Said Lugumi Kosa lake ni Kuwa Darasa La Saba Au what?

W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
STRAIGHT TALK:- Kwa wiki nzima sasa Wananchi wa Tanzania tumekuwa tukipokea taarifa mbali mbali za Media na Wanasiasa kuhusiana linaloitwa sakata la Mkataba wa Polisi na Mfanyabiashara maarufu hapa nchini Said Lugumi,kilichomtokea Said ni kama yaliyowatokea Mkurugenzi wa zamani wa NSSF Ramadhani Dau na Mfanyabiashara maarufu pia hapa nchini Ghalib (GSM).

Wananchi Masikini kama kawaida yetu tumekuwa tukizipokea habari hizi zenye utata mwingi wa Vyanzo vyake na nia na madhumuni ya wanaotupatia bila kuuliza wala kujiuliza maswali ya msingi na matokeo yamekuwa ni wazungu wanaita "MOB LYNCHING" au "MOB JUSTICE" bila kujali FACTS wala EVIDENCE so kilichofanyika mpaka sasa ni kuwakaanga hawa Wananchi kwenye Public Opinion halafu baadaye kutafuta kuwahukumu kwenye Mahakama ya National Politics.

Ingawa on the other hand, watuhumiwa hawa wote wana one common denominator nayo ni wote ni Marafiki wa Karibu wa aidha Rais aliyepita au Familia yake, mashambulizi hayo yamekuwa nonstop na bila huruma kila siku kukitolewa mambo mapya na ya kutisha lakini hakuna kitengo wala sehemu ya sisi Wananchi kutafuta FACTS isipokuwa watu kama mimi ambao kwa kuzaliwa na kukulia kwenye National Politics tumejifunza kuwa waangalifu sana kabla ya kutoa maoni ya ishu yoyote inayohusu National Politics kwa sababu kwa kawaida huwa unaambiwa habari bila kuambiwa agenda na wimbo huo ameutunga nani.

Tukianza na Mfanyabiashara maarufu Ghalib, yeye alikuwa mtuhumiwa wa kwanza wa hii Kangaroo Court ambayo Prosecutors wake wanajulikana ni nani na ni nini agenda yao, lakini cha muhimu ni kwamba kwa watu kama mimi tunajua kwamba tatizo namba moja la Ghalib ni kuwa Rafiki wa Familia ya Rais aliyepita, sasa some of us tunabaki tunajiuliza je tatizo ni Urafiki au ni kweli wana makosa? Takwimu na maelezo yote ya Bandarini hakuna sehemu hata moja ambapo Ghalib amekutwa amehusika na faulo yoyote ya kupitisha Makontena bila kulipiwa lakini wapo waliopatikana now ungetegemea in a perfect system of life Media na hawa Volunteers Public Prosecutors wangemuomba radhi Ghalib kwa kumchafua sana bila FACTS lakini wapi waliposhindwa kumnasa Ghalib wakamrumkia Dr. Dau Ramadhani na yeye wakamkaanga kwenye Public Opinion mpaka akawa amebakia kuzikwa kwenye kaburi la Rais Magufuli ambaye wanaamini kwamba wakianza tu kumshambulia mtu yoyote maarufu basi atawasikiliza bila FACTS na kumkaanga.

Rais Magufuli aliwashangaza sana majuzi kwenye kufungua Daraja la Kigamboni alipomuita Dr. Dau the masterminder wa ujenzi wa daraja lile aje aongee na the very same Public iliyokuwa na hamu kubwa ya kuona Rais Magufuli akimkaanga Dr. Dau, ambaye mimi binafsi nimekuwa nikimtetea kwa muda mrefu sana kwenye Social Media kwamba Dr. Dau ana akili ya kuwa Rais sio Mkurugenzi tu wa NSSF kama alivyokuwa. Sasa baada ya kuona Dr. Dau hana hatia kesi ya Public Opinion sasa ikahamishiwa kwa Said Lugumi kwamba ni jipu kwa sababu ameshirikiana na Polisi kuliibia Taifa kwa sababu ameoa mtoto wa Mkuu zamani wa Jeshi la Polisi Mzee Said Mwema ambaye alimpa Mikataba kuholela na ni kwa sababu Kampuni ya Lugumi ina washiriki wawili muhimu yaani Mtoto wa Rais aliyepita na Mkuu wa zamani wa Polisi.

Lakini siku chache baadaye sasa imeshajulikana kwamba sio kweli kwamba Lugumi ameoa mtoto wa Mkuu wa zamani wa Polisi Tanzania na si kweli kwamba Mtoto wa Rais wa zamani ana hisa kwenye kampuni hiyo na infact hata Documents za Lugumi tulizoambiwa zinatafutwa sana na Kamati ya PAC ya bunge kwamba zina a bomb la kumfunga Lugumi for the rest of his life kumbe ni hadithi tu za mtaani ukweli ni kwamba Lugumi amefunga mitambo yote kama alivyoagizwa kwenye mkataba wake na Polisi kwa hiyo habari zote tulizouziwa kwenye media na Wanasiasa nawaita Uchwara zilikuwa ni kutuuzia mbuzi kwenye gunia tu. Sasa habari mpya ni kwamba kinachotafutwa sio wizi wa Lugumi bali ni thamani ya mitambo aliyofunga kama kweli inafikia thamani ya pesa aliyolipwa na Polisi.

Now in a perfect system ungetegemea hata PAC wamuombe radhi kama walivyoshitaki kwa Public lakini wapo kimya. Kwa haya yote some of us tunabaki na maswali mengi kuliko majibu kwamba je kuna kikundi cha Wanasiasa wanaolala macho kuwagonganisha Rais wa sasa na aliyepita? I mean mfano ni kawaida ya National Politics kwamba kila anapoingia Rais mpya ni lazima aje na watu wake wapya isipokuwa kunakuwa na utaratibu wa kuwabadilisha pole pole mpaka Rais mpya anapokuwa ameridhika kwamba sasa ana team yake nzima ni mambo ya kawaida Dunia nzima, lakini Rais Magufuli alipombadili Katibu Mkuu Kiongozi kuna gazeti moja maarufu sana nchini likalia kwa sauti kubwa sana kwamba "HATIMAYE RAIS MAGUFULI AMMALIZA MASALIA WA MWISHO WA KIKWETE"

Jamani Tanzania tumefikia huku lini kwenye siasa uchwara ambazo sasa kwa maneno mengine tunaanza kuambiwa hata kuwa rafiki na Rais na familia yake ni makosa ya kutosha kushitakiwa kwenye Public Opinion. Sasa ukweli umeshajulikana kwamba Said Lugumi hajaoa mtoto wa Kamishna wa zamani wa Polisi, Kwamba Kampuni yake haina ubia na mtoto wa Rais wa zamani, na kwamba Said Lugumi ametimiza masharti ya mkataba wake wa kuweka mitambo ya kufanyia kazi za Polisi kama mkataba ulivyomtaka, sasa kwanini Public Prosecutors hawajajitokeza kuomba radhi au hata kujiosha kwa makosa makubwa sana ya kumchafua mwananchi wa Tanzania kijana mdogo ambaye kosa lake sasa linaonekana kuwa na urafiki na mtoto wa Rais wa zamani na kuwa na pesa akiwa na umri mdogo. Inasikitisha sana kwamba kwenye kumshambulia mara kwa mara our rotten National Media imekuwa ikilia sana kwamba Lugumi ni darasa la Saba ambaye alikuwa Shoe Shinner tu, which in the process unknowingly sisi wenyewe tunadharau system yetu wenyewe of Education kwamba Darasa letu la Saba haliwezi kutoa kijana mdogo kama Said Lugumi akaishia kuwa Mfanyabiashara mkubwa mpaka kuaminiwa na Taifa letu kuwaletea Polisi mitambo ya kisasa.

It is wrong and unfair, lakini ninaamini kwamba kuna kikundi chenye agenda hii maalum ya kuwachafua wale wote waliokuwa marafiki wa Rais na familia yake bila ya ushahidi wala facts isipokuwa wanategemea uwezo mdogo wa our Public kuelewa na kufikiri, umefika wakati wa Kamati ya PAC kumuomba radhi Said Lugumi, badala ya kuanza kumtafutia kesi mpya ya thamani ya mitambo ambayo pia haitasimama kwa sababu kulikuwa na kamati ya wataalamu wa Polisi iliyoridhia kwamba bei aliyoitoa Said Lugumi ni sawa sawa kabisa pamoja na malipo ya kuwaleta wataalamu maalum wa mitambo hiyo kuifunga kila mkoa wa Tanzania. PAC muombeni radhi tu Lugumi na Jeshi la Polisi kwa sababu ni Kamati yenu ndiyo iliyokuwa chanzo cha madudu yote tuliyoyasikia kwenye media zetu chanzo ni nyinyi!! - Le Mutuz Nation
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,158
2,000
Kusoma yote ina bore, nimeishia paragraph ya kwanza na kichwa cha habri tu; kosa la Lugumi sio elimu yake wala uhusiano wake na wenye mamlaka, KOSA lake ni hili; kwanini aingine mkataba wa kufunga mitambo vituo 108 halafu afunge vituo 14 tu na pesa alipwe 99%? Hi ni kwa mujibu wa kamati ile ya bunge.
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,088
2,000
Na na na na!..unajuwa kwa sasa wanasiasa uchwara wanapapasa kila pahala ili kupata kiki....ila ngoja tuweke akiba ya maneno ili tupate fursa na uhalali wa kulijadili kwa uhakika baada ya ripoti ya kamati ya bunge.
 

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,863
2,000
Mkuu yawezekana una dhamira ya dhati kuwatetea/kumtetea Lugumi...

Yawezekana ni kweli hana hatia...

Ungeweka na evedence kidogo ingesaidia...

Tunaomba umfikishie Magufuri taarifa kuwa aache kutumia mob justice kutumbua majipu hata kama kweli ni majipu kama alivyofanya juzi pale juu ya daraja!
 

W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
Kusoma yote ina bore, nimeishia paragraph ya kwanza na kichwa cha habri tu; kosa la Lugumi sio elimu yake wala uhusiano wake na wenye mamlaka, KOSA lake ni hili; kwanini aingine mkataba wa kufunga mitambo vituo 108 halafu afunge vituo 14 tu na pesa alipwe 99%? Hi ni kwa mujibu wa kamati ile ya bunge.
- Ni uongo wa kitoto Lugumi amefunga vituo vyote kasoro 4 tu na yupo kwenye masharti ya mkataba na muda, ni uzushi mtupu!!

le Mutuz
 

W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
Mkuu yawezekana una dhamira ya dhati kuwatetea/kumtetea Lugumi...

Yawezekana ni kweli hana hatia...

Ungeweka na evedence kidogo ingesaidia...

Tunaomba umfikishie Magufuri taarifa kuwa aache kutumia mob justice kutumbua majipu hata kama kweli ni majipu kama alivyofanya juzi pale juu ya daraja!
- Wanaomtuhumu Lugumi hakuna aliyeweka evidence, sasa kwa nini yeye aweke mapema hivi?

le Mutuz
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom