Saikolojia: Hisia, akili na Sheria ya Mvuto (Kupenda, kupendwa, kupendana)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
upload_2018-5-28_23-47-49.png

Kweli hipo sheria flani katika ulimwengu ambayo inafanya kazi katika upendo wa mahusiano kwa njia ya hisia na akili.

NB: Sheria ya mvuto ujulikana pia kama "Law of attraction"

Namna inavyofanya kazi ni kwa namna nyingi sana mojawapo tunaita soul ties yaani muunganiko wa kiroho au nafsi mfano Kuna muda unaweza ukawa unamuwaza mtu au unamfikiria halafu akakupigia simu au akapita sehemu hiyo au akagonga mlango wako nyumbani kwa wakati huo huo na unajikuta yaani unamwambia “yaani nilikuwa nakufikiria wewe sasa hivi kweli una maisha marefu!”

Sasa hipo nguvu inayofanya kazi kubwa kama hiyo hiyo katika uchaguzi wetu wa wenza wa maisha.

Lakini bahati mbaya hatuitambui au tunaipuuzia tu sababu inahitaji nidhamu kuu sana ni Mungu muumba mbingu na nchi mwenye ndiye aliyeitengeneza na inafanya kazi kwa kila Binadamu pasipo mipaka na jinsia rangi au dini zetu wapo wengine wameibatiza “machale yakanicheza”.

Usia wangu vijana wenzangu wasaka wenza ndani ya jamii forum hisia zisiwe na nguvu sana kuathiri maamuzi, ruhusu kipengele muhimu cha akili kifanye kazi pia.

formula ilivyo ukitulia utapata aliyetulia mwenzako kifupi ndege wanaofanana wanaruka pamoja labda wasipende tu hao ndege wenyewe.

Unaweza nikatalia hilo nina mifano mingi sana kuhusiana na hilo.

Hamna mtu asiyependa vitu vyema ndio maana waleta thread wengi katika sifa zao za kusaka wenza wa maisha watataka mwanamke au mwanaume mcha Mungu hiki kitakuwa kipengele cha msingi sana hata kama mwenye kutafuta mwenza sifa hizo hana.

NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA

Ni sawa na stori niliyowahi pewa na brother mmoja akinipa mausia kuhusu maisha hasa kwenye nyumba za ibada. Kuna jambazi alianza kwenda akisaka mke mwema huko kwahiyo akawa anapigia hesabu sana warembo walio humo kweli akampata mmoja haraka haraka wakafunga ndoa. Baadae ndio anapata mkanda kamili huyo mrembo aliyempata alikuwa anajiuza katika kumbi za usiku baada ya kukinai maisha hayo na yeye akazama ibadani kutafuta mwanaume mchaji hivyo ndivyo walivyokutana na wana watoto tiyari.
upload_2018-5-28_23-48-32.png

(Bwana Bonnie na mkewe cylide waliotingisha katika uharifu wa siraha zama hizo na kuimbwa na Tupac baadae Jayz na Beyonce)

Pia tunajifunza kupita Bonnie and cylide hawa bwana na bibi ambao walikuwa watu hatari sana kifupi walikuwa ni ndege waliofanana nguvu ya mvuto ilichangia wakakutana na kuoana sababu tabia aua character zilifanana hivyo hata mwisho wao walikuwa pamoja wakiwa na matundu zaidi ya 30 ya risasi baada ya kuwasumbua sana FBI.

AKILI ZINAPO POFUSHWA NA HISIA “TUNAINGIA WAZIMA WAZIMA”

Hii pia inanikumbusha dada yetu Neema mwita aliyemwagiwa uji wa moto kifuani na mumewe siku za nyuma alivyoelezea namna watu walivyomuonya juu ya huyo anayeenda kuolewa naye ni mtu wa aina gani. Lakini bahati mbaya hisia zilipozidi zilimpofusha asione kingine na akili haikufanya kazi ingawa tayari kashapewa ulemavu.

Lakini kwanini nguvu ya mvuto kuhusu mwenza haikufanya kazi ndani yake? Sababu hakuruhusu akili ijapokuwa alijua kweli anaingia hatarini lakini hisia zilifunga macho akili akaingia mzima mzima.

Kisa kingine ni cha Uhusiano wa kati ya Bobby Brown na Whitney Houston uliokolea sana mwanzoni mwa miaka ya 1990 Whitney hisia zilimpofusha na yeye akukubali kuona mpaka alipolazimishwa kuona akiwa kashaua kipaji chake na ni teja aliekufa kifo cha kusikitisha sana. Akiwa na bomba la sindano mkononi mwake.
upload_2018-5-28_23-48-56.png

(Boby na Whity kwenye harusi yao)

Whitney hisia zilimzidi nguvu akajikuta kaingia katika ugomvi mzito hata na baba yake mzazi kisa alimkatalia kuolewa na bobby ikafikia Mzee Houston amefariki whitney hakuenda kumzika baba yake na wala hakutaka baba yake ahudhurie harusi yao.

Kifupi hakutaka kumsamehe baba yake kwa kitendo cha kumkataa bobby awe mkwe wake lakini kile alichokiona mzee Houston ndicho miaka ishirini mbele ndicho kilichomuua Whitney na kuna wakati aliwahi sema kabla hajafariki "sitamsamehe kabisa Bobby kayaharibu maisha yangu" .

ANGAZIA HAYA

1. Wengi sana baada ya maafa baada ya kuingia niliokutana nao waliniambia tu nilidhani nitambadilisha, au atabadilika mbele ya safari au nilikuwa mjinga sijui kwanini.

2. Kifupi usifumbie macho yale umeyaona kwa sasa pima kama utaweza stahimili.

3. Miezi mitatu kwenda hadi kutoa posa ni michache sana kumfahamu mtu.

4. Labda vipi una amani naye sasa hivi kuwa naye? na sio “furaha ya shauku” nazungumzia utulivu ndani yako.

5. Hisia ni nzuri lakini jifunze akili iwe kazini katika maamuzi yako.

6. Uvumilivu kipimo muhimu sana katika hatua za awali

7. Umekutana nae humu pitia hata thread na content sababu ulimwengu huu uwakilisha mengi sana halisi kifupi ndipo tunapojifichia humu. hahaaha (Natania)

(Mnisamehe kwa nilichoandika leo pengine naweza kuwa nimewakwaza wengi lakini ndio taaluma yangu kama mwanasaikolojia inanibidi nizungumze ukweli)

Cc: Mdogo wangu Quijote na wengine katika safari ya kutafuta wenza wa maisha.

Asanteni...................................................................
 
Mkuu kuna kitu hapa tuwekane sawa kidogo. Hayo yote katika mahusiano tunaweza kuyabatiza kama ni mvutano wa hisia. Kumbuka pia sumaku huvuna na sumaku nyenzake au chuma, na katika hili haizuiliki maana imeumbwa iwe hivyo.
Sidhani kama wale wanao kuwa wamekumbwa na zahama hizo za kuathiriwa na hisia au mvutano wa hisia kwamba ni lazima akili ndio itangulie kwani tayari pia inakuwa ishaumbwa hivyo.

Binafsi nina hiyo changamoto yla kumfikiria mtu na baada ya muda mcheche sana nikatokewa na kitu au jambo litakalo muhusu mhusika, either kwa kunipigia simu au kumuona sehemu hiyo nilipo.
 
Kwenye mAhusiano hisia ndio kuanza siku zote na wachache sana wana nidhamu ya kuruhusu akili Ifanye kazi pia.

Kumfikiria mtu halafu kutokea ni nguvu hiyo hipo kama rada ndani ya Roho za wanadamu.
 
vipi kuhusu wale wenzi wema ambao baadae hubadilika na kuwa na tabia mbaya ilhali hawakuwa hivyo awali
 
Ni somo ambalo inabidi utulize kichwa sana na uushinikize moyo wako kulielewa. Hii ni tafakuri na hakika ipo chanya kabisa, binaadam mara nyingi sana tunapotea kwa kufuata yale ambayo nafsi zetu zinayataka pasi na kushirikisha akili zetu.

Ni kweli mapenzi huanza kupitia hisia, lakini atakuwa mwenye akili mno yule ambae ataipa nafasi akili (tafakuri) yake ili imuongoze. Tunatofautiana na aina nyengine za wanyama kwa kuwa sisi tumejaaliwa tafakuri, na pale tu tutakapoacha kutumia akili katika mambo yetu na kufuata nafsi/mioyo yetu basi hatutakuwa na tofauti kubwa sana na wanyama wengine.

Kwa mfano:- Nafsi/Moyo unakusukuma katika matumizi ya pombe, akili yako inakwambia kabisa kwamba matumizi ya pombe si mazuri kwa mustakabali wako (kijamii na kiuchumi) lakini kwa kuwa umeamua kuufuata moyo/nafsi yako na kuipuuza akili yako mwishowe unaharibikiwa.

Ni heri ukatumia akili yako ili ubaki kama binaadam au kuisaliti akili hiyo na ukafanana na mnyama!
 
asante mkuu kwa kuongeza kitu
 
Mie Kuna mtu hunifatilia hachoki kah sasa kawa rafiki yangu mda mrefu when he kissed me and hugged me for the first time I felt like kama kamifyonza my energy yangu nakuniingizia kitu, sijawahi ku feel hivo before. I have been thinking what happened to me, kwanini hiyo Hali sipati jibu, ngoja nifanye research. Hyo Hali ni hatari sana loh
 
Back
Top Bottom