza maelekezo toka serikalini. kama kuna issue yoyote hapo waulizwe serikali. sasa ninachokiona mimi ni kuwa tusipende kulaumu watu wenye hadhi na heshima zao tuwe makini na wenye busara. tuiche serikali ifanye kazi yake.
kwaida ya binadamu ukiguswa sehemu laini lazima utingishike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom