Saikolojia: Jifunze mambo yatakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (Case study Finland)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
SEHEMU YA KWANZA

Saikolojia: Jifunze mambo yakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha duniani ( na fahamu vigezo vilivyotumiwa kuichagua Finland kuwa nchi ya kwanza (Juu) kwa watu wenye furaha na Tanzania ya tatu (kutoka mwisho).

“..Katika makala hii nimejikita kuchambua vigezo vilivyoifanya Finland kuwa nchi ya watu wenye furaha kama Case study na kisha kuangazia sababu..” Education Mentor
upload_2018-4-6_20-57-45.png

1. MWANZO
Wanavyoeleza wanafalsafa na wasaikolojia kuhusu dhana ya kuwa na Furaha ni nini?


Dhana ya tafsiri kuhusu nini maana ya furaha imejadiliwa sana Duniani kuanzia katika mataifa mbalimbali ulimwenguni kwa watu wa dini, wanafalsafa na mwishoni mwa karne ya 20 ikachipukizia kwa wanasaikolojia mfano William James (1842-1910) “Functionalism school of thought” na Abraham Maslow (1908-1970) wa “Humanistic School of thought”.

i. Falsafa

Katika Falsafa (Philosophy) tafsiri ya msamiati furaha ni kuishi maisha mazuri au yenye ustawi mzuri ambapo kwa wagiriki utumia msamiati “eudaimonia” ambapo wanasisitiza furaha ni kuwa na maisha mazuri na maisha mazuri ni maisha yenye maadili mema.

Hivyo kwa maelezo mafupi, Plato Socrates na Aristotle wanaweka hitimisho katika suala la kuwa na maisha mazuri(Furaha) na yenye ustawi ni nini? Ni pale mtu, watu au jamii inapotaafuta kuenenda au kuishi maisha ya maadili/maadili mema ndipo kuna kustawi na kuwa na furaha kunapotokea ndani yao.

ii. Saikolojia

Katika Saikolojia (Postive Psychology) Furaha tafsiri yake ni kuwa na hali njema na ustawi katika akili na kihisia ambao wanaokuzunguka kukutafsiri mtu chanya au mwenye furaha.

iii. Tafisri nilizozipata

Kwa kujumuisha falsafa, saikolojia na maandiko vitabu vya Mungu ili huwe na furaha ya kweli na kudumu inaanzia na wewe kwanza kubadilisha mfumo wa maisha yako kabla ya kumbadilisha mtu mwingine au mazingira yako ya nje.

iv. Baadhi ya Vigezo vilivyotumiwa katika kuchagua nchi yenye furaha duniani kwa mujibu wa ripoti

a) Upatikanaji wa msaada kwa mtu kutoka katika jamii inayokuzunguka hasa wakati wa uhitaji.

b) Kutokuwepo kwa vitendo vya rushwa

c) Hali ya uhuru katika Jamii

d) Matendo ya ukarimu na msaada kwa wahitaji

2. FINLAND TAIFA LINALOONGOZA KWA KUWA NA FURAHA ULIMWENGUNI. (CASE STUDY)

i. Ifahamu Finland kwa ufupi ilipotokea karne ya 20.

Finland mwaka 1993 tafiti zinasema iikuwa taifa lenye visa vingi vya ulevi kupindukia na watu kujiua na hali ya uchumi mbovu ulioharibika hii baada ya uhuru wake baada ya kuvunjika kwa Soviet Union (USSR).

upload_2018-4-6_20-59-56.png

(Baadhi ya picha za matukio katika vita ya kati ya Finland na Soviet Union “Winter War”)

Ikumbuke mwaka 1939 taifa la Finland lilikuwa katika vita na Soviet Union (USSR) katika kujitetea na sera ya utanuzi mipaka (expansionism) wa Soviet katika magharibi mwa mipaka mwa nchini Finland.

Finland kwa kuwa kiuchumi na kimabavu hisingeweza kuishinda ili kurudisha mipaka yake iliyoiochukuliwa. Hivyo Finland ikajikuta inaingia katika mapatano na Nazi ujerumani chini ya Adolf Hitler katika kushirikiana kivita (Mutual Alliance) katika vita dhidi ya Soviet Union (USSR) ili kurudisha sehemu ya nchi yake.

Ili iweze rudisha mipaka iliyoipoteza katika vita “winter war” bahati mbaya sana kwa Finland vita ikawa kinyume cha Adolf Hitler na washirika wake hivyo kushindwa kwa Hitler ndio ikawa anguko kamili la Finland yote na uhuru wake katika makucha ya Soviet union (USSR). Hivyo hali zao zilikuwa si nzuri kama hilivyokuwa kwa mataifa yote chini ya umoja wa nchi za kisovieti hadi kusambaratika kwa umoja huo mwanzoni mwa miaka ya 1990.

ii. Finland hilipo sasa.

Mwaka huu 2018 taifa la Finland ndio taifa ambalo limetangazwa kuwa na watu wenye furaha sana kimaisha wakati huo Tanzania ikiwa chini sana ya tatu kutoka mwishoni katika viwango vya mataifa ya watu wasiokuwa na furaha. katika ulimwengu. Kwa kweli baada ya kusoma ripoti hiyo ilinifanya kwanza na mimi niangalie ni vipi taifa hilo limefanikiwa kuwa nafuraha katika ulimwengu. Kama Mwanasaikolojia na mpenzi wa kujifunza na pia kusoma falsafa za maisha nikatamani nifahamu hivyo nikaanza kupekua pekua vitabu vyangu ili iwe rahisi kupembua kwa mapana kuhusu dhana ya furaha na maisha mazuri huku nikijifunza kupitia Finland.

iii. Baadhi ya sababu zilizoifanya Finland kuwa taifa la watu wenye furaha kwa mujibu wa tafiti.
upload_2018-4-6_21-1-54.png

(kwa tafiti zilizotolewa na IMF 2017 Finland haipo katika 30 bora ya nchi Tajiri wala 30 zenye uchumi mkubwa duniani. Ni nchi yenye wakazi wengi wa kipato cha kati au wastani)

a) Viwango vidogo vya rushwa katika serikali yao (Rushwa inapokuwa viwango vya chini Haki inatawala).

b) Uwepo wa bendi nyingi za muziki (Heavy Metal Bands)

c) Mfumo bora wa elimu hasa kwa masomo ya sayansi kusoma na mathematics

d) Taifa linaloongoza kwa kunywa kahawa ulimwenguni hivyo kipindi cha winter huwa hawasumbuliwi na baridi

e) Ni taifa lenye utulivu ikiwemo viwango vya chini vya uharifu, rushwa na hakuna eneo ambalo haritawaliki au kushindwa fikiwa na serikali katika huduma muhimu za kijamii.

f) Uwepo wa tamaduni ya Sauna kwa taifa lote (Sauna ni aina ya vyumba vya mvuke wa moto viavyotumiwa kuliwadha wakati wa baridi).

g) Taifa lenye viwango vya chini vya vifo vinavyotokana na uzazi na yanayohusu wamama wajawazito hivyo ndio taifa zuri kwa mtu kuwa mama na kuwa na familia.

h) Ni moja ya Taifa linaloongoza kwa unywaji wa maziwa ijapokuwa pia ni taifa la kumi na moja duniani “kugida bia”.

i) Mji wake mkuu Helsinki ni kati ya miji mikuu inayoongoza na kuwa na watu waaminifu utafiti uliofanywa katika mitaa ya miji hiyo kwa wakati tofauti tofauti ziliangushwa wallet 12 lakini 11 zilirudishwa kwa wenyewe na nyingine haikurudi.

j) Ni moja ya taifa linaloongoza katika uazimishaji na usomaji wa vitabu. Wastani wa vitabu 100 kwa kila mwaka kwa kila familia ya nchi hiyo.

“Furaha inaanzia ndani ya fikra kabla ya kuathiriwa hasi au chanya na mazingira unayokabiliana nayo

Je unajua? nchi zenye vita Libya (70/156) na Iraq (117/156) zimeipiku Tanzania (153/156) kwa kuwa na watu wenye furaha duniani. “

3. BAADHI YA MAKOSA TUNAYOYAFANYA KATIKA KUTAFUTA FURAHA

i. Mtu mwingine kukupa furaha.
upload_2018-4-6_21-3-0.png

(Mahusiano yoyote (Urafiki,Ndugu, familia na kazini) ni kama akaunti ya uwekezaji usitarajie kupata furaha kwa mtu kama wewe haujawekeza hisa ya furaha katika akaunti ya mahusiano “reciplocity”)

Sehemu tunayofanya makosa katika jamii zetu watanzania wengi sana ni kuamini katika watu wengine kuwa sababu ya furaha kwetu

Wengi wwaliovunjika moyo na kukata tamaa katika mahusiano walitarajia ndoa kuwa sababu ya kufurahi kwao

Mfano Viongozi, Ndoa na Marafiki nk ukweli ni kwamba furaha ni kitu ndani ya nafsi yako kama unategemea sana watu wakupe furaha katika maisha yako. Pasipo wewe mwenyewe kuwa sababu ya furaha hiyo ni kama unapoteza wakati wako au tarajia kuvunjika moyo au matarajio yako “Disappointed” pia fahamu na ujifunze kumuwekea tumaini kiongozi yoyote au mwanadamu mwenzako sana hupo njiani kuishi bila furaha na kukosa utulivu ndani yako.

Formula ni hivi hisia chanya au hasi zinatabia kuambukiza au kuambukizwa kustawi au kusinyaa kutokana na watu unaochangamana nao “interacting”

“..Msimwekee kiongozi tumaini...” <Mika7:5>

ii. Kutarajia Vitu (material things) vitakupa furaha.
upload_2018-4-6_21-3-46.png

(Nchini China mwaka 2012 kijana wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Wang haliuza figo ili apate fedha kununulia i phone na i pad)

Jifunze kitu kwa mara ya kwanza ulipopata simu, gari, nyumba au kitu chochote cha ndoto yako hali uliyokuwa nayo (mimi binafsi siku ya kwanza nilikosa usingizi kabisa) halafu tafakari leo hapo hulipo. Jiulize kiwango cha furaha yako kipo sawa sawa na siku za hapo mwanzoni hulipokipata? au siku ulipompata huyo Mr/Mrs right wako? .

Ukishapata jibu sahihi basi fahamu wanadamu tunakitu ku “cope” na hali. hii ndio inatufanya kila leo kuwa katika safari ndefu ya kutafuta furaha katika vitu (Material things) na kamwe tunakuwa hatuliziki na wenye mashindano sana yasiyo na tija yoyote na mara nyingi yametuacha kuwa na majuto ya muda mrefu sana au kushindwa tafsiri furaha hipo katika vitu hitaji? au tumizi?.

iii. Kutafuta kukubalika au kupendwa na kila mtu.
upload_2018-4-6_21-4-17.png

(Msichana Sahar Tabar(Kulia) alifanya Cosmetic Plastic surgery ili awe na muonekano wa Angelina Jolie pengine ndiyo furaha yake ilipokuwa? Furaha yako hipo wapi?)

Kwa mujibu wa tafiti sehemu mojawapo inawafanya watu kutokuwa na furaha ni kutokana kutokubaliana na mwonekano wao kisura na kimaumbile hadi jinsia (Transgender na transsexual) zao hivyo imewafanya wengi kujaribu kujibadili ili kuboresha namna ya muonekano wao hata kwa kutumia vipodozi vyenye kemikali zenye nguvu.

lakini pia tafiti zinasema wengi huishia katika kujiua wanapogundua wameharibu zaidi au wamepotea katika hayo mengi waliyofikiria hapo awali kabla ya kufanyiwa operation au kubadili jinsia zao.

Sababu moja iliyo kuu ni kujaribu au kutafuta kukubalika, kupendwa na kila mtu au kutaka sifa kutoka katika kila mtu kwenye jamii yako ni mtego sana. Kifupi huwezi kupendwa na kila mtu katika jamii yako inayokuzunguka hata kama ungefanya vipi lakini kulinda afya ya akili yako tafuta kufanya mema na yenye maadili na maamuzi mazuri ili kusudi kama wapo watu wakina “melancholic” wasipate sababu ya kukuchafua ili wapate wakuwasapoti katika chuki zao juu yako

Furaha ni sababu zinazotokana na ndani ya mtu kwanza kabla ya za nje kufanya kazi.

iv. Matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya kukupa furaha.
upload_2018-4-6_21-4-41.png

(Vijana wengi huingia katika matumizi ya madawa ya kulevya katika kutafuta furaha na kujiliwaza).

Ningeanza kuelezea “alosto” au “kupata stimu” ni kitu gani kisayansi

Ni pale vilevi au madawa ya kulevya (psychoactive drug) katika utendaji kazi wake kwenye ubongo kwa kuzuia utumikaji kwa kemikali Neurotransmitter ambazo zinaitwa dopamine, norepinephrine na serotonin katika mfumo wa neva katika mwili.

(kutolingana “imbalance” kemikali “dopamine, norepinephrine na serotonin” nisababu ya magonjwa ya akili mengi baadhi yanahusiana na mood ya mtu mfano Bipolar disorder)
upload_2018-4-6_21-5-1.png

(Ugonjwa wa akili Bipolar Disorder unatajwa kuwa sababu ya tabia za Chris Brown ikiwemo kupigana na kupiga watu Baba yake wakambo ni moja waliowahi kupigwa naye )

Hivyo zuio hilo la matumizi ya kemikali hizo zinafanya kuwepo kwa wingi wa neurotransmitter hizo katika Ubongo hivyo kuathiri mfumo mzima wa utendaji wa kazi (sympathetic division, autonomic nervous system).

Madhara yanatokea ikiwemo uongezekaji wa mapigo ya moyo na upumuaji mboni kuwa pana na kuongezeka sukari katika damu ikiambatana kukosa appetite.

Hivyo utumizi huo baada ya muda unasababisha hali tegemezi kisaikolojia (Psychological) na kimaumbile (Physiological) na kusababisha madhara katika akili na utendaji wa mwili kikawaida hasa alosto inapoondoka muda baada ya kujidunga au kutumia kilevi au madawa hayo.

Kifupi kutafuta kuliwazika, furaha au burudiko la namna yoyote kwa njia ya vilevi na madawa ya kulevya ni sawa kutaka maliza kiu cha maji kwa kunywa maji ya bahari inakuwa kwa kadili unavyoongeza kasi uikate kiu ndio unavyokaribia mauti yako.

v. Umaarufu na kuwa na pesa nyingi.

upload_2018-4-6_21-5-49.png

(Kelvin Cubain muigizaji wa filamu za “Home Alone” licha ya kuupata umaarufu ulimwenguni kote na kuwa na pesa nyingi akiwa na umri mdogo, kwa sasa ameangukia na matatizo ya utumiaji wa madawa ya kulevya)

Katika masuala ambayo wanasaikolojia (Marekani na Ulaya) wanaendelea kuyafanyia utafiti ni pale kwanini watu wengi ambao ni maarufu wenye fedha nyingi na ambao tunadhania wanaishi maisha yenye kila kitu (Perfect life) katika jamii zao kuamua kujiua. licha ya kuwa na vitu vingi vya anasa vinavyotamaniwa na kila mtu na fedha nyingi wapo wanaoishia kujiua au kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya au kuugua magonjwa ya akili hasa Msongo “depression”.

Hata hapa nyumbani wengi tumeshuhudia katika kesi mbalimbali za watu maarufu wakiwa na mashtaka ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Katika jarida moja nchini marekani inabainisha kuwa nchi zenye watu wenye kipato cha juu au hadhi flani na sababu kubwa inasemekana wengi wanashindwa kukubaliana na hali zinapobadilika au kushindwa kwa kushuka chini.

Hivyo fahamu umaarufu na pesa (Ukweli tunahitaji pesa sababu ni ulinzi kwetu) lakini kupata vyote hivyo sio sababu ya kuwa na furaha kamili na kujitosheleza katika maisha ni zaidi ya hivyo.

vi. Kuwa matarajio au kunuia matarajio au ndoto kubwa kuliko uhalisia.
upload_2018-4-6_21-6-18.png

(Rudolf Hess baada ya matarajio yake kushindwa akiwa bado mtu wa pili katika Chama cha Nazi chini ya Adolf Hitler tu, mwaka 1941alifanya misheni ya hatari kuruka na ndege binafsi kwenda Uingereza (wakati nchi zikiwa kwenye vita ya pili ya dunia) kwa lengo kutafuta amani na suluhu na Uingereza (Ijapokuwa Hitler baadaye alikaliliwa kuwa hakumtuma na aliagiza auliwe popote atakapopatikana ). Baadae alipatwa na ugonjwa wa akili “paranoia”)

Kweli kuwa na ndoto kubwa katika maisha ni jambo zuri sana na tena ni msingi mzuri katika kutupa matumaini mbalimbali kuhusu kesho yetu. Sababu tumaini ni kuwa kuota ndoto pasipo kuwa usingizini. Hili kutimiza ndoto zetu ni si tumaini tu linahitajika bali Upendo na Imani. Upendo Imani na tumaini kwa pamoja vinapofanya kazi ndani yetu vinatusaidia sana kuwa katika matarajio yenye uhalisia.

Kuna kitabu kimoja niliwahi kukisoma kulikuwa na utafiti uliofanya na chuo kikuu cha Havard nchini marekani katika utafiti huo wanaeleza mara nyingi uchaguzi wetu katika masuala tunayotazamia kutupa furaha katika maisha asilimia kubwa wengi huafanya uchaguzi sio sahihi (kukosea.)

Hivyo sio kwamba hata mimi hayajanikuta hivyo kisehemu hiki nina kiuzoefu. Kwahiyo wakati wote jaribu kupembua matarajio yako kusudi yawe na uhalisia na kipawa uwezo ambao Mwenyezi Mungu amekupatia. Kusudi husije ukapita katika kama hii huwa inasumbua sana. Hali hizi huwakuta wafanyabiashara katika wakati wa kupanga maamuzi, Wanafunzi katika kusubiria Matokeo yawe kidato cha nne au sita, hata wachumba wanapokuwa wanafikiria maisha ya ndoa hapo baadaye.

ITAENDELEA SEHEMU YA PILI NIKIANGAZIA SABABU ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUWA NA FURAHA KWA MUJIBU TAFITI (RESEARCH) , WANASAIKOLOJIA WANAFALSAFA NA MAANDIKO. (USIKOSE SEHEMU YA PILI)

KUHUSU MWANDISHI,

Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).

Pia ni Msomaji wa Mzuri wa vitabu vinavyohusu Falsafa, Nyurolojia, Historia, Maandiko pamoja na Vitabu vinavyooelezea maisha ya watu mashuhuri (Biography book).

Ingia hapa kusoma Sehemu ya pili.

Saikolojia: Jifunze mambo yatakayokusaidia kuwa na maisha yenye furaha (sehemu ya pili)

Makala nyingine alizoandika Education Mentor..

Saikolojia: Fahamu tabia ya hasira, madhara yake na namna za kuishinda

Saikolojia: Sababu zinazosababisha magonjwa ya akili ambazo wengi hawafahamu. (psychological disorder)
 

Attachments

  • 08e31360-2780-11e8-b567-adb1113855b0_1280x720_201142.jpg
    08e31360-2780-11e8-b567-adb1113855b0_1280x720_201142.jpg
    28.5 KB · Views: 276
Napenda mno mada zako kamwe sikujua kuwa Chriss Brown tabia ya kupiga ni ugonjwa kwa mtindo huu basi wanaume wengi wa kiafrica wana bipolar disorder
Karibu sana.......naandaa makala nitafundisha magonjwa hayo common ambayo wengi wanaumwa pasipo kujua na dalili zake
 
Asante kwa makala nzuri. Endelea kutoa elimu hii muhimu kwa taifa.

Hili somo linatuambia kuwa kabla ya kufanya chaguzi za maisha na aina ya watu tunaotaka kuwa, basi twapaswa kujitathmini siye tuko vipi. Ama tunapochagua wa kutuongoza basi pia twapaswa kutambua tabia zao.

Yanayotokea duniani kwa sasa miongoni mwa Viongozi ni mkusanyiko wa sababu nyingi za kisaikolojia hasa wakitafuta furaha ambayo ni ngumu kwao hatimaye wanaishia kuikosa furaha hiyo.
 
Asante kwa makala nzuri. Endelea kutoa elimu hii muhimu kwa taifa.

Hili somo linatuambia kuwa kabla ya kufanya chaguzi za maisha na aina ya watu tunaotaka kuwa, basi twapaswa kujitathmini siye tuko vipi. Ama tunapochagua wa kutuongoza basi pia twapaswa kutambua tabia zao.

Yanayotokea duniani kwa sasa miongoni mwa Viongozi ni mkusanyiko wa sababu nyingi za kisaikolojia hasa wakitafuta furaha ambayo ni ngumu kwao hatimaye wanaishia kuikosa furaha hiyo.
ahsante....Ni kweli mkuu
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom