Saini ya Pinda yaghushiwa bungeni; kunawaathiri zaidi wabunge wa upinzani, hasa wa Chadema

Fake MPs, fake proceedings, fake bills, fake enactments, fake..........!
False representation, forged documents, bogus leaders,............!
 
Kweli kabisa na ninakubalianan na wewe, usalama wa taifa upo kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu binafsi na uroho wa watu wa chahce, visiku vyawe naghamba
ni bunge la kihistoria na la mfano wakijuha duniani, aibu hii kwa watanzania.
 
Zaidi ya uijuavyo Tanzagiza!!!!!!!!! Na bado viti maalumu tutawawekea mchanga na chupa wacheze rede huko mjengoni!!!!!
 
Mazoezi huanza utotoni, watoto huiga tabia na mienendo ya wazazi wao hata kusema wanafanya kazi za wazazi wao katika michezo yao.
Serikari yetu ni corrupt, na inafanya kila aina ya mambo yasiyofaa ya wizi, ufekifeki na mambo kama hayo.
Hao wanaotumia saini ya pinda wanafanya mazoezi ili baadaye wakikua( wakipewa nyadhifa) wawe na ujuzi wa kughushi nyaraka kwa utendaji wao serikarini.
Like father like son.
 
Kwa ufahamu wangu mdogo wa Mambo ya Kisheria, nadhani kughushi saini ya mtu yeyote ni Kosa la jinai. Na sasa kama saini hiyo inagushiwa ndani ya muhimili mmoja kati ya ile mitatu ya uongozi wa nchi, tena muhimili wa kutunga sheria, je ni suala dogo hilo? Kibaya zaidi ni saini ya Kiongozi wa Shughuri za Serikali Bungeni. Jamani, mamlaka iko wapi? Usalama mpo wapi? Hivi kweli ktk team yote ya viongozi wetu serikalini hakuna hata mmoja wa kusisimama na kukemea waziwazi haya mambo? Juzi tumesikia habari za Samaki wa Sumu, mamlaka husika karibu 4 hivi zilikuwa wapi? TFDA, TRA, TPA, TBS pamoja na Wizara ya Afya?, Tupo bado kwenye lindi la tatizo la umeme, porojo tu, Wiki hilohilo tena, rushwa kwa wabunge toka kwa hao akina Gairo sijui? Mambo ya vijisenti, mara takululu, mara DPPPPs, mara Watu wa mambo ya kimataifa wanasema wahusika wapo, lakini kuna mamlaka za kuwatajani. Jamani mnashida gani na mnatupeleka wapi?

Kusema ule ukweli, nilisema ktk thread moja wiki iliyopita, SERIKALI HII MNATUTIA KINYAA TENA KINYAA CHA KUTAPIKA, HEMBU JIPAMBANUENI KAMA MMEKWAMA. Kama mtu umeshikwa na tumbo la kuendesha (Kuharisha), dawa yake ni kukimbilia chooni ukajisitiri, huwezi kabisa kuizuia hali hiyo, na kama utajifanya kuizuia, basi Kinyesi kitakuumbua. Serikali, msisubili kufika huko.

My Take: Kuna haja ya kuanza kutengeneza Kikosi kazi ndani ya JWTZ. Ili siku moja mambo ya Katiba yawekwe pembeni, na watu waende kwa Amri kwa miaka kama miwili hivi, kusafisha halii hii iliyopo ktk Utumishi wa umma, na kisha kurudi ktk katiba, nina uhakika ndiyo suluhisho tunalolihitaji Watanzania.
 
Back
Top Bottom