Said Mwema + Charles Chagonja: Kuparaganyika kwa jeshi la Polisi; Lowassa hapa vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Said Mwema + Charles Chagonja: Kuparaganyika kwa jeshi la Polisi; Lowassa hapa vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 5, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Polisi liko matatani. Polisi wetu wanawaona wananchi kama maadui zao kiasi kwamba hakuna ile heshima ya polisi kwa raia. Tumeyaona Nyamongo, tumeona Songea na sasa yametokea tena Mwanza. Na hatujasahau yaliyotokea Arusha mwaka mmoja uliopita. Kuna dharau ya aina fulani ambayo inaendana na ubabe wa polisi. Kwa mfano, majibu ya polisi kwenye matukio ya Arusha, Songea na Mwanza yamejadaa dharau (contempt) ya wananchi.

  Lakini baya zaidi ni kuwa hakuna mfumo mzuri wa kushughulikia polisi wanapofanya au kutuhumiwa kufanya mambo mabaya ambayo mengine yanapakana na uhalifu. Kwa muda wote huu wa Said Mwema na Mkuu wa "Operesheni na Mafunzo" Bw. Chagonja kumekuwepo matukio mengi sana ya uvunjaji wa haki za raia, matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya raia wasio na silaha na kukosekana kwa umakini katika kushughulikia maandamano au mikusanyiko mikubwa ya watu.

  Kwa kadiri tumeendelea kuwaachilia hawa watu kwa vile wao ni "polisi" ndivyo wanavyozidi kusimamia jeshi with impunity. Hivi ndivyo lilivyokuwa jeshi la Polisi la Hosni Mubarak. Lilikuwa jeshi ambalo lilikuwa linaweza kufanya lolote, kwa yeyote na bila kuulizwa. Leo hii wabunge wawili wamepigwa mapanga "mbele ya polisi" kama walivyodai wenyewe na polisi hawashtuki? Yaani, polisi wale wale wanaotuhumiwa kusimamia kupigwa kwa wabunge wa JMT ndio wameachwa kujichunguza wenyewe? Halafu hao hao wanasema ndio wanataka waje kuwahoji wabunge wanaowatuhumu na Makao Makuu ya POlisi imeshindwa kutoa tamko hata la kuonesha uzito? Ni dharau gani hii kina Mwema na Chagonja wanayo?

  Kamati ya Bunge ya Usalama chini ya Lowassa - anayesremwa kuwa ni kiongozi mwenye nguvu- iko wapi? Hatujawahi kuisikia hata mara moja kuwaita viongozi wa polisi kuwahoji juu ya mambo haya na sasa wabunge wa CDM wamepigwa na Lowassa (Mwenyekiti) hajaonesha hata uongozi wa kutaka kuwatembelea hawa wabunge au kwenda Mwanza au hata kujaribu kuonana na wakuu wa jeshi? Au anafikiria ni usalama wa vitu gani ambao kamati yake inausimamia?

  Viongozi wa CDM niliwahi kuwaambia kuwa wanavyoendelea kulilea jeshi la polisi na kulilalamikia tu ndivyo linavyozidi kuthubutu kuwa wakali (it becomes more hostile) kwa viongozi wa upinzani. Binafsi naamini wakati umefika wa viongozi wa CDM kuitisha maandamano makubwa tu ya kupinga ubovu na uzembe wa Jeshi la POlisi kwani hadi hivi sasa ni wao CDM ndio wanakiona cha moto dhidi ya mkono wa askari wa Mwema.

  Jeshi hili ni la raia (civilian police force) na hivyo nilazime lilazimishwe kujifunza kuheshimu na kujali raia. Siyo polisi wanapoenda kwenye nyumba ya mtu wanaanza kuvunja na kuingia kwa nguvu wakati hawana waranti ya kufanya upekuzi au wanatumia silaha za moto dhidi ya raia wasio na silaha yoyote.

  Nani atathubutu kusema kuwa Mwema na Chagonja waondolewe?
   
 2. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Pamoja sana MMM... salute!!
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mimi nashauri baada ya Bunge kuanza Jumanne Kiongozi wa upinzani bungeni atoe tamko baadae wabunge wa CDM waelekee Mwamza kwenye mkutano mkubwa wa hadhara hata ikiwezekana maandamano ya kulaani vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na jeshi la polisi. Kwa sababu hii sasa imekuwa too much.
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Mkuu MMM,Umetoa uchambuzi mzuri,ila sina hakika kama viongozi wetu serikalini wana masikio!
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Polisi tanzania ni taasisi ya kula rushwa!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hofu yangu ni kuwa wahalifu wanaweza kuwa ndio wanavutiwa kujiunga humo ndani; kwa hivyo hata wale askari wazuri waliomo humo hawang'ari ipasavyo. Ndio maana wakati umefika kuanza kulazimisha mabadiliko ndani ya hili jeshi ili hata watoto wetu na vijana wavutiwe kuingia kutumikia taifa.
   
 7. U

  Ugweno Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkuu, kuna haja ya kulazimisha mabadiliko
   
 8. R

  Rwamarungu Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Personally niliona kitendo kibaya sana cha askari magereza kumpiga dreva wa fusopale traffic lights Magomeni simply kuwa kwa nini hakuwapisha wakati hakuwa na nafasi ya kuwapisha, ikanikumbusha jinsi ilivyokuwa wakati wa vita nchini Sierra Leone, kila nyumba iliyokutwa na waasi ikiwa na vazi la polisi,jaji n.k. ilichomwa moto.

  Vyombo vyetu vya kulinda na kutoa haki vimegeuka vichaka vya kula haki za raia wake.
  Itafika wakati hatutakubali kufa kwa njaa bali kwa risasi.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, nimeipenda hiyo ya Kamati ya Bunge ya Usalama, usahihi, ni Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
  Aliyesema ni kiongozi mwenye nguvu ni mimi kwa kuzingatia haya

  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama itasimamia shughuli
  za Wizara zifuatazo:-
  (a) Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
  (b) Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki;
  (c) Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; na
  (d) Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Baada ya kuisoma thread yako, ndio nimegundua kuwa ni kweli he is supposed to be very powerful, ili nikifanya tathmini amewahi kufanya nini/kamati yake imefanya nini cha maana, sijabahatika kukiona!, nikijumlisha na matokeo ya juzi ya Arumeru, naomba kuendelea kukiri kuwa huyu jamaa yangu, ameisha jichokea, funzo amelipata na pembeni sasa atajikalia!.

  Sithubutu kusema, Mwema na Chagonja waondolewe, bali wananchi waelimishwe udhaifu wa watu hao, kama aliyewateua hauoni udhaifu huo, then for 2015 it makes it easier kwa kuturahisishia kazi, japo by then tutakuwa tumeshaumia sana!. No gain without pain!.

  Pasco.
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mimi nisichokielewa kwa nini ukifanya U turn unakamtwa haya kama hakuna kibao kinachokataza?

  well jeshi la polisi hawataki kujibu hii hoja

  [​IMG]
   
 11. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Labda tujiulize, ni kwa nini asilimia kubwa ya watu waliofeli sekondari na vyuoni (sorry waliopata alama za mwisho mwisho) ndio wanahamasishwa kujiunga na Jeshi la Polisi?
  Wengi wao upeo wao ni mdogo (hivyo ni rahisi kuwabrainwash) na wengine historia zao zinawahukumu tangu shuleni (wana spirit ya uhalifu) na wakitoka CCP wanachojua wao ni rushwa, kupiga na dharau (sijui ndicho wanachofundishwa kule).
  Kila nikisoma ile makala ya mwigamba inayohusu jeshi hili, nashawishika kuamini kuwa mafunzo yao mengi yanawaandaa kuja kuonyesha dharau kwa wananchi
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Masikio wanayo ila hawasikii na macho wanayo ila hawaoni. Kwa kutosikia kwao, tutawasikizisha na kwa kutoona kwao, tutawaonesha!.
   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi nashawishika kuamini kuwa Jeshi letu la polisi lina fanya kazi kwa maelekezo ya wanasiasa wa CCM (waliopo madarakani) na ndio maana mpaka sasa kila mtu yupo kimya!
  Na ndio maana wengi wetu tunashauri nafasi hii ya IGP isipatikane kwa kudra za mwenyekiti wa chama cha siasa bali iwe ni nafasi ya kikatiba inayoombwa na watu makini na wawe wanafanyiwa vetting
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,776
  Trophy Points: 280
  Maandamano nchi nzima ya kupinga unyanyasaji dhidi ya raiya yanahitajika.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni Lowassa. Lakini sijamsikia hata mara moja akiongelea mauaji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na polisi. Sijamsikia akiongea bungeni kudai iundwe tume ili kuchunguza utendaji wa jeshi la polisi. Kazi yake kubwa imekuwa kuhubiri kwenye makanisa na kutoa michango. Hivi hii ndio kazi ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama? Na kadri siku zionavyoenda hali ya usalama wa raia inazidi kuwa tete. Raia hawana imani kabisa jeshi la polisi.
   
 16. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  easy fit, ni kweli kuna jinai tayari imefanyika, na kujichulia sheria mkononi haitakiwi hata kidogo. lakini umejiuliza kwa nini hawataki kuwataja wahusika?
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  mda ukifika, hapo kwenye bolded blue tutafahamu mengi zaidi. kuna uwezekano siyo kweli. tusubiri tuone, kuna mtu ataumbuka hapo. Kama umefuatilia matamshi ya diwani mteule kirumba, anaeleza wakati yote yanatendeka yeye alikuwepo lakini hakutaja POLICE, mbunge kataja POLICE.
   
 18. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Pasco, Leo sijakuelewa umesimamia wapi maana u msemaji au mtetezi mkubwa wa Lowasa.
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Asante sana MMM na wadau kwa ujumla,
  Huu sijui ni (uzi) wa ngapi wenye kuonesha na kulalamikia utendaji mbovu, unyanyasajia na ukosefu wa maadaili wa jeshi Tz. Mengi yamesemwa na kuandikwa lakini hakuna hatua za kuboresha wala nafuu:-
  1) Je watawala hawajui wala hawajasikia?
  2) Kazi ya TISS ni nini katika suala husika?
  3) Jeshi la Polisi TZ ni kwa maslahi ya nchi au chama na watu fulani tu?
  4) Dhana ya ulinzi shirikishi ubunifu wa kiini macho au umekwamishwa na wahalifu wachache ndani ya PT?
  5) Hiyo Kamati ya Kudumu ya Bunge mbona ni mkono mwingine wa watawala wenye kutawaliwa na ubinafsi?

  Baada ya kujibiwa hayo hapo juu, nafikiri hivi:
  Ni lazima tupate Katiba Mpya Tz. Ni LAZIMA. Katiba ifumue, ifutilie mbali sturcture za sasa za PT kwani ni ya miaka ileee ya chama kushika hatamu. Kisha itengeneze structure na ethics mpya za PT.
   
 20. N

  Njaare JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji,

  Kumbuka kauli ya Lusinde kuwa wanakifahamu wanasiasa wanaoenda mahabusu wanachokifanyiwa. Haitashangaza kuona kuwa kama wanakifahama basi ndo wanakipanga. Hivyo yaweza kuwa Lusinde alikuwa anaisemea kamati ndo maana haichukui hatua.
   
Loading...