Said Issa Mohamed aionya CCM

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111
CHADEMA nayo imeionya CCM kuacha kupandikiza mbegu za udini kwa kuwatumia waumini wa dini ya Kiislamu katika kampeni za jimbo la Igunga.

Onyo hilo lilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Saidi Issa Mohamed, akisema CCM imeanza kuwatumia baadhi ya viongozi wa Kiislamu kueleza kuwa chama hicho kimemdhalilisha mkuu wa wialaya ya Igunga kwa kumvua Hijab, hivyo wananchi wakikatae.

Alisema viongozi wa dini, kwa bahati mbaya bila kutafakari, wamejikuta wakiwa sehemu ya timu ya kampeni za CCM ambacho hivi sasa kina hali mbaya katika kampeni hizo.

“Naliomba Baraza la Maulamaa kuwa makini na wanasiasa,” alisema na kuwaomba wavute subira juu ya jambo hilo kwa kuwa liko mahakamani.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Mkoa wa Tabora, Kansa Mohamed, alisema serikali ya CCM imekuwa ikizitumia taasisi za dini na viongozi wake kufanikisha ushindi wake kwenye chaguzi mbalimbali.

Alisema mwaka 2000, CCM ilieneza propaganda kuwa CUF ni chama cha kidini lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa Kiislamu aliyesimama na kupinga kauli hiyo.

Alisema mwaka 2010 CCM ilikuja na propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha kidini na Waislamu wakahimizwa kumchagua Kikwete ambaye leo hii amebainika kuwa aliwahadaa juu ya Mahakama ya Kadhi na shule zilizotaifishwa. “CCM inataka kuwagawa Waislamu na Wakristo ili iendelee kutawala; Watanzania wawe makini na jambo hili,” alisema.

Source : Tanzania Daima
 
CHADEMA nayo imeionya CCM kuacha kupandikiza mbegu za udini kwa kuwatumia waumini wa dini ya Kiislamu katika kampeni za jimbo la Igunga.

Onyo hilo lilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Saidi Issa Mohamed, akisema CCM imeanza kuwatumia baadhi ya viongozi wa Kiislamu kueleza kuwa chama hicho kimemdhalilisha mkuu wa wialaya ya Igunga kwa kumvua Hijab, hivyo wananchi wakikatae.

Alisema viongozi wa dini, kwa bahati mbaya bila kutafakari, wamejikuta wakiwa sehemu ya timu ya kampeni za CCM ambacho hivi sasa kina hali mbaya katika kampeni hizo.

"Naliomba Baraza la Maulamaa kuwa makini na wanasiasa," alisema na kuwaomba wavute subira juu ya jambo hilo kwa kuwa liko mahakamani.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Mkoa wa Tabora, Kansa Mohamed, alisema serikali ya CCM imekuwa ikizitumia taasisi za dini na viongozi wake kufanikisha ushindi wake kwenye chaguzi mbalimbali.

Alisema mwaka 2000, CCM ilieneza propaganda kuwa CUF ni chama cha kidini lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa Kiislamu aliyesimama na kupinga kauli hiyo.

Alisema mwaka 2010 CCM ilikuja na propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha kidini na Waislamu wakahimizwa kumchagua Kikwete ambaye leo hii amebainika kuwa aliwahadaa juu ya Mahakama ya Kadhi na shule zilizotaifishwa. "CCM inataka kuwagawa Waislamu na Wakristo ili iendelee kutawala; Watanzania wawe makini na jambo hili," alisema.

Source : Tanzania Daima
Hapo kwenye red pamenivutia coz jamaa wanatumiwa kama toilet paper bila wao kujijua.
 
linalosemwa lipo, viashiria vya udini chadema vinaonekana ndio maana wanasema watu wanasema ni chama cha kidini.
 
Bora mseme nyie labda wanaweza kuwaelewa wasiotaka kuelewa juu ya hizo propaganda za Magamba
 
linalosemwa lipo, viashiria vya udini chadema vinaonekana ndio maana wanasema watu wanasema ni chama cha kidini.
Hapo kwenye Red panadhihirisha sentesi yako inachain ndefu ya hear says. Na wewe unasemaje baada ya hao unaosema wamesema??
 
Bora mseme nyie labda wanaweza kuwaelewa wasiotaka kuelewa juu ya hizo propaganda za Magamba

huku jf kuna wanafiki siku ile jk kazungumzia suala la mahakama ya kadhi mukamsifu ujue jinsi cdm wanavyo wachukia waislam hata mkichukia hamuwezi zima nuru ya mwenyezi mungu kwa midomo yenu na huyo said mohamed ndio walewale wake zao wanavaa vimini
 
Ccm inajua dini legelege ni ipi na hiyo dini imegeuzwa toilet paper ..!watatumiwa then wakija kupiga tathmini wamebaki na ndevu ndefu au nikab!
 
linalosemwa lipo, viashiria vya udini chadema vinaonekana ndio maana wanasema watu wanasema ni chama cha kidini.

Ni kweli viashiria vipo ndio maana mgombea mmoja aliitwa na kiongozi wa dini mojawapo kuwa ni chaguo la mungu na sikusikia kiongozi yeyote wa dini wala siasa akihoji uhalaliwa kauli kama hiyo.
 
CCM, nawapa Ushauri japo najua hamna vichwa vya kushika; Mnajua kuwa Taliban ilihasisiwa na Marekani ili kuwadhibiti Warusi kule Afghanstan? Mnajua kwamba I Bin Ladin alipewa mafunzo na misaada na Wamarekani wakati wa vita baridi?
Na nyie Mkishamaliza kuandaa Udini kwa ajili ya kupambana na Chadema na Mapambano yakiisha hakikisheni mnalo zizi la kutosha la kuufungia huu uhalifu au Udini utakaokuwa umepevuka kipindi hicho. Kama mna kumbukumbu isiyo na shaka mmewalea akina Sheikh Ponda, Sheikh Khalifa, Kundecha, Magezi, Mazinge n.k wakati wa kumdhibiti Mrema mlipomwona ni tishio, na hao ndio sasa pamoja na uchache wao, wakikosa hela ya kula tu wanawatia jamba jamba. Je wakiwa wengi itakuwaje wakati huo.

Huu ni ushauri tu, mtaukumbuka.
 
huku jf kuna wanafiki siku ile jk kazungumzia suala la mahakama ya kadhi mukamsifu ujue jinsi cdm wanavyo wachukia waislam hata mkichukia hamuwezi zima nuru ya mwenyezi mungu kwa midomo yenu na huyo said mohamed ndio walewale wake zao wanavaa vimini

acha kutumia masaburi kufikiri kauli ya kikwete ilisifiwa na CDM au ilisifiwa na viongozi wa dini ya kikriso? mwenzio Maralia sugu jana alinzisha thread kuuliza msimamo wa CDM kuhusu hiyo mahakama fuatilia uone na hapo kwenye red hili nalo linakujaje hapo? Zinduka kaka...

nyie pandeni tu hizo mbegu lakini muombee ziangukie kwenye udongo usio na rutuba na zisije kunyeshewa mvua zikaota, mbali na hapo mtajua kua matunda ya mbegu hizo ni machungu zaidi ya hizo elfu kumi mnazopewa na hao wanaowatuma!
linalosemwa lipo, viashiria vya udini chadema vinaonekana ndio maana wanasema watu wanasema ni chama cha kidini.
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom