Sakata Kibanda: CCM Mkoa Maalum watoa tamko, wamuweka pabaya Dr. Slaa!

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Mkoa maalum wa vyuo vikuu, kanda ya Dar es salaam, umefanya kikao cha kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuimarisha Mkoa huo na Chama kwa ujumla.

Pamoja na Ajenda hiyo, pia kikao hicho:-

· Kimelaani vikali matukio ya kuvamiwa, kudhuru mwili na kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa Dini na wanahabari. Mkoa umesikitishwa sana na tukio la kushambuliwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Ndugu Absalom Kibanda.
· Lakini pia, kimevitaka vyombo vya Dola kuwakamata, kuwashikilia na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliothibitika kuhusika na matukio ya namna hiyo bila kuangalia Itikadi za Kivyama, Cheo ama Kundi. Na pia kuyataka makundi ya kijamii, wanaharakati na wanasiasa kuacha kuingilia/kuvuruga kwa namna yeyote taratibu za kisheria na kiusalama.
· Pia, kuwataka wanausalama kumhoji kwa kina Dr Slaa juu ya tuhuma zake dhidi ya Kurugenzi ya Usalama wa Taifa (TISS) na kumtaka kuthibitisha madai yake kuwa baadhi ya watendaji wa taasisi hiyo muhimu na nyeti wanaripoti kwake kinyume cha utaratibu, kanuni na maadili ya taasisi hiyo.

Kwani tuhuma hizo ambazo Dr Slaa amekuwa akizisema mara kwa mara tangu kipindi cha Kampeni za Urais Mwaka 2010 zimeanza kuaminika, lakini pia zimepelekea wananchi sasa kukosa imani na Taasisi hiyo na zaidi kupoteza imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na kuwahakikishia Usalama wa maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la serikali.

Imetolewana:-

Daniel Zenda.

Katibu wa Wilaya (Dar es salaam.)
na Mwandishi wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kwamba kuna baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wanaripoti kwake, kimesababisha baadhi ya wananchi kukosa imani na vyombo hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkoa Maalum wa CCM Dar es Salaam baada ya kikao chao kutathimini mambo na matukio mbalimbali yanayolitikisa taifa kwa sasa.

Katika taarifa yao iliyosainiwa na Katibu wa Wilaya ya Dar es Salaam (ya kisiasa - CCM), Daniel Zenda ilisema kuwa Dk. Slaa amekuwa akitoa kauli hizo mara kwa mara tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2010, lakini hajaitwa kuulizwa wala kuchukuliwa hatua.


"Lakini pia kauli ya Dk. Slaa imesababisha wananchi wakose imani na Idara ya Usalama na zaidi kupoteza imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na kuwahakikishia usalama wa maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la serikali," ilisema taarifa hiyo.


Vijana hao wa CCM, wameitaka Idara ya Usalama kumhoji kwa kina Dk. Slaa athibitishe madai yake kuwa baadhi ya watendaji wa taasisi hiyo muhimu na nyeti wanaripoti kwake kinyume na utaratibu, kanuni na maadili ya taasisi hiyo.


Chama hicho pia kimelaani vikali matukio ya kuvamiwa, kudhuru mwili na kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa dini na wanahabari.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkoa huo umesikitishwa na tukio la kushambuliwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006, Absalom Kibanda.


"Tunavitaka vyombo vya dola kuwakamata, kuwachukulia hatua za kisheria wote waliothibitika kuhusika na matukio ya namna hiyo bila kuangalia itikadi za kivyama, cheo ama kundi.


"Na pia kuyataka makundi ya kijamii, wanaharakati na wanasiasa kuacha kuingilia/kuvuruga kwa namna yeyote taratibu za kisheria na kiusalama," ilisema taarifa hiyo.
 

Attachments

  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-vyuo.docx
    17.1 KB · Views: 223
What kind of reasoning is this?Badala ya kurudisha intergrity katika taasisi hiyo wanashughulikia watu wanaopata taarifa kutoka huko?What if kama wangekua ni maadui wa nje? Hizi akili primitive kama hizi zinapata wapi termerity ya kuitisha press conference au press release? mbona wanakidhalilisha sana chama chao na serikali kwamba ukomo wao wa kufikiria ndiyo umeishia kwenye busara za aina hii?

Ndiyo kazi waliyokua wakifanya lumumba leo?Maana huyo wa pili kutoka kulia aliyevaa shati la kijani ndiye Muandishi wa hili tamko leo.

attachment.php
 

Attachments

  • zenda.jpg
    zenda.jpg
    119 KB · Views: 1,643
Hivi nyie magamba mmekosa cha kusema?kwa nn mnakuwa vipofu hivyo?rama si mnamjua?anafanya kazi magogoni...ameshakamatwa?nendeni mkamhoji kwanza fastjet then ndio mje kwa Dokta,acheni upuuzi wenu tekelezeni ahadi zenu kwa wananchi mjipe uhalali ila mbinu zenu chafu hizi zimeshajulikana ndio maana mmeacha maadui ujinga,umasikini na maradhi na sasa mmeongeza adui wa nne ufisadi wakitamba badala yake mnapanga jinsi ya kuiua Chadema!!!!Laana hii haitawaacha kamwe siku si nyingi...
 
Kwanza hadi sasa Mkurugenzi wa usalama wa Taifa Rashid Othumani pamoja na waziri husika wa utawala bora(if there is any) alitakiwa awe amejiuzulu.Hii ni gross misconduct!
 
Kama TISS ipo,mara ngapi tunaona maharamia toka somalia,ethiopia wanakufa katikati ya nchi kama morogoro,kiteto!wameingiaje bila TISS kujua?
 
Elimu mnayoipata bado haiwasaidii mana mnakalia kufanya majungu badala ya kuangalia Taifa linaenda wapi. Binafsi naona nyie ni wehu tu katamko kenu kalikoka up uuzi mwingi. Nyamba fu nyie kasomeni
 
sijawahi kusikia dr.slaa akisema kuwa kurugenzi ya tiss wanaripoti kwake.ingekuwa vyema kama ungejulisha lini na wapi alisema hayo maneno?
 
Na Mwigulu Nchemba ahojiwe na kukamatwa maana yeye alisema ana mkanda unao onesha jinsi chadema wanavyo panga mauaji ya wananchi hadi leo yupo mtaani labda mtwambie huo mkanda ndio huu wa lwakatare aliokuwa anasema na yeye ndio ameuweka youtube!

Hakuna siri kuwa ccm na TISS ni wahusika wakuu wala hilo halina siri na tunajua Dr slaa kawshika pabaya hile mbaya na huo ndio ukweli.

Mgekuwa wasomi wa kweli na mnao jua kuhoji msingemtenganisha Mwigulu Nchemba na hili swala.

Ccm+mwigulunchemba+TISS=lwakatare clip!

Ukweli umeanza kuwaingia na mmeanza kuropoka!

Kwanini hamjiulizi hadi sasa lwakatare hajapelekwa mahakamani na wakati masaa24 yalishapita? Kwa nini tusiseme hapa kuna maagizo maalum kutoka juu?
Hili picha mmelifanyia production wenyewe alaf mnashangaa matokeo yake!
Cc Nape Nnauye
Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
Hicho kikao inaonekana wamekaa wahitimu wa shule za ununda. Taasissi zote za awamu ya nne zinaripoti kwa Dr. Slaa kwa vile zinamtambua kuwa yeye ndiye rais halali. hilo nalo wanashindwa kulitambua?
 
Kwani TISS haijui kuwa Rais aliyeshinda uchaguzi huo 2010 alikuwa Dr. Slaa? Wanatoa taarifa kwa Rais aliyehujumiwa na chombo hicho hicho......Nakupenda Tanzania kwa maajabu yako.
 
Back
Top Bottom