SAIKOLOJIA YA AKILI( chapter2) 18:40:60

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
441
500
Habari za asubuhi ndugu zangu;Baada ya makala ya brain programming leo nimekuja na hii kanuni ya 18:40:60.
Hivi karibuni tumeona ujio wa mabilionea wengi vijana wadogo duniani hasa katika sekta ya technolojia;masuala ya technolojia yanajitaji akili ya hali ya juu sana.
Ni nini kinakufanya ushindwe kusonga mbele?.
18-40
Binadamu anapokuwa na miaka 18-40 kila anachofanya hudhani ya kuwa watu wanamuangalia na kuwaza ya kuwa watu humuwazia sana,so chochote anachofanya kwenye maisha ya kile siku yanakuwa based na nini watu wanasema juu yake,hata akivaa nguo mpya anadhani kila mtu anajua kavaa nguo mpya.
40-60
Mtu anapfikisha miaka arobaini huona mambo mengi kwenye maisha hayajafika level aliyokua anataka ifikie ivyo sasa anasema: SITAJALI NINI WATU WANASEMA JUU YANGU, hivyo hupambana na maisha lakini anahisi watu wanamsema na kumfuatilia lakini hajali kitu .
60 years na kuendelea
Binadamu anapofika miaka 60 anagundua kuwa hakuna mtu alikua anamuwaza kumbe yalikua ni mawazo ya fikra zake tuu;Alikua mfungwa wa fikra hasi katika gereza la akili yake mwenyewe.
Badilika hakuna mtu anakuwaza wala kukufuatilia. Tangu nigundue hii kanuni miaka saba nyuma nilikua huru sana na mpaka sasa nipo huru.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom