Said Meck Sadick Mkuu wa Mkoa wa Lindi ni mzigo kwa CCM kwani anawalizimisha wanachi kuwa masikini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Said Meck Sadick Mkuu wa Mkoa wa Lindi ni mzigo kwa CCM kwani anawalizimisha wanachi kuwa masikini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dostum, Jun 18, 2011.

 1. d

  dostum JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambae pia ni kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Said Meck Sadick sijui yupo kwa maslahi ya nani. Tuna nina wasiwasi viongozi wanaopelekwa mikoa mingine ambao si wazawa wa eneo husika wanakua na agenda za makusudi wa kuwadumaza wenyeji. Au huenda uwezo wao kiutendaji umekua mdogo na kuwa mzigo kwenye siasa zenye ushindani zinazoendelea. Uwezo wa kiutendaji wa mkuu huyu umeonekana kuwa mdogo hata wakati wa suala ya mabomu ya gongolamboto alivyolishughulikia. Mkuu huyu amewalazimisha wakulima wa ufuta mkoani Lindi kuuza mazao yao kwa bei ya shs 1,000/-kupitia mfumo wa stakabadhi badala ya shs1,200/- – 1,500/- kwa kilo, ni kwa maslahi ya nani? Ni kwa Maendeleo ya wakulima? auya kwake? Mkuu huyu wa mkoa alituma askari wakiwa na silaha na risasi za moto kwa ajili kuwalazimisha wakulima wasiuze kwa bei hiyo na atakaekaidi ametishia atauwawa. Wakulima hawa kipindi cha kilimo walikwenda serikalini kuomba msaada wa askari waje kuuwa wanyama waharibifu walioharibu mazao kama ufuta na serikali ilisema haina risasi ya kuwaulia. Sasa iweje wakati wa kuuza mazao yao yaliyobaki serikali inawafata wakiwa na risasi za moto kwa ajili ya kumuua mtu yeyote atakae kaidi amri ya huyu mkuu wa mkoa. Mkuu huyu ambae ni mwenyekiti wa Kamati ya ushauri ya maendeleo ya mkoa wa Lindi imelikataa pendekezo la wabunge la kutaka zao la ufuta liondolewe katika utaratibu wa kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani kwa kuwa unawanyonya na badala yake wauze kwa wafanya biashara. Mapendelekezo hayo yamekataliwa kwa kuwa tu wabunge ni wa chama cha upinzani CUF.Mimi nikiwa mpenda maendeleo nadhani Mkuu huyu ni mzigo kwa CCM na anawalizimisha watu kuwa masikini.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Said Meck Saddick mkuu wa mkoa wa Lindi na huku anakaimu ukuu wa mkoa wa Dar es Salaam? Hivi Tanzania ina shida ya viongozi kiasi kwamba mtu mmoja anakuwa na majukumu mengi kiasi hicho? Na inakuwaje mkuu wa mkoa wa Lindi (ambao ni hundreds of kilometers aways) akaimu ukuu wa mkoa wa Dar es Salaam? practically hii inakuwaje? Na Dar es Salaam is not like any other city, hapa ndio kitovu cha shughuli zote za nchi!

  Huu mzaha inabidi ukomeshwe.
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  mkuu hata asipokuwepo hakuna kinachoharibika, acha tu ale kuku wakuu wa wilaya wanatosha
   
 4. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kuna posho hapo... anagawana na anayempa
   
 5. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua huyu mzee ni lofa alipata kuwa Mkuu wa WIlaya ya Tanga Mjini (2000), wakati ule Mrs. Nuru Millao alikuwa District Administrative SEcretary, lakini mama alikuwa ametulia na alikuwa anaheshimika kuliko huyo Mecky Sadiq, haikunishangaza kusikia Nuru Millao alikuja kuwa Regional Administrative SEcretary wa Arusha...na sasa ni Naibu Katibu Mkuu wizara mojawapo....where is Mecky? Anaendeleza utumbo wake....

  Hii ndiyo mizigo ya CCM
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Samahani ndugu yangu, naujua sana utaratibu huu nina maswali amabyao yanataka majibu.
  1. Je huu ndio wakati wa mavuno au /
  2. Je hiyo 1500 na 2000 ndio maximum bei wanayoweza kupata?

  Wadau utaratibu wa stakabadhi ghalani upo hivi,
  kwa kuwa wakati wa mavuno supply huwa inakuwa kubwa sana na beio huwa inashuka serekali kupitia mabenki ikaleta utaratibu kuwa kwa wakati huo bei inpokuwa chini wakulima wanauza mzigo kwenye mabenki na kupewa bei fulani ya chini na bei ya soko wakati huo, ila kwa kuwa m,zigo upo ghalani ikifika kipindi bei inakuwa maximum ndio mzigo unaunzwa chini ya uangalizi wa benki na kwa vyovyote bei huwa inakuwa juu sana. kwahiyo benki inatoa bei ya mwanzo na riba kidogo na mkulima anajikuta anauza kwa bei ya juu na yenye faida.
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nini maana ya kusoma sasa,kama mtu mmoja ana vyeo 700 kidogo,mimi nadhani hata wakuu wa mikoa wangekuwa wanagombea hizo nafasi kuliko haya mambo ya kuteuwana,yaaaaaani watanzania milioni 40 bado mtu mmoja anavyeo kibao,haina maana ya kuwa na wasomi ktk hii nchi kama ndio hivyo
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa Mecky Sadikki ndio zile nafasi za kupeana na kulipa fadhila!!jamaa ameoaa ukoo wa Mwinyi mzee ruksa!!alikuwa dereva wa Mwinyi muda wote wa miaka 10....sasa aka pick ka binti akajuaa lazima na yeye atapewa fadhila ili wasilie njaa kwa mzee siku zote.....anabebwa kwa jina baba mkwe!!period!!
   
 9. faithful

  faithful JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Usilo lijua ni usiku wa giza....hao wafanyabiashara unaowaongelea ni wahindi na ni wezi kichizi....huwa wanaanza na bei ya juu makusudi kupita ile ya mfumo ili wananchi waukatae mfumo ila wakishapata ruksa ya kununua hushusha bei kwa kasi sana kwa maslahi yao....ushahidi uliza wana mtwara na lindi kuhusu uuzaji wa korosho miaka4 iliyopita au uliza uuzaji wa choroko mwaka huu hukohuko washenzi walitangaza bei 1500 wakaishusha hd mia5.....pia nakuelimisha hakuna mnyama anakula ufuta ht mmoja ni wadudu ambao hawauliwi kwa silaha....;mwisho mfumo huo mkulima analipwa malipo awamu tatu!nakushaurifanya utafiti pande zote mbili kabla hujalaumu.
   
 10. d

  dostum JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ahsante wadau kwa michango yenu. kwa mujibu maelezo ya washika dau (watu wa karibu wa maendeleo wa Lindi) ni kwamba mazao yanayokua ktk mfumo ya stakabadhi yanasimamiwa na bodi husika bali zao la ufuta halina bodi na hivyo hawakupaswa wakulima kulazimishwa kupitia mfumo huo.

  Pili mfumo huu haupingwi kama kukiwa na usimamizi mzuri bali kwasasa msimamizi mkuu ni Mr. Sadick ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ushauri wa maendeleo ndie mzigo. Mfano halisi mwaka jana ufuta ulizwa kwa njia ya stakabadhi kwa shs 1000/- na baadae waliahidiwa watalipwa 650/- matokeo yake walikuja kulipwa 120/- tu na inasemekana wengi wa wakulimwa hao hawakulipwa, bali wale wakulima waliouza kwa kujificha kwa mwaka jana kwa wafanya biashara waliuzwa hadi shs 1500/-.

  Nashaukuru pia kuwa wabunge wetu wamelisema hili bungeni wiki iliyopita na waziri kalitolea ufafanuzi kuwa sheria haiwabani wakulima, kuwa si lazima wauze ufuta njia ya stakabadhi bali watauza watapoona kuna manufao kwao. Ingawa hii si mara ya kwanza kwa viongozi ambao ni mizigo kutoa kauli zinazokinzwana pasipo wanufaisha wahusika.
   
 11. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  .
   
 12. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2017
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,911
  Likes Received: 12,091
  Trophy Points: 280
  Jamiiforums katika ubora wake!
   
Loading...