Saikolojia: Fahamu tatizo sugu la wasiwasi (Anxiety disorder)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
396
687
Saikolojia: Fahamu tatizo sugu la wasiwasi (Anxiety disorder).

1593958900478.png

Imenisukuma wakati huu kuandika kwa ajili ya makala hii kuhusiana na somo la Hofu au uoga kupitiliza na wasiwasi kutokana tatizo hili limekuwa halisikiki lakini lipo kila itwapo leo katika jamii zetu na wapo wengi baadhu yetu tumeona ni kitu cha kawaida sana.

Katika lugha ya kiingereza tatizo la wasiwasi sugu linajulikana kama Anxiety Disorder.

Ni muhimu sana kabla ya kuanza jadili kufahamu kwanza wasiwasi ambao ni suala la kawaida na ule ambao nimeuelezea sugu yaan umeshakuwa tatizo la kisaikolojia ni hupi

Tafsiri ya Kamusi

ni hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu jambo, shaka, tashwishi.

Tafsiri ya Kisaikolojia

tunasema ni hali ya kiasili inayotupata au hali ya mfadhaiko au uoga kutokana na shughuli, suala, tukio au jambo linalokuja au kuhisi linakuja kutukabili.

Muhimu kujua

Fahamu kwamba kuwa na wasiwasi ni muhimu kibinadamu sababu moja ya kazi ya hisia hizi kifiziolojia na kihisia inatupa motisha ya kujiandaa na lolote linalotaka kutukabili.

Mfano 1

Wasiwasi wa juu ya mitihani basi itatufanya tusome kwa bidii ili tufaulu vizuri.

Mfano 2

Wasiwasi juu ya maisha ya kesho itakuaje kiuchumi basi itatufanya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya kijamii au kujiwekea akiba kiulinzi kwajili ya kesho yetu.

Basi kwa maelezo na mifano hapo juu tunajifunza kuwa na wasiwasi si vibaya kibinadamu lakini ni je? kivipi linakuja kwa ni tatizo la kisaikolojia

Wasiwasi ni jambo la kifiziolojia kabisa kwa wanadamu, lakini tunasema linakuwa tatizo la kisaikolojia pale tu linapoweza msumbua mtu kwa kipindi kirefu hata kuweza kuathiri utendaji wa mwili na akili.

Wasiwasi ambao ni ugonjwa wa akili (Anxiety Disorder) utatambua ni ugonjwa kama utadumu muda mrefu na itakuzuia kufanya au kuepuka masuala mengi ya kimaisha, hata kukosa amani furaha na utulivu

Mfano

Paka kulia usiku, kuona paka mweusi au kuumwa homa na kudhani unalogwa,

kuogopa kwamba kuna watu wanafuatilia maisha yako wakudhuru.

Kudhani unasemwa vibaya kila wakati

Mifano ni mingi sana na wapo wengi wamejikuta wakipoteza fedha nyingi tu au kupeleka fedha pasipostahili. Unakuta ndugu ni mwathirika lakini wapo ndugu wanapoteza fedha kwa waganga waanaamini kalogwa na wabaya wake.
  • AINA YA MAGOJWA YA SAIKOLOJIA YANAYOTOKANA NA TATIZO LA WASIWASI.
Panic Disorder tafsiri nyepesi ya Kiswahili ni zile hofu za ghafla inaweza ikawa mfano mtu anashtuka usiku anaanza kupiga makelele au yowe na mnaweza shindwa elewa tatizo ni nini.

Phobia hizi zipo za aina nyingi sana mfano mmojawapo niliuleleza hofu ya kuogopa uchawi (wiccaphobia), hofu ya kuoa/ kuolewa (Gamophobia), Hofu ya giza au usiku (Noctiphobia), hofu ya wadudu (Entomophobia) na hofu ya kutenda dhambi (Peccaphobia) nk

Social anxiety Kuogopa kujichangaya na watu au jamii yako sababu tu kuhisi hawakupendi au wanakuhukumu watakudharau. Hipo kama woga wa watu.

Separation anxiety inaweza kufanana na wivu pale mmoja wa wenza kuwa na hofu isiyo na msingi ya kumpoteza mchumba mume au mke, Hivyo ujipa jukumu la ulinzi dhidi ya watu wa jinsia tofauti na ya kwake na ugomvi usioisha.

Post Stress Traumatic Disorder kwa Kiswahili chepesi tungesema matukio yanayosabaisha majeraha ya nafsi. Mfano kukuta binti anachukia wanaume au anaogopa sababu tu alibakwa akiwa mdogo hivyo hilo linakuwa jeraha kwake. Pia mara nyingi hii uwapata watu waliopitia katika vipindi vigumu kama vile vita, ajali na magonjwa mfano Covid-19. Hivyo inasababisha matatizo ya akili au uoga.

Usikose sehemu ya pili......................Utajifunza Dalili za wasiwasi kama Ugonjwa na pia kwanini watu wanapatwa na tatizo hilo

Soma ...SEHEMU YA PILI
 
Asante,nimekuwa na hili tatizo toka muda mrefu sana na miaka mitano sasa... Kiukweli nilikuwa muhanga wa Masterbation toka nikiwa kidato cha kwanza mpaka namaliza ... Sasa inakuja nikipata demu moyo wangu huzidisha mapigo ya moyo sana .. kana kwamba kuna mtu anakuja kunifumania au kuna mtu anakuja kunikamata, Pia mimi na police huwa sipendi sana kuisikia ,sasa sjui wasiwasi wangu ntawezaje kuutoa ... Hasa Suala nikipata Mwanamke nifanye nae mapenzi hofu na wasiwasi hinizidi nashindwa kujiamini kabisa ... Nafikiria atanionaje nikishindwa kumridhisha ? ... Ataendaje kuniongelea huko kwa wenzake ? .... Doctor please usiache kutoa na Suluhisho nini tufanye ili tuepukane na hili tatizo la wasiwasi .... Asante sana
 
Pia hamu ya Mwanamke kwa sasa imepungua sana japo wanawake ni wengi wanaonitaka .... Nikifikiria kwa umakini kuna mdada mmoja nilimpa mimba aise huyu alikuwa ananipigia simu jioni jioni kabla hata sjala ... Ananitishia ntakupeleka police, ntakufunga, Huyu ndo kanisababaishia hili tatizo kabisa ... Doctor please nahitaji msaada wako nipate kuondokana na hili tatizo
 
Uko vizuri mkuu.Endelea kutupa Elimu hii adhimu.Ni kweli jamii yetu sasa hivi ina shida kubwa sana ya wasiwasi/hofu na hii imepelekea watu kuugua magonjwa km vile presha,kisukari,n.k.
 
Asante,nimekuwa na hili tatizo toka muda mrefu sana na miaka mitano sasa... Kiukweli nilikuwa muhanga wa Masterbation toka nikiwa kidato cha kwanza mpaka namaliza ... Sasa inakuja nikipata demu moyo wangu huzidisha mapigo ya moyo sana .. kana kwamba kuna mtu anakuja kunifumania au kuna mtu anakuja kunikamata, Pia mimi na police huwa sipendi sana kuisikia ,sasa sjui wasiwasi wangu ntawezaje kuutoa ... Hasa Suala nikipata Mwanamke nifanye nae mapenzi hofu na wasiwasi hinizidi nashindwa kujiamini kabisa ... Nafikiria atanionaje nikishindwa kumridhisha ? ... Ataendaje kuniongelea huko kwa wenzake ? .... Doctor please usiache kutoa na Suluhisho nini tufanye ili tuepukane na hili tatizo la wasiwasi .... Asante sana
Usijali mkuu sehemu ya pili ntagusia hilo
 
Nini tofauti ya hofu, machale, wasiwasi, Mashaka na dukuduku?
kuwa na Hofu ni kawaida mfano Hofu ya Mungu tunasema ni normal lakini Woga wa Mungu ni abnormal

Machale huambatana au kubeba tahadhari katika tendo au uamuzi na sio uoga au kuogopa

Wasiwasi soma nimeelezea vizuri ktk tafsiri na mifano yake ila unapoendelea ndio huzaa woga

ni misamiati inayoingiliana lakini ni tofauti



Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom