Saikolojia: Matatizo ya utu(Personality disorders)

Kuna kipengele hapo maelezo yake yanamuhusu huyu rais wetu namba moja,huyu wanayesema Ni muhutu. Huyu kichwa upanga. Sasa tutawezaje kumpa dawa Na nani atamueleza tatizo lake.

nani atamfunga paka kengele???
 
Paranoid Personality Disorder anayo Mange.
maana kila linalofanyika anahisi kuna mtu ana plot against her
 
Mimi nina tabia za kupenda kukaa mwenyew tu sehem mfno chumban shulen cpend kuongea na watu Sana hata akija mtu nahic ananisturb nikickia saut sauti nahic zinanikera nakuwa nataman niende sehem ambazo watu hawanijui nianze maisha mwenyew nataman niende km beach nikae tu then niondoke hotel niwe tu mwenyew cpendi kumwambia yeyote shida yngu nataman kwenda sehem km kusafir na nikifka huko nataman kurudi najiona nipo mwneyew tu kwnye maisha hata ndugu wa damu siwambii chochote kuhusu mm siamin mtu yeyote km atatokea anijali Mimi kila cku nawaza tu negative thoughts na hii imetokana na experience ya maisha yngu nimelost both parents in a short period nashkur nilipata kila nilichoomba kutoka kwao japo tuliishi mbali mbali kwa sasa naiona dunia imeturn kinyume na ninavyotaka experience nyengne watu walionilea wamenifanyia mengiii ya kuniumiza nimebak mtu wa kuhandle mwenyew tu kila kitu nawaza tu negative always nashindwa kufocus kwneye mambo yngu masomo Sina interest na vitu nahic hopeless sad anxiety depression NILKUA NAULIZA MIMI NINA TATIZO GANI HASA AU HII NI HALI YA KAWAIDA
Sijajua kwa uhakika ila kwa maelezo yako ni dalili za depression. Njia nzuri ya kukabiliana na haya matatizo ni kuyaelewa vizuri, jaribu kusoma na kuelewa kuhusu depression. Pia kuna kitu tunaita rumination, mtu anakuwa anakazia mabaya tu akifikiria historia yake, hilo linamfanya aone hata yanayokuja yatakuwa mabaya tu, hii inaweza pelekea kujiua. Jitahidi kuwa positive, kumbuka mazuri uliyotendewa hata na hao ndugu waliokuumiza, kumbuka good moments kwenye maisha yako, tembelea watu hata kama hupendi maana ni dawa hiyo, Dawa huwa hatupendi ila hunywa. Ikiwezekana muone hata counselor shuleni kwenu, matatizo ya kisaikolojia yakianza kuathiri kazi, masomo au maisha huwa yanakuwa yamefika level ya kuhitaji matibabu.
 
Tatizo kubwa la watu wenye Personality disorders ni kuwa huwa hawakubali kuwa wana tatizo
Hii hufanya iwe kazi sana kuwatafutia matibabu.
Mkuu nin rafiki yangu ana tatizo la kuamini uchawi kupita kiasi yani yeye amepanga nyumba zaidi ya tano ndani ya mwaka mmoja. Kote anakohama anakubali kuacha kodi kwenda kuhamia sehemu nyingine anasema hizo nyumba anarogwa.

Mara ya kwanza tulimchukulia kawaida lakini hali imezidi kuwa mbaya mpaka ofisini amefikia hatua haelewani na wafanyakazi wengine anasema ni wachawi.

Yani nikikaa naye ni stori za yeye kurogwa, akiumwa, akiumia, akipoteza fedha yeye ni kurogwa.

Amepoteza fedha nyingi, ameshindwa kudumu hadi kwenye mahusiano kwa tatizo hili.

Je hili nalo ni tatizo la kisaikoloji? Kama ndio je ninaweza kumsaidiaje?
 
Mkuu nin rafiki yangu ana tatizo la kuamini uchawi kupita kiasi yani yeye amepanga nyumba zaidi ya tano ndani ya mwaka mmoja. Kote anakohama anakubali kuacha kodi kwenda kuhamia sehemu nyingine anasema hizo nyumba anarogwa.

Mara ya kwanza tulimchukulia kawaida lakini hali imezidi kuwa mbaya mpaka ofisini amefikia hatua haelewani na wafanyakazi wengine anasema ni wachawi.

Yani nikikaa naye ni stori za yeye kurogwa, akiumwa, akiumia, akipoteza fedha yeye ni kurogwa.

Amepoteza fedha nyingi, ameshindwa kudumu hadi kwenye mahusiano kwa tatizo hili.

Je hili nalo ni tatizo la kisaikoloji? Kama ndio je ninaweza kumsaidiaje?
Kun kitu tunaita delusion. Hii ni kuamini vitu ambavyo ushahidi unaonyesha dhahiri kuwa havipo. Hii ni moja ya dalili ya ugonjwa wa akili(Schizophrenia). Mara nyingi imani za kidini na kiuchawi huwa haziwekwi kama zinatokana na kichaa ila zikizidi kama za huyo jamaa yako au mtu akianza kusema anaongea na Mungu huchukuliwa kama ni dalili za ugonjwa wa akili.
 
Kun kitu tunaita delusion. Hii ni kuamini vitu ambavyo ushahidi unaonyesha dhahiri kuwa havipo. Hii ni moja ya dalili ya ugonjwa wa akili(Schizophrenia). Mara nyingi imani za kidini na kiuchawi huwa haziwekwi kama zinatokana na kichaa ila zikizidi kama za huyo jamaa yako au mtu akianza kusema anaongea na Mungu huchukuliwa kama ni dalili za ugonjwa wa akili.
Tiba?
 
I see! Lakini tatizo zaidi, huyo Mheshimiwa ninayehisi ana hilo tatizo is extremely difficult to deal with!!

Hamuamini yeyote na kila mtu kwake ni mbaya/mchawi to the point hata kumsaidia ni ngumu kupita maelezo! Mi mwenyewe hataki hata kuniona kudadaki unless kichwa kiwe kimetulia kweli kweli!!
Poleeee weeeh
 
Uzi huu tutazungumzia matatizo ya utu au matatizo ya kimtazamo. Matatizo haya huhusisha zaidi jinsi mtu anavyoshirikiana na wengine. Tutayazungumzia yote polepole. Tuanze!.
Paranoid personality disorder

Hili ni tatizo la kisaikolojia ambapo mtu anakuwa haamini watu wengine bila sababu za msingi. Muda wote anahisi watu wengine wanampangia njama au wanataka kumdhuru.

Watu hawa wanahisi mambo hufanywa kwaajili yao. Basi likichelewa wanaweza wakahisi limechelewa makusudi ili kuwachelewesha. Hawa ndiyo wale kwenye mahusiano unakuta wana wivu wa kupindukia kwasababu kila kitu wanakitafsiri ni njama. Huwa hawadumu kwenye mahusiano yoyote na hata kazi maana huwa wabishi walalamishi, Huweka vinyongo, Hulipa visasi na wasusaji

Watu hawa huwa hawapendi kukosolewa wala kuingiliwa kwenye maamuzi yao au mambo yao.

Sababu kubwa ya Tatizo hili ni kurithi. watu wengi wenye shida hii unakuta wana ndugu mwenye ugonjwa wa kuchanganyikiwa/schizophrenia na ndiyo sababu dalili zake hufanana sana.

Matibabu ya shida hii huwa ni kumuona mwanasaikolojia ambaye hutumia Mbinu za kicognitive(kubadili namna unavyofikiri) na mbinu za kunadilisha tabia ili kutibu.

Schizoid Personality Disorder

Watu wenye tatizo hili hupendelea kuwa peke yao peke yao. Hawapendi kuchangamana na wengine. Kazini, Shuleni huwa kivyaovyao. Watu wa hivi huwa hawaonyeshi emotions zozote hata wakikosolewa au kusifiwa. Huonekana wana kiburi au majivuno. Hawa watu huwa hawafurahii uhusiano wowote na wengine na mara nyingi huwa hawana wapenzi. Wasipokuwa na wapenzi hawaoni kuwa wamepungukiwa kitu. Huwa hawana marafiki na hupenda kufanya kazi zao peke yao.

Shida hii husababishwa na sababu za kibiolojia ambazo hurithiwa, pia ilionekana kuwa watoto ambao hawajaliwi/waliotelekezwa na wazazi wao au watoto wenye aibu kupita kiasi hupatwa na tatizo hili ukubwani. Matibabu ya shida hii hutolewa na wanasaikolojia ambapo mtu huelezwa umuhimu wa mahusiano ya kijamii na pia hufumdishwa social skills..

Schizotypal Personality disorder

Tatizo hili hufanana sana na Schizoid hapo juu ambapo mtu hupendelea kukaa peke yake na hapendelei mahusiano. Ila hapa mtu huyo anaweza kuwa na mawazo au imani ya ajabu au akaanza kufanya vitu vinavyoonekana vya ajabu kwenye jamii. Pia hawa jamaa huwa ni watu wa kutilia mashaka vitu na watu bila sababu za msingi(kama wale wa paranoid).

Tatizo hili linauhusiano mkubwa sana na ugonjwa wa kichaa(schizophrenia) sema huu unakuwa siyo mkali sana. Tatizo hili ni la kurithi na watu wengi wenye ndugu wenye kichaa huonyesha tatizo hili. Pia mazingira kama vile umasikini au ukatili huweza fanya watu wenye vinasaba(genes) vya ugonjwa huu uwalipuke. Matibabu ya hii shida huhusisha kumuona mwanasaikolojia na kufundishwa social skills.

Antisocial Personality disorder

Hawa watu wenye tatizo la antisocial ni wanoma sana na yafaa kuwaepuka. Hawa ni watu ambao hawajali haki za wengine, Vinga'ng'anizi, Hiwa hawafikirii future, wagomvi, wasiowajibika, wadanganyifu na watu wasiojutia makosa yao.
Hawa jamaa ni wale wanakuwaga matapeli. Huwa wachangamfu sana lakini ni uchangamfu superficial tu.

Watu hawa hukosea na kuumiza wengine mara nyingi na mkikaa vikao watajidai kwamba wanajutia makosa yao lakini ni ulaghai mtupu, huwa hawajuti. Wengi wao hutumia madawa ya kulevya, huwa maskini na hufa vifo vitata.

Borderline personality disorder

watu wenye shida huwa wanashindwa kuwa na uhusiano wa kudumu na watu wengine. Sifa kubwa ya watu wenye shida hii ni kujidhuru. Unakuta wanajikata, wanang'oa nywele zao au kujiua. Watu wa hivi huwa hawajithamini na kujiona wasiofaa kitu. pia watu wa hivi hawatabiriki anaweza kuwa na hasira kali sana lakini baada ya muda akawa mwenye huzuni sana. Pia huwa na tabia za kutojali kama matumizi ya madawa.

Hii shida imeonekana inatokana na kurithi na kutendewa vibaya utotoni. Mara nyingi hali ya watu hawa huboreka wanapokuwa watu wazima. Tiba ya hili tatizo huwa ni ushauri wa kisaikolojia na kudeal na mambo yanayoweza sababisha kujiua.

Histrionic Personality disorder.

Kiujumla hawa ndiyo wale tunaita madrama queen. Watu wa hivi wanapenda kukubalika na watu mda wote. Hata kuvaa utakuta wanavaa ili kuonekana. Watu hawa huwa wanakuza sana mambo kiasi kwamba wanakuwa kama wanaigiza. Mnaweza kuwa mnajuana siku mbili tu lakini anakuwa kama mmejuana mwaka akikukuta full kukuhug. Kitu kidogo atakikuza sana. Mara zote wanapenda kuwa centre ya attention na hawawezi kuwa na raha mpaka wawe centre ya attention. wanajali sana jinsi wanavyoonekana na hutumia pesa nyingi kwenye nguo na mapambo. Wanapenda kusifiwa na humaind wasiposifiwa. Tatizo hili mara nyingi hotokea zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.Watu wa hivi huwa wana pozi za kujitongozesha na huwa na uhusiano na watu wengi ambao haudumu. Mara nyingi huwa na matuamaini makubwa sana na mahusiano yao, ataanza uhusiano leo lakini tayari anapanga ndoa huku akiusifu sana uhusiano huo.
Watu wa hivi mara nyingi hawawezi kufanya kitu kikakamilika au kikafaulu hufanya mambo kwa kukurupuka na hukosa mpangilio. Sababu za ishu hii hufanana na zile za antisocial na mara nyingi watu wenye hili tatizo huwa pia na tatizo la antisocial.

Narcissistic personality disorder

Kuna kijana mmoja wa kigiriki alikuwa anaitwa Narcissus. Inasemekana baada ya kujiangalia kwenye kioo/maji alijipenda kupita kiasi. Basi kuanzia hapo alikuwa anashinda kwenye kioo akijitazama na kujikubali. Basi watu ambao huwa wanajikubali kupita uwezo wao halisi husemwa wana narcissism.

Watu wa hivi hujiona wao ni special na wanahiraji special treatment. Watu wa hivi tunaweza sema huwa na kimbelembele. Atataka siti ya mbele, kuwa wa kwanza nk. Akikutana na mtu anayemzidi uwezo hununa, wivu na kujikweza.

Watu wa hivi huwa wanamatatizo sana kazini na shuleni. Kuna watu kazini ukifika kwa mara ya kwanza utawaona yes huyu ndiyo rafiki lakini baadaye ukagundua ni mtu wa kujikweza tu na mwenye wivu!?
Tatizo hili husababishwa na malezi mabaya. Wazazi wakishindwa kuwafundisha watoto kubalance na kujua uwezo wao. Kuwaacha watoto wajione wao ni special na wanauwezo kupita uhalisia huleta hili tatizo.

Avoidant personality disorder.

Watu wenye hii shida huwa wako sensitive sana na jinsi wengine wanavyowaongelea hivyo wanachofanya ni kutokuwa na mahusiano na wengine(avoidant).
Watu hawa huwa wanajidharau sana hivyo huona wengine pia watawadharau na kuwapuuza. Watu wa hivi huwa na marafiki wachache na urafiki wenyewe wa mbalimbali. Watu wa hivi huepuka mahusiano, mikusanyiko kama sherehe nk. Shida hii inaonekana hutokana na sababu za kurithi na huongezewa na kutokea kwa sababu za kimazingira hasa malezi. Watu wengi wenye hili tatizo huwa na malezi ambayo walikuwa wamedharauliwa na kuwacriticized kupita kiasi. Hii imewafanya wajione hawafai kitu.

Dependent personality disorder

Kama jina lilivyo watu hawa huwa wategemezi. Ni watu ambao huwategemea wengine kuwafanyia maamuzi hata yale maamuzi muhimu maishani. Watu wa hivi huwa wanaogopa sana kuvunja mahusiano na wale wanaowategemea. Utakuta mtu yupo kwenye ndoa au uhusiano wa mateso lakini hataki kutoka au anatoka na kurudi.

Watu wa hivi unakuta hata kwenye urafiki au mahusiano ni watu wa kuburuzwa. Atakubaliana na wewe hata kama anaona si sawa.

Tabu hii hutokana na malezi. Kitendo cha wazazi kuwafanya watoto kuwa tegemezi kupita kiasi hufanya wawe na hili tatizo ukubwani.





itaendelea..
Nashangaa uzi wenye mambo...muhimu kama haya, unakuwaje na wachangiaji wachache hv? Hapa ndio utagundua kundi kubwa lililopo Jamii Forum ni watu wa aina gani, any ways...mtoa mada umenifunza mengi sana...natamani kujua zaidi. Mfano kipengele cha ant-social personality diosioder, mama mwenye nyumba wangu ana hizo tabia 100%. Mungu akubariki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kun kitu tunaita delusion. Hii ni kuamini vitu ambavyo ushahidi unaonyesha dhahiri kuwa havipo. Hii ni moja ya dalili ya ugonjwa wa akili(Schizophrenia). Mara nyingi imani za kidini na kiuchawi huwa haziwekwi kama zinatokana na kichaa ila zikizidi kama za huyo jamaa yako au mtu akianza kusema anaongea na Mungu huchukuliwa kama ni dalili za ugonjwa wa akili.
unanikumbusha kaka yangu alikuwa mlokole kupitiliza unaweza kutembea nae akawa anakamata fly's kama nzi, mbu, vipepeo n.k anadai eti ni mapepo yametumwa kwake kuharibu huduma nikaona huyu ni kichaa mtarajiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom