SAIDI MWEMA IGP MFANO WA KUIGWA AFRICA.....BRUNDI, RWANDA & tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SAIDI MWEMA IGP MFANO WA KUIGWA AFRICA.....BRUNDI, RWANDA & tz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by cray, Feb 6, 2011.

 1. c

  cray Senior Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  VIONGOZI 105 wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoka nchi za ukanda wa Maziwa Makuu na Kusini mwa Afrika wamemtaja Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jeneralali Saidi Mwema kuwa anashika nafasi ya kwanza katika kusimamia haki za raia na demokrasia.
  Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na viongozi hao wenye taaluma za utafiti, elimu, mazingira, haki za binadamu na maendeleo kutoka nchi za Burundi, Malawi, Uganda, Tanzania, Kenya, Kongo, DRC, Zambia na Rwanda wakati wa mkutano wao wa siku mbili wa kubadilishana utaalamu na uzoefu katika kutatua migogoro na kuchochea maendeleo kwa jamii.
  Mwenyekiti wa mkutano huo kutoka Uganda, Paulo Gabriel, aliwashambulia viongozi wa kisiasa katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu kwa kutengeneza migogoro, migomo, maandamano pamoja na kung’ang’ania madaraka.
  Gabriel aliwatahadharisha wanasiasa wa nchi za Maziwa Makuu na Afrika kumcha Mungu na kuacha kukodolea macho yanayotokea katika nchi za Misri na Tunisia, kwani hayo si mfano wa kuigwa badala yake waachane na kiburi cha kupenda madaraka yasiyoleta tija kwa wananchi.
  Naye Mchungaji Alex Alexander, Mchungaji Philip Kamau na Sheikh Akbar Mohamed kutoka Human Rights DR Congo, wamesema utafiti wao wa miaka minne katika nchi zote za maziwa makuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, chini ya Saidi Mwema, limeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa sehemu ya wananchi tofauti na wakuu wa majeshi ya polisi kwenye nchi hizo ambako polisi ni sehemu ya wanasiasa.
  “IGP Mwema ni mfano wa kuigwa, kwa umakini wake, kwani tumejifunza pia wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hapa Tanzania, ambapo wananchi walikuwa huru kupiga kura kwa utulivu mkubwa ingawa utulivu huo uliharibiwa na wanasiasa wenyewe wakati wa kuhesabu kura, tofauti na nchi nyingi ambako polisi hutumiwa na wanasiasa kuwalazimisha wapiga kura kuwapigia, jambo ambalo huleta machafuko ya kisiasa.

  Source, Tanzania daima.
   
 2. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  teh teh mzee wa Intelijensia kapewa shavu...
  Kweli isiyokuwasha hujailamba
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mzee, nina mashaka na hicho chanzo cha habari au ulikuwa unamaanisha HABARI LEO?
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Binafsi nakubaliana kabisa kuwa IGP Said Mwema ni mfano wakuigwa, nikilinganisha na mtangulizi wake kwakweli watu wa upinzani walipata virungu sana, sote ni mashahidi. Ila hawa watoa maoni waliotangulia nadhani watakuwa wamelewa mbege ndo maani kila kitu wao nikuponda tu. Shame on you.
  Go Mwema go, and wish you all the best.
   
 5. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kaka una linganisha nini na nini? linganisha alichotakiwa kufanya na alichofanya, mauaji ya Arusha, mbeya, na huko kanda ya ziwa ni uchafu. vikao vingine hivyo havina tija vinaweza pata influence kwa kuongea na mmojawao pale nje akaingia ndani na akakusifu basi. Si ulimsikia yule waziri wa mambo ya nje alivyokuwa anajigamba (Membe ) sasa ungekuwa kwenye mkutano mambo huwa hayako hivyo.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mwema ni muuaji wala hastaiki kuigwa ndio walewale wamo kwenye mfumo wa ufisadi kazi kulinda ufisadi. kama intelejensia yao inafanyakazi tusingeingizwa kwenye mikataba feki ya Mkapa na kikwete:twitch:
   
Loading...