SAIKOLOJIA: Wema wa mwanzo hufunikwa na ubaya wa mwisho. (Mfahamu Dr. Fitz Haber mshindi wa Nobel prize 1918)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
‘Hupo msimu wa mvua na mafuriko katika maisha ambapo sisimizi hugeuka chakula cha samaki, pia hupo msimu wa kiangazi na ukame samaki nao hugeuka chakula cha sisimizi”
1544212115573.png

(Mabaya ya mwisho hufanya wema wa mwanzo usikumbukwe)
Habari za kipindi kirefu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala za Saikolojia kupitia jukwaa hili. Ni kipindi kirefu kweli nilipotea kutokana na sababu zilizokuwa nje na uwezo wangu ikiwemo na majukumu ya hapa na pale.

Basi leo nimeandaa makala kuhusu kanuni za kimaisha nikiangazia hasa sehemu moja tu ya “Heri mwanzo mbaya wenye mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri wenye mwisho mbaya”

Pengine unaweza ukawa hujawahi kusikia kanuni zinazoongoza kimaisha ndio zipi hizo. Sababu naposema kanuni zinazoongoza maisha ya wanadamu wengi hasa waswahili wamezitafsiri kupitia Semi mithali na nyingine nyingi utazipata katika vitabu vya maandiko.
Nikupe mfano moja ya kanuni hizo ambazo zimetafsiriwa kupitia katika semi za Kiswahili

Mfano
i.Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
ii.Apandacho mtu ndicho atakachovuna
iii.Ushinde ubaya kwa wema
iv.What goes around comes around

Nini maana ya kanuni (Kamusi ya Kiswahili)Pengine ni misemo tumeizoea sana maisha yetu na hasa kuiona ni kitu cha kawaida sana na pengine tumekizoea sana hata mashuleni na mitaani kukitamka lakini ndio uhalisia wa maisha.

Tafsiri ya kanuni?
Taratibu za kuendesha au kufanya jambo desturi kaida masharti kawaida mila.Sababu kila kitu duniani unachokiona chochote kinatumika au kinaendana au kinaendeshwana kanuni flani.

Na kanuni hiyo ndio inayozaa mavumbuzi leo tukizungumzia kanuni za fizikia nyingi ndio tunapata uvumbuzi wa Ndege, Magari pamoja na teknolojia nyingi na kanuni hizo zinapovunjwa au kutozingatiwa lazima madhara yafuatie.

Muda si mrefu kuna ajali ya kivuko ambayo imetokea ziwa la ictoria Mv Nyerere na sababu kubwa ya ajali kwa mujibu wa uchunguzi na baadhi ya mashahidi ilikuwa kujaza watu na mizigo kupita kiasi.

(Yaani kwa lugha ngumu kidogo kukiukwa kwa kanuni za watengenezaji ambacho kuna kiwango flani kiliitajika tu ambacho kivuko ndipo kiliweza kubeba watu na mizigo yao, matokeo ya kukiuka kanuni hiyo ndio ikazaa madhara ya kuzama na kupoteza ndugu wetu wengi).Basi pasipo kupoteza muda turudi tuangalie kanuni inayobeba dhima ya somo letu leo tukijifunza kupitia Dr Fritz Haber mshindi wa Nobel Prize katika taaluma ya Kemia akitokea nchini Ujerumani mwaka 1918.

CASE STUDY (Dr Fritz Haber mshindi wa Nobel Prize)MWANZO MZURI
1544212162585.png
(Nembo aina ya stempu iliotoka baada ya Dr Fritz Haber kushinda tuzo ya Nobel Prize)

Dr Fritz Haber ni mzaliwa wa Breslau nchini Prussia (Ambayo sasa ni Ujerumani) mwenye asili ya kiyahudi kama vile isivyokuwa jambo geni hasa kwa Wayahudi katika Nyanja za uvumbuzi wa vitu mbalimbali ulimwenguni.

Katika masuala ambayo yalimsumbua sana Fritz wakati akiwa ni kijana ni kutaka heshima ya kuonekana na yeye pia ni Mjerumani kwa kuzaliwa pasipo kuzingatia asili yake ya kiyahudi. Hivyo ndio ilikuwa ni masuala ambayo yalimuangaisha sana tangia akiwa shule za chini kabisa, familia yake bado ilikuwa ni ku-maintain uasili wao kama wayahudi.

Alikuwa ni moja ya wanafunzi walionesha nyota njema uanzia asubuhi kupitia ufaulu wake mzuri katika masomo ya sayansi hadi alipokuja jiunga na masomo ya chuo kikuu akijikita katika kemia. Baadae baada ya kuhitimu alirudi kufanya kazi katika biashara za kemikali, kutokana na baba yake kuwa na mtandao mkubwa katika makampuni ya kemikali hivyo ilikuwa nafasi nzuri sana kwake kwenda makampuni tofauti kufanya kazi za muda ilikuweza kuongeza uzoefu na ndipo mawazo ya ubunifu katika tasnia ya kemikali yalipotokea, hivyo akamuomba baba yake aende chuoni tena kujiendeleza na alipomaliza akarudi kwenye biashara za baba yake.

Mpaka walipokuwa wakiingia katika migogoro tofautitofauti kiasi kwamba wakaamua kukubaliana kwamba hawataweza kufanya kazi pamoja tena.

Baadae ndipo akapata kazi yake ya kwanza kama msaidizi wa Ludwig Knorr kwenye chuo kikuu cha Jena na baadae Knorr akamtambulisha na kumsihi profesa mwingine wa Kemia wa chuo cha Karlsruhe ambaye aliekuwa akijishuhulisha sana na masuala ya uvumbuzi hasa katika teknolojia za kemikali hasa kwenye viwanda vya nguo. Na hivyo akachukuliwa kama msaidizi pia wa Professor huyo.

Nyota yake baada ya hapo ndipo ilipozidi kuangaza na kuanza kupata fursa mbalimbali za kufundisha vyuoni hadi hapo alipotunikiwa kuwa Profesa wa fizikia na chemia na waziri wa Elimu katika chuo cha Karlsruhe.

Baada ya kupitia na kujifunza kanuni za watangulizi mbalimbali katika tasnia ya kemia ndio akapata msingi wa kanuni mpya ambayo leo hii inatumiwa katika kutengeneza mbolea ambazo ni salama na zenye kusaidia kukomaa zaidi kwa mimea mashambani, iliweza kusaidia kuokoa mabilioni ya watu hata hii leo ulimwenguni dhidi ya mabara ya njaa . kwa wale ambao wamepitia Organic chemist wanaweza wakaeleza vizuri zaidi kuhusu “Haber Process”Hivyo mpaka kufikia baadae mwaka 1918 akapewa na tuzo ya heshima ya Nobel Prize kutokana na uvumbuzi mzuri wake.

“..Inaelezwa kuwa kila wanadamu wawili katika watu watano ulimwenguni ni wanufaika wa uvumbuzi wa Dr Fritz Haber”

KUANZA NA KUELEKEA MWISHO MBAYA
1544212226492.png

(Dr Fritz akikagua siraha zake za kemikali kabla ya kwenda kujaribiwa dhidi ya adui zao wakati huo Uingereza urusi na ufaransa)

Kuibukakwa vita ya kwanza ya dunia ndio ilianza tengeneza mwisho mbaya au anguko la mwanzo mzuri na kufuta wema wote wa Dr Fritz Haber na kumbukumbu au alama nzuri kwa dunia aliyoiacha sababu ni wachache sana wasomi ndio walioweza kuchambua mema aliyoyaanza.

Hali yake ya kutaka kujionesha ni mzalendo mjerumani na si myahudi kwa asili ndipo alijiunga na jopo la maprofesa wenzake ambao wakitumika katika kikosi cha uvumbuzi wa siraha mbalimbali ambazo kwa mara ya kwanza ndio zinatumika duniani, Yaani siraha za kemikalipamoja na matumizi ya siraha za gesi zenye sumu katika viwanja vya mapambano.

Matumizi ya siraha za kemikali licha ya kukiuka tu sharia za utu na ubinadamu (Ijapokuwa Vita ni mgogoro ambao hauepukiki kwa binadamu) na pia mkataba wa Hague convection1907 ambapo Ujerumani ilikuwa ni moja ya nchi iliyosaini.

Kujionesha mzalendo kulizidi mzalia tunu mbalimbali ikiwemo kupanda cheo katika wizara ya vita ya Ujerumani na pamoja katika jeshi la ujerumani kama kapteni huku akitunikiwa nishani mbalimbali za heshima katika jamii.

Fritz alikuwa na falsafa tatu kichwani pake na alizozizungumza mara kwa mara

i. Ni Nchi kwanza na uzalendo, wakati wa amani wanasayansi tunainufaisha dunia yote lakini wakati wa vita lazima masirahi ya nchi yawe ya kwanza.

ii. Kuimaliza vita haraka kwa gharama yoyote (Matumizi ya siraha za kikemikali za sumu).

iii.Kifo ni kifo tu kiwe cha sumu au risasi.

Kwa mara ya kwanza anavumbua gesi ya sumu ya aina Chloride pamoja na vilipukizi ambavyo vinatumika katika pigano la Ypres 1915 na kutokana na matokeo ya maangamivu ya watu wengi hasa upande wa maadui zao na kufikia majeruhi 65,000(yaani upande wa Uingereza, Urusi na Ufaransa), na baada ya mafanikio hayo anapandishwa cheo cha kuwa kapteni katika jeshi la ujerumani.

Na usiku huo akisherekea tunu na tuzo aliyoipata kutoka kwa Kansela wa ujerumaniusiku huo huo kipenzi mke wake Clara Immerwahr anajiua kwa msongo wa mawazo kutokana na kazi anayoifanya mumewe ya maangamizi jambo lililomuumiza sana moyo Dr Fritz na kumpa upweke.

Vita inaisha huku Ujerumani ikishindwa vibaya na haishii hapo anaanza kuishi kwa hofu ya kushitakiwa kama muhalifu wa kivita kutokana na uhusika wake katika utengenezaji wa siraha za sumu kutoka katika mataifa washindi.

Anajaribu tena kuonesha uzalendo kwa taifa lake hasa kuisaidia serikali mpya Weimar Republic kuinua uchumi kwa kuvumbua namna ya kuchukua dhahabu iliyo baharini ili kusaidia Ujerumani kutoka katika ukata wa kiuchumi uvumbuzi ambao ulikwama.

ANGUKO LINAANZA KUCHIPUZA
1544212263012.png

(Kuibuka kwa sera za kifashisti nchni ujerumani chini ya cha Nazi kilichoongozwa na mawazo ya veteran wa vita ya kwanza ya dunia Adolph Hitler)

Mwaka 1930s hali ya ubaguzi na sera za kifashisti unazidi shamiri kiasi kwamba madai ya uzalendo wa Fritz yanatupiwa mbali. Siku moja binti yake wakati anaenda katika tasisi aliyoifanyia kazi Dr Fritz anakutana na bango linalosema “Dr Hebz Myahudi hatakiwa hapa” inamuumiza sana Fritz anaamua kujiuzulu kama mkemia. Kama ilivyokuwa kwa wayahudi wenye nyadhifa za juu wakati huo akiwemo Albert Einstein wanaondoshwa kwa kufukuzwa au kukimbia wenyewe nchini ujerumani.

Baadae alienda kuishi Ufaransa na akahamia Uhispania na kuenda kuishi pia Switzerland wakati huo afya yake ikiwa mbaya sana.

Licha ya mazuri aliyotenda hawali hayakuweza kufutika alialikwa chuo cha Cambridge na kwa mara ya kwanza akakutana na wanasayansi ambao walikuwa ni maadui katika vita ya kwanza ya dunia wapo waliomsamehe na ndio waliomsaidia kuweza kuondoka ujerumani hasa majira ya joto la ubaguzi anti semitic na wapo waliokataa hata kupeana mikono nae katika mualiko wake nchini uingereza.

Na hata halipopata kazi nchini uingereza hakupata nafasi ya kuishi alielekezwa akaishi eneo la Israel mashariki ya kati wakati huo likiwa bado koloni la muingereza akuweza kufika akiwa njiani akafariki.

BAADA YA KIFO CHAKE

Kama mwanasayansi alieponzwa na dhana ya uzalendo pasipo kuzingatia misingi ya utu na upendo kwa wanadamu wengine pasipo mipaka ya utaifa na jamii.

Hali ya nchini ujerumani licha ya kuondoka na familia yake wapo jamaa zake waliobakia, ijapokuwa alijitahidi sana kuwaokoa mikononi mwa sera za kifashisti kutokana na nafasi yake ya umaarufu na kulitumikia taifa la ujerumani. Ndugu zake wakaribu hasa dada zake walikuwa ni moja wa watu waliouwawa katika vyumba vya sumu ambayo ni gesi aliyoibuni yeye mwenyewe, katika mauaji yaliyojulikana kama “Holocaust” ambapo inakadiliwa wayahudi ambao ni watu wa jamii ya kwake zaidi ya milioni 6.

Baadae mzaliwa wa kwanza wake aalichukua maamuzi ya kujiua 1946 na baadae binti wake wa mwisho aliamua kujiua mwaka 1949 baada ya kuambiwa utafiti wake wa dawa ya kusaidia mtu aliyepatwa na madhara ya sumu Chlorine gas (Sumu aliyeibuni baba yake) kuachwa na serikali ya Marekani.

NINI TUNAJIFUNZA WATU WA KIZAZI HIKI KANUNI MUHIMU ZINAZOFANYA KAZI.

1544212319886.png

(Kundi la watu waliotengwa kwa ajili ya kwenda kuuliwa kwenye vyumba vya Gesi za sumu gereza la Auschwitz)

  • Zipo kanuni za kimaisha ambayo mojawapo ni hii nimekuandikia “Ukianza vyema na kumaliza vibaya hata ule wema wa kwanza hautakumbukwa” na kuhidhibitisha hasa zinazofanya kazi katika maisha yetu ya kila siku kwa kujua au kutokujua na tunapokiuka huwa na madhara pia kama jinsi madhara yanavyokuwa tunapoenda kinyume na kanuni ya matumizi ya vitu mbalimbali vya kieletroniki

Fritz anakumbukwa zaidi katika kubuni gesi za kemikali za maangamizi na vilipuzi katika vita ya kwanza ya dunia kuliko uvumbuzi wa aina bora za mbolea katika kilimo iliyosaidia maelfu ya binadamu dhidi ya mabaa ya njaa na pia dawa za kuulia wadudu mashambani, lakini kinachokumbukwa zaidi ni mauaji ya kemikali katika vita ya kwanza na yale ya watu wa jamii yake zaidi ya milioni 6 (Holocaust).

(mfano injini zozote hutumia mafuta lakini kila moja ina kanuni za matumizi yake ili ifanye kazi ikiwemo na aina ya mafuta yake, ukiweka mafuta ya dieseli katika injini ya petrol basi utaiua injini hiyo )

    • Kusamehe na kuishi kwa kujali na kuzingatia utu sababu hujui nani hatakusaidia kesho. Unayemuona kamaadui yako leo ndio msaada wako kesho na rafiki yako leo anaweza kuwa adui wako kesho,

Mfano wale Dr Fritz alioona kama maadui zake na kubuni mbinu za kuwaangamiza ndio waliomuokoa mikononi mwa Adolf Hitler sababu Hitler angemuua tu na wale aliowaona rafiki na nduguze ndio waligeuka na kutaka kumuua na pia piakuua ndugu zake wa karibu pamoja na watu wa jamii yake zaidi yamilioni 6 (Wayahudi).

( Hii tutajifunza tena kuna mada naiandaa katika eneo hili).

    • Ukipanda wema utavuna mema na pia ubaya utavuna ubaya “apandacho mtu ndio atakachokivuna”. Usijidanganye kijana, binti baba au mama au hata mzee leo haya mabaya unayowafanyia watu na kuwaumiza huwa yanarudi (fitina ikimaliza kazi au ubaya sharti urudi kule ulipozaliwa au kutokea) kwa namna tofauti na hata utakapofariki yataendelea kula vizazi vyako katika saikolojia tunaita sababu za kurithi in heretic factor na katika imani inaitwa Laana au Curse.

Hii tunaona pia katika visa vya kujiua katika watoto wa Fitz ambao wengi wanaonesha kuelemewa na hatia ya aliyoyafanya baba yao na pia ndugu zake wa karibu waliouliwa na hiyo hiyo gesi aliobuni.

HITIMISHO

Yapo mengi ya kujifunza hasa katika udhibitishaji wa kanuni ya unapoacha mema na ukaanza kutenda mabaya wema wako unasahaurika na heri mwanzo mbaya na mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri na mwisho mbaya. Hizi ndio kanuni ya kimaisha na inafanya kazi ulimwenguni kote.

Jifunze Jirekebishe na badili mfumo wa maisha yako asante.

KUHUSU MWANDISHI,
Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Pia ni Msomaji wa Vitabu vinavyohusu Falsafa, Nyurolojia, Historia, Maandiko pamoja na Vitabu vinavyooelezea maisha ya watu mashuhuri (Biography book).
 
Mimi kutokana na kusoma kwangu hizi nakala nimejaribu kuishi maisha fulani katika jamii ambapo nimejaribu kuweka watu wanaonizunguka katika jamii kujiona sisi sote ni bora na hakuna bora zaidi ya mwingine.
Ni wachache sana wamenielewa na katika wachache hao ni mmoja tu alifaulu vizuri. Anaitwa Juma, Juma alinielewa kwa kuniambia aliwahi kuambiwa na babu yake, "Ukienda kwenye jamii ngeni weka sana ukaribu na mtu anayechukiwa na jamii hiyo utajifunza mengi sana kupitia yeye".
 
Si mbaya. Sasa jifunze na lugha maana kuna maneno ya kiswahili yanakushinda.wenzangu wameelezea tayari sina haja kurudia. Unapoandika bandiko hata kama ni zuri unapokosea lugha linatu kwaza sisi wengine. Lina "bore" so pata muda pia ujifunze lugha ya kiswahili.

‘Hupo msimu wa mvua na mafuriko katika maisha ambapo sisimizi hugeuka chakula cha samaki, pia hupo msimu wa kiangazi na ukame samaki nao hugeuka chakula cha sisimizi”
View attachment 959690
(Mabaya ya mwisho hufanya wema wa mwanzo usikumbukwe)
Habari za kipindi kirefu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala za Saikolojia kupitia jukwaa hili. Ni kipindi kirefu kweli nilipotea kutokana na sababu zilizokuwa nje na uwezo wangu ikiwemo na majukumu ya hapa na pale.

Basi leo nimeandaa makala kuhusu kanuni za kimaisha nikiangazia hasa sehemu moja tu ya “Heri mwanzo mbaya wenye mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri wenye mwisho mbaya”

Pengine unaweza ukawa hujawahi kusikia kanuni zinazoongoza kimaisha ndio zipi hizo. Sababu naposema kanuni zinazoongoza maisha ya wanadamu wengi hasa waswahili wamezitafsiri kupitia Semi mithali na nyingine nyingi utazipata katika vitabu vya maandiko.
Nikupe mfano moja ya kanuni hizo ambazo zimetafsiriwa kupitia katika semi za Kiswahili

Mfano
i.Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
ii.Apandacho mtu ndicho atakachovuna
iii.Ushinde ubaya kwa wema
iv.What goes around comes around

Nini maana ya kanuni (Kamusi ya Kiswahili)Pengine ni misemo tumeizoea sana maisha yetu na hasa kuiona ni kitu cha kawaida sana na pengine tumekizoea sana hata mashuleni na mitaani kukitamka lakini ndio uhalisia wa maisha.

Tafsiri ya kanuni?
Taratibu za kuendesha au kufanya jambo desturi kaida masharti kawaida mila.Sababu kila kitu duniani unachokiona chochote kinatumika au kinaendana au kinaendeshwana kanuni flani.

Na kanuni hiyo ndio inayozaa mavumbuzi leo tukizungumzia kanuni za fizikia nyingi ndio tunapata uvumbuzi wa Ndege, Magari pamoja na teknolojia nyingi na kanuni hizo zinapovunjwa au kutozingatiwa lazima madhara yafuatie.

Muda si mrefu kuna ajali ya kivuko ambayo imetokea ziwa la ictoria Mv Nyerere na sababu kubwa ya ajali kwa mujibu wa uchunguzi na baadhi ya mashahidi ilikuwa kujaza watu na mizigo kupita kiasi.

(Yaani kwa lugha ngumu kidogo kukiukwa kwa kanuni za watengenezaji ambacho kuna kiwango flani kiliitajika tu ambacho kivuko ndipo kiliweza kubeba watu na mizigo yao, matokeo ya kukiuka kanuni hiyo ndio ikazaa madhara ya kuzama na kupoteza ndugu wetu wengi).Basi pasipo kupoteza muda turudi tuangalie kanuni inayobeba dhima ya somo letu leo tukijifunza kupitia Dr Fritz Haber mshindi wa Nobel Prize katika taaluma ya Kemia akitokea nchini Ujerumani mwaka 1918.

CASE STUDY (Dr Fritz Haber mshindi wa Nobel Prize)MWANZO MZURI View attachment 959691(Nembo aina ya stempu iliotoka baada ya Dr Fritz Haber kushinda tuzo ya Nobel Prize)

Dr Fritz Haber ni mzaliwa wa Breslau nchini Prussia (Ambayo sasa ni Ujerumani) mwenye asili ya kiyahudi kama vile isivyokuwa jambo geni hasa kwa Wayahudi katika Nyanja za uvumbuzi wa vitu mbalimbali ulimwenguni.

Katika masuala ambayo yalimsumbua sana Fritz wakati akiwa ni kijana ni kutaka heshima ya kuonekana na yeye pia ni Mjerumani kwa kuzaliwa pasipo kuzingatia asili yake ya kiyahudi. Hivyo ndio ilikuwa ni masuala ambayo yalimuangaisha sana tangia akiwa shule za chini kabisa, familia yake bado ilikuwa ni ku-maintain uasili wao kama wayahudi.

Alikuwa ni moja ya wanafunzi walionesha nyota njema uanzia asubuhi kupitia ufaulu wake mzuri katika masomo ya sayansi hadi alipokuja jiunga na masomo ya chuo kikuu akijikita katika kemia. Baadae baada ya kuhitimu alirudi kufanya kazi katika biashara za kemikali, kutokana na baba yake kuwa na mtandao mkubwa katika makampuni ya kemikali hivyo ilikuwa nafasi nzuri sana kwake kwenda makampuni tofauti kufanya kazi za muda ilikuweza kuongeza uzoefu na ndipo mawazo ya ubunifu katika tasnia ya kemikali yalipotokea, hivyo akamuomba baba yake aende chuoni tena kujiendeleza na alipomaliza akarudi kwenye biashara za baba yake.

Mpaka walipokuwa wakiingia katika migogoro tofautitofauti kiasi kwamba wakaamua kukubaliana kwamba hawataweza kufanya kazi pamoja tena.

Baadae ndipo akapata kazi yake ya kwanza kama msaidizi wa Ludwig Knorr kwenye chuo kikuu cha Jena na baadae Knorr akamtambulisha na kumsihi profesa mwingine wa Kemia wa chuo cha Karlsruhe ambaye aliekuwa akijishuhulisha sana na masuala ya uvumbuzi hasa katika teknolojia za kemikali hasa kwenye viwanda vya nguo. Na hivyo akachukuliwa kama msaidizi pia wa Professor huyo.

Nyota yake baada ya hapo ndipo ilipozidi kuangaza na kuanza kupata fursa mbalimbali za kufundisha vyuoni hadi hapo alipotunikiwa kuwa Profesa wa fizikia na chemia na waziri wa Elimu katika chuo cha Karlsruhe.

Baada ya kupitia na kujifunza kanuni za watangulizi mbalimbali katika tasnia ya kemia ndio akapata msingi wa kanuni mpya ambayo leo hii inatumiwa katika kutengeneza mbolea ambazo ni salama na zenye kusaidia kukomaa zaidi kwa mimea mashambani, iliweza kusaidia kuokoa mabilioni ya watu hata hii leo ulimwenguni dhidi ya mabara ya njaa . kwa wale ambao wamepitia Organic chemist wanaweza wakaeleza vizuri zaidi kuhusu “Haber Process”Hivyo mpaka kufikia baadae mwaka 1918 akapewa na tuzo ya heshima ya Nobel Prize kutokana na uvumbuzi mzuri wake.

“..Inaelezwa kuwa kila wanadamu wawili katika watu watano ulimwenguni ni wanufaika wa uvumbuzi wa Dr Fritz Haber”

KUANZA NA KUELEKEA MWISHO MBAYA
View attachment 959694

(Dr Fritz akikagua siraha zake za kemikali kabla ya kwenda kujaribiwa dhidi ya adui zao wakati huo Uingereza urusi na ufaransa)

Kuibukakwa vita ya kwanza ya dunia ndio ilianza tengeneza mwisho mbaya au anguko la mwanzo mzuri na kufuta wema wote wa Dr Fritz Haber na kumbukumbu au alama nzuri kwa dunia aliyoiacha sababu ni wachache sana wasomi ndio walioweza kuchambua mema aliyoyaanza.

Hali yake ya kutaka kujionesha ni mzalendo mjerumani na si myahudi kwa asili ndipo alijiunga na jopo la maprofesa wenzake ambao wakitumika katika kikosi cha uvumbuzi wa siraha mbalimbali ambazo kwa mara ya kwanza ndio zinatumika duniani, Yaani siraha za kemikalipamoja na matumizi ya siraha za gesi zenye sumu katika viwanja vya mapambano.

Matumizi ya siraha za kemikali licha ya kukiuka tu sharia za utu na ubinadamu (Ijapokuwa Vita ni mgogoro ambao hauepukiki kwa binadamu) na pia mkataba wa Hague convection1907 ambapo Ujerumani ilikuwa ni moja ya nchi iliyosaini.

Kujionesha mzalendo kulizidi mzalia tunu mbalimbali ikiwemo kupanda cheo katika wizara ya vita ya Ujerumani na pamoja katika jeshi la ujerumani kama kapteni huku akitunikiwa nishani mbalimbali za heshima katika jamii.

Fritz alikuwa na falsafa tatu kichwani pake na alizozizungumza mara kwa mara

i. Ni Nchi kwanza na uzalendo, wakati wa amani wanasayansi tunainufaisha dunia yote lakini wakati wa vita lazima masirahi ya nchi yawe ya kwanza.

ii. Kuimaliza vita haraka kwa gharama yoyote (Matumizi ya siraha za kikemikali za sumu).

iii.Kifo ni kifo tu kiwe cha sumu au risasi.

Kwa mara ya kwanza anavumbua gesi ya sumu ya aina Chloride pamoja na vilipukizi ambavyo vinatumika katika pigano la Ypres 1915 na kutokana na matokeo ya maangamivu ya watu wengi hasa upande wa maadui zao na kufikia majeruhi 65,000(yaani upande wa Uingereza, Urusi na Ufaransa), na baada ya mafanikio hayo anapandishwa cheo cha kuwa kapteni katika jeshi la ujerumani.

Na usiku huo akisherekea tunu na tuzo aliyoipata kutoka kwa Kansela wa ujerumaniusiku huo huo kipenzi mke wake Clara Immerwahr anajiua kwa msongo wa mawazo kutokana na kazi anayoifanya mumewe ya maangamizi jambo lililomuumiza sana moyo Dr Fritz na kumpa upweke.

Vita inaisha huku Ujerumani ikishindwa vibaya na haishii hapo anaanza kuishi kwa hofu ya kushitakiwa kama muhalifu wa kivita kutokana na uhusika wake katika utengenezaji wa siraha za sumu kutoka katika mataifa washindi.

Anajaribu tena kuonesha uzalendo kwa taifa lake hasa kuisaidia serikali mpya Weimar Republic kuinua uchumi kwa kuvumbua namna ya kuchukua dhahabu iliyo baharini ili kusaidia Ujerumani kutoka katika ukata wa kiuchumi uvumbuzi ambao ulikwama.

ANGUKO LINAANZA KUCHIPUZA
View attachment 959695

(Kuibuka kwa sera za kifashisti nchni ujerumani chini ya cha Nazi kilichoongozwa na mawazo ya veteran wa vita ya kwanza ya dunia Adolph Hitler)

Mwaka 1930s hali ya ubaguzi na sera za kifashisti unazidi shamiri kiasi kwamba madai ya uzalendo wa Fritz yanatupiwa mbali. Siku moja binti yake wakati anaenda katika tasisi aliyoifanyia kazi Dr Fritz anakutana na bango linalosema “Dr Hebz Myahudi hatakiwa hapa” inamuumiza sana Fritz anaamua kujiuzulu kama mkemia. Kama ilivyokuwa kwa wayahudi wenye nyadhifa za juu wakati huo akiwemo Albert Einstein wanaondoshwa kwa kufukuzwa au kukimbia wenyewe nchini ujerumani.

Baadae alienda kuishi Ufaransa na akahamia Uhispania na kuenda kuishi pia Switzerland wakati huo afya yake ikiwa mbaya sana.

Licha ya mazuri aliyotenda hawali hayakuweza kufutika alialikwa chuo cha Cambridge na kwa mara ya kwanza akakutana na wanasayansi ambao walikuwa ni maadui katika vita ya kwanza ya dunia wapo waliomsamehe na ndio waliomsaidia kuweza kuondoka ujerumani hasa majira ya joto la ubaguzi anti semitic na wapo waliokataa hata kupeana mikono nae katika mualiko wake nchini uingereza.

Na hata halipopata kazi nchini uingereza hakupata nafasi ya kuishi alielekezwa akaishi eneo la Israel mashariki ya kati wakati huo likiwa bado koloni la muingereza akuweza kufika akiwa njiani akafariki.

BAADA YA KIFO CHAKE

Kama mwanasayansi alieponzwa na dhana ya uzalendo pasipo kuzingatia misingi ya utu na upendo kwa wanadamu wengine pasipo mipaka ya utaifa na jamii.

Hali ya nchini ujerumani licha ya kuondoka na familia yake wapo jamaa zake waliobakia, ijapokuwa alijitahidi sana kuwaokoa mikononi mwa sera za kifashisti kutokana na nafasi yake ya umaarufu na kulitumikia taifa la ujerumani. Ndugu zake wakaribu hasa dada zake walikuwa ni moja wa watu waliouwawa katika vyumba vya sumu ambayo ni gesi aliyoibuni yeye mwenyewe, katika mauaji yaliyojulikana kama “Holocaust” ambapo inakadiliwa wayahudi ambao ni watu wa jamii ya kwake zaidi ya milioni 6.

Baadae mzaliwa wa kwanza wake aalichukua maamuzi ya kujiua 1946 na baadae binti wake wa mwisho aliamua kujiua mwaka 1949 baada ya kuambiwa utafiti wake wa dawa ya kusaidia mtu aliyepatwa na madhara ya sumu Chlorine gas (Sumu aliyeibuni baba yake) kuachwa na serikali ya Marekani.

NINI TUNAJIFUNZA WATU WA KIZAZI HIKI KANUNI MUHIMU ZINAZOFANYA KAZI.

View attachment 959697
(Kundi la watu waliotengwa kwa ajili ya kwenda kuuliwa kwenye vyumba vya Gesi za sumu gereza la Auschwitz)

  • Zipo kanuni za kimaisha ambayo mojawapo ni hii nimekuandikia “Ukianza vyema na kumaliza vibaya hata ule wema wa kwanza hautakumbukwa” na kuhidhibitisha hasa zinazofanya kazi katika maisha yetu ya kila siku kwa kujua au kutokujua na tunapokiuka huwa na madhara pia kama jinsi madhara yanavyokuwa tunapoenda kinyume na kanuni ya matumizi ya vitu mbalimbali vya kieletroniki

Fritz anakumbukwa zaidi katika kubuni gesi za kemikali za maangamizi na vilipuzi katika vita ya kwanza ya dunia kuliko uvumbuzi wa aina bora za mbolea katika kilimo iliyosaidia maelfu ya binadamu dhidi ya mabaa ya njaa na pia dawa za kuulia wadudu mashambani, lakini kinachokumbukwa zaidi ni mauaji ya kemikali katika vita ya kwanza na yale ya watu wa jamii yake zaidi ya milioni 6 (Holocaust).

(mfano injini zozote hutumia mafuta lakini kila moja ina kanuni za matumizi yake ili ifanye kazi ikiwemo na aina ya mafuta yake, ukiweka mafuta ya dieseli katika injini ya petrol basi utaiua injini hiyo )

    • Kusamehe na kuishi kwa kujali na kuzingatia utu sababu hujui nani hatakusaidia kesho. Unayemuona kamaadui yako leo ndio msaada wako kesho na rafiki yako leo anaweza kuwa adui wako kesho,

Mfano wale Dr Fritz alioona kama maadui zake na kubuni mbinu za kuwaangamiza ndio waliomuokoa mikononi mwa Adolf Hitler sababu Hitler angemuua tu na wale aliowaona rafiki na nduguze ndio waligeuka na kutaka kumuua na pia piakuua ndugu zake wa karibu pamoja na watu wa jamii yake zaidi yamilioni 6 (Wayahudi).

( Hii tutajifunza tena kuna mada naiandaa katika eneo hili).

    • Ukipanda wema utavuna mema na pia ubaya utavuna ubaya “apandacho mtu ndio atakachokivuna”. Usijidanganye kijana, binti baba au mama au hata mzee leo haya mabaya unayowafanyia watu na kuwaumiza huwa yanarudi (fitina ikimaliza kazi au ubaya sharti urudi kule ulipozaliwa au kutokea) kwa namna tofauti na hata utakapofariki yataendelea kula vizazi vyako katika saikolojia tunaita sababu za kurithi in heretic factor na katika imani inaitwa Laana au Curse.

Hii tunaona pia katika visa vya kujiua katika watoto wa Fitz ambao wengi wanaonesha kuelemewa na hatia ya aliyoyafanya baba yao na pia ndugu zake wa karibu waliouliwa na hiyo hiyo gesi aliobuni.

HITIMISHO

Yapo mengi ya kujifunza hasa katika udhibitishaji wa kanuni ya unapoacha mema na ukaanza kutenda mabaya wema wako unasahaurika na heri mwanzo mbaya na mwisho mzuri kuliko mwanzo mzuri na mwisho mbaya. Hizi ndio kanuni ya kimaisha na inafanya kazi ulimwenguni kote.

Jifunze Jirekebishe na badili mfumo wa maisha yako asante.

KUHUSU MWANDISHI,
Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Pia ni Msomaji wa Vitabu vinavyohusu Falsafa, Nyurolojia, Historia, Maandiko pamoja na Vitabu vinavyooelezea maisha ya watu mashuhuri (Biography book).
 
niombe radhi tu ktk matatizo ya uandishi ntarekebisha hapo.....asante
Si mbaya. Sasa jifunze na lugha maana kuna maneno ya kiswahili yanakushinda.wenzangu wameelezea tayari sina haja kurudia. Unapoandika bandiko hata kama ni zuri unapokosea lugha linatu kwaza sisi wengine. Lina "bore" so pata muda pia ujifunze lugha ya kiswahili.
 
Mimi kutokana na kusoma kwangu hizi nakala nimejaribu kuishi maisha fulani katika jamii ambapo nimejaribu kuweka watu wanaonizunguka katika jamii kujiona sisi sote ni bora na hakuna bora zaidi ya mwingine.
Ni wachache sana wamenielewa na katika wachache hao ni mmoja tu alifaulu vizuri. Anaitwa Juma, Juma alinielewa kwa kuniambia aliwahi kuambiwa na babu yake, "Ukienda kwenye jamii ngeni weka sana ukaribu na mtu anayechukiwa na jamii hiyo utajifunza mengi sana kupitia yeye".
asante karibu sana......naomba radhi ktk matatizo ya kiuandishi
 
Shukrani sana, tena sana kwa elimu unayotupatia.. ubarikiwe sana.. maana umenibadilisha sana mtazamo wangu kuhusu binadamu wenzangu.. Naomba uwe unanitag kila uletapo somo jipya. asante.
 
Wakosoaji hamkosekani mbona hyo ni minor issue
Si mbaya. Sasa jifunze na lugha maana kuna maneno ya kiswahili yanakushinda.wenzangu wameelezea tayari sina haja kurudia. Unapoandika bandiko hata kama ni zuri unapokosea lugha linatu kwaza sisi wengine. Lina "bore" so pata muda pia ujifunze lugha ya kiswahili.
 
Similar Discussions

27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom