Saido Antibiotics & Co wanapofufua mipira iliyokufa, wako wapi specialist wa "dead balls" kutoka Tanzania

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,280
Kupitia Runinga leo nimetazama mechi ya Ruvu dhidi ya Yanga, Nilichokiona cha maana leo ni goli la Saido Ntibazonjiza "antibiotic akipiga free kick maridhawa kabisa, nikimtazama vizuri alijiamini mno, body language inaonesha alidhamiria kuupeleka wapi mpira, curve yake si ya kubahatisha kwani ni kama anarudia tu.

Nilipomaliza kumtazama na ufundi wake nikamkumbuka mkali wa krosi na kona Carlinhos, Nikamkumbuka fundi BM23, nikakumbuka Curve zenye nguvu kutoka kwa Konde boy Mickson bila kusahau soft touch zile za kama "Dochi" mpira ukisimama za Triple C Lusaka. At the same time anasubiriwa Djuma Shaban kuja kufanya hayo hayo ya kumwaga maji kiufundi kabisa.

Nikaanza kujiuliza mbona huu ujuzi umeyeyuka kwa wachezaji wetu wa ndani?. Ni nani sasa hivi anaweza kuogopwa akutenga mpira kama wakati ule wa kina Abdi Kassim Babi, Zamoyoni Mogella, Sekilojo fundi, Edibily J. Nakumbuka hata George Masatu alikuwa anaipatia sana hii. Sijahitaji kuwataja kina Nteze na hao wa nyuma zaidi ambao ikiwekwa free kick mnahesabu nusu goli, robo anakosa na robo inakula mti au kipa anatema.

What wente wrong na Free kickers wetu? Au ni yaleyale ya Thadeo Lwanga kuchukua namba ya Mkude na Mukoko Tonombe kumziba Zawadi Mauya.

What went wrong?
 
Mipira iliyokufa mchezaji uwa anajitafutia muda wake ili aifanyie mazoezi, ni Jambo linalo wagharimu wachezaji muda wao mwingi mbaka wawe wanapiga kwa uhakika. Apa bongo sio wachezaji wengi baada ya kocha kumaliza kipindi wao wenyewe wajifunze vitu vipya. Yale unayo yaona kwenye mechi nyuma yake Kuna kazi kubwa ya kujifunza kupiga mipira iliyo kufa. Saido ana nikumbusha Captain wa Yanga Fred Felix kataraiya Minziro na stail yake ya Banana Chop.
 
Kupitia Runinga leo nimetazama mechi ya Ruvu dhidi ya Yanga, Nilichokiona cha maana leo ni goli la Saido Ntibazonjiza "antibiotic akipiga free kick maridhawa kabisa, nikimtazama vizuri alijiamini mno, body language inaonesha alidhamiria kuupeleka wapi mpira, curve yake si ya kubahatisha kwani ni kama anarudia tu.

Nilipomaliza kumtazama na ufundi wake nikamkumbuka mkali wa krosi na kona Carlinhos, Nikamkumbuka fundi BM23, nikakumbuka Curve zenye nguvu kutoka kwa Konde boy Mickson bila kusahau soft touch zile za kama "Dochi" mpira ukisimama za Triple C Lusaka. At the same time anasubiriwa Djuma Shaban kuja kufanya hayo hayo ya kumwaga maji kiufundi kabisa.

Nikaanza kujiuliza mbona huu ujuzi umeyeyuka kwa wachezaji wetu wa ndani?. Ni nani sasa hivi anaweza kuogopwa akutenga mpira kama wakati ule wa kina Abdi Kassim Babi, Zamoyoni Mogella, Sekilojo fundi, Edibily J. Nakumbuka hata George Masatu alikuwa anaipatia sana hii. Sijahitaji kuwataja kina Nteze na hao wa nyuma zaidi ambao ikiwekwa free kick mnahesabu nusu goli, robo anakosa na robo inakula mti au kipa anatema.

What wente wrong na Free kickers wetu? Au ni yaleyale ya Thadeo Lwanga kuchukua namba ya Mkude na Mukoko Tonombe kumziba Zawadi Mauya.

What went wrong?
Mchawi ni BALL CONTROL
 
Back
Top Bottom