Saikolojia: Fahamu Ugonjwa wa Bipolar Disorder (Kanye West)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
392
1,000
1597594245213.png
Habari wasomaji wangu, wa makala za jifunze saikolojia.

Basi leo nimeleta somo kuhusu ugonjwa wa saikolojia unaofahamika kama Bipolar Disorder. Pengine wengi wetu neno ili au msamiati huu ni mpya kabisa kuusikia au wengi waliousikia lakini hawakuweza ingia kujifunza kuelewa Bipolar ndio ukoje.

Moja ya watu maarufu ambao wameripotiwa kuugua ugonjwa huu ni kama vile Chris Browm na na siku hizi za karibuni ndugu Kanye West.

Jambo ambalo naweza kukuhakikishia tu ndugu msomaji huu ugonjwa hupo sana kwa asilimia kubwa katika jamii yetu. Ingawa wengi watanzania kutokana na uamsho mdogo wa taaluma ya saikolojia hatujafahamu. Na umekuwa na madhara mengi sana kwa jamii yetu na kichochezi cha kuamsha uadui na majeraha ya nafsi baina ya familia, koo na hata nchi.

Siku zetu katika maisha haya, utendaji kazi wetu kuwa unaathiriwa kikubwa sana na hisia zetu ziwe hisia zakufurahi au hisia za huzuni, Hivyo kuwa na mood hasi basi utendaji na mienendo yetu nao unakuwa sio mzuri pia.

Ndio maana kuna msemo unasema usipende kufanya maamuzi makubwa ukiwa na furaha sana au uamuzi ukiwa na hasira.

TAFSIRI

Bipolar Disorder ndio ugonjwa gani huu?

Ni ugonjwa wa kiakili (kisaikolojia) ambapo huambatana na sifa ya mabadiliko ya makubwa ya kihisia yaani (mood) kusipokuwa kwa kawaida,

hasa kugusa utendaji wa mtu bidii na shughuli zake wakati mwingine unasababisha mtu kuwehuka (maniac) na kupatwa na Msongo au sonona (Depression).

Kutokana na namna ugonjwa huu unavyojitokeza inakuwa vigumu sana kama mwanasaikolojia au madaktari kumgundua mgonjwa wa bipolar sababu kuna wakati anatokea kuwa na dalili zote za depression na wakati mwingine kama kuwehuka au kuchizika kitabia iwe gadhabu, furaha au matamanio ya kingono.

Bipolar pia unaweza kujitokeza kwa mtu wa rika au umri wowote au jinsia yoyote pia.

Zipo namna ambazo Bipolar Disorder ujitokeza
  • Namna ya kwanza mtu anaweuka hadi wiki kihisia hadi wiki na kupelekea kulazwa kabisa hospitali.
  • Namna nyingine kuweuka na kupelekea kukosa mood kabisa.
  • Namna nyingine vyote kwa pamoja vina ambatana.


DALILI ZA KUATHIRIWA NA BIPORAL DIS ORDER

Athari kitabia na mahusiano na wengine

Furaha feki ya kifani (Euphoric)

Ushawahi kukutana na mtu ambae sio rahisi kumuelewa mood yake. Yaani kuna siku mnakuwa vizuri tu mnaongea na kucheka na kufurahi (Euphoric) na kupanga mipango mingi tu yaani uchangamfu wa hali ya juu kama hautamuelewa au ukimuelewa utashangazwa jinsi halivyokuwa na furaha kweli.

Kuwehuka kiakili au kupatwa na sonona (Maniac and Depression)
Halafu muda huo huo au baadae mood imebadilika anakuwa na jazba au gadhabu na (si hasira) ya hata kudhuru au kumuumiza mwingine au kuwa/kupatwa na sonona au msongo mzito.

Mara nyingi kuwa haeleweki haeleweki katika maamuzi kutokana na mabadiliko ya mood mara kwa mara hivyo ni rahisi kuathiri mahusiano na mwenza au jamii ya watu wanaomzunguka.

Kuwehuka kwa kuwa na furaha ya kifani (euphoric) kuchizika kuwa na gadhabu zisizoeleweka(maniac)wakati mwingine zikiambatana na ukatili na maamuzi mabaya au kupatwa na sonona (Msongo mzito).

Kuwa na hali ya juu ya kihisia za tendo la ndoa (Hypersexual)
Pia ugonjwa huu una tabia kuathiri utendaji wa mapenzi au hisia za mapenzi

Mara nyingi uathiri utendaji kwa hamu au ashiki kuzidi (hypersexual)

Mambo haya ujitokeza katika utendaji wa hisia za kimapenzi (tendo la ndoa)
  • Kutoridhika kabisa na tendo la ndoa kwahiyo kama mwenza wake anakuwa na changamoto sana kumridhisha.
  • Pia kama kujichua wakati mwingine kuzidi sana kwa tabia hiyo husababishwa na tatizo ili kama lipo katika utendaji kazi wa ubongo wako.
  • Kufanya mapenzi na watu wengi au michepuko mingi
  • Mara chache pia uathiri matatizo ya nguvu za kiume
  • Kama ni watoto au vijana wadogo kupenda onesha ishara za kingono kwa watu wazima (kama tabia hizi hazikurithiwa au kujifunza kwa rafiki anao) unajikuta kama mzazi unajiuliza huyu binti yangu au kijana wangu tabia hizi nyingi kazipata wapi? Au kajifunzia wapi?
Usikose kusoma mwendelezo au sehemu ya pili, ambapo utajifunza ni nini kinasababisha ugonjwa au tatizo hilo? na pia tiba yake.

(Niombe radhi kwa tatizo lolote na kiuandishi na pia kutokana na misamiati mingine ya kitaaluma ambayo haijaweza kupata tafsiri nzuri inapotafsiriwa katika lugha ya Kiswahili ).
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
65,653
2,000
Ni tatizo baya sana...

Kama hujui mtu ana Bipolar unaweza dhania anafanya kusudi...
Mara nyingi wanaonekana kama ni binadamu wa dakika mbili mbele...
 

cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
19,493
2,000
Na hii bipolar hata bongo tunao wagonjwa wengi SEMA huwa tunapuuzia tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom