Saidi Maulid Mtulia atangaza kugombea tena jimbo lake la Kinondoni kwa tiketi ya CCM

kinundu

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,029
2,129
Aliye kua mbunge WA cuf ambaye alihamia ccm kupitia ukurasa wake wa facebook ametangaza kuchukua form ya ubunge kupitia ccm hivyo kaomba mumuunge mkono kwa mara nyingine..
ef5dec6f13200408b37749dd08dc7821.jpg



--------------

Gazeti Mwananchi limeandika;

Mtulia kuwania ubunge tena

Kwa ufupi

  • Desemba 2 Mtulia amejiuzulu nafasi ya ubunge, huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.

Aliyekuwa Mbunge Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia ambaye amehamia CCM ametangaza nia ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho tawala.

Desemba 2 Mtulia amejiuzulu nafasi ya ubunge, huku akisema amefikia uamuzi huo bila kushawishiwa mtu yeyote na amebaini Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani iliahidi kuyatekeleza.

Baada ya hatua hiyo, chama cha CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba ametangaza kuwaomba radhi wapiga kura wa Kinondoni kwa Mtulia kujiuzulu uanachama kisha ubunge.

Lakini leo Jumanne Desemba 19, 2017 kupitia andiko lake alilolituma kwa vyombo vya habari, Mtulia amesema atachukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya CCM ili agombee tena nafasi hiyo.

“Chama changu kikiridhia nitakwenda mbele ya Wanakinondoni kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya ubunge kupitia CCM. Pia nawapa pole sana kwa maumivu mliyoyapata kutokana na uamuzi wangu wa kujiuzulu ubunge wa Kinondoni,” amesema Mtulia.

Hata hivyo, Mtulia amewahakikishia wakazi wa Kinondoni kuwa bado anawapenda na yupo tayari kutumikia tena kwa lengo la kuleta maendeleo ya jimbo hilo ambalo awali lilikuwa likishirikiliwa na CCM kwa kipindi cha muda mrefu.
 
Naona ya wabunge kumekucha..

Ina maana atakuwa ameona akiwa chini ya CCM atatenda kazi vizuri.. yaani chini ya uongozi wa JPM.

Kapendezwa na hapa kazi tu... hivi huko Chadema si wanalia au?
 
Duh anapataje hiyo confidence??? Ni vile tu hamna tume huru na sio mwaka wa uchaguzi ila wananchi wangemnyoosha ili liwe fundisho kwa wengine kituko na yye ataiba kura wakati 2015 kuna wananchi walivunjwa miguu kisa kumlindia kura leo hiii anahamia kwa watesaji

Kwenye kampeni apigwe mawe huyu mnafki
 
Naona ya wabunge kumekucha..

Ina maana atakuwa ameona akiwa chini ya CCM atatenda kazi vizuri.. yaani chini ya uongozi wa JPM.

Kapendezwa na hapa kazi tu... hivi huko Chadema si wanalia au?
Kupendezwa na magufuli ndio asaliti waliomlindia kura 2015??? Tena hata hakuaga wala kuita mkutano aliibukia tu kwa maCCM

Kuna watu wangefaa kumininiwa risasi 38 na tusiumie ila wanaoetetea wananchi ndio wanapigwa risasi mxeeuwwwww
 
Back
Top Bottom