Elections 2010 Said Arfi atangaza kung’atuka 2015, wananchi waangua kilio

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
May 12, 2011
arfi-CACD8HG5-195x110.jpg


BAADHI ya wakazi na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mjini Mpanda mkoani Rukwa, waliangua vilio baada ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi kutangaza nia ya kutogombea tena ubunge kwenye jimbo hilo ifikapo mwaka 2015.

Arfi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara, ametangaza nia hiyo wakati anazungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kuhutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.

Mbunge huyo kutokana na mabadiliko ya kisiasa yaliyopo hivi sasa ambapo vijana wanajitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo na kuwa na mvuto mkubwa wa kisiasa unaowafanya wakubalike zaidi, ameona kuna haja ya yeye kuachia ngazi kwa heshima.

Baada ya kutoa kauli hiyo, zililipuka kelele za kupingana na uamuzi wake kwa kutogombea tena, na wananchi wengine wakiwemo kinamama na wazee waliangua vilio na kumtaka kufikiria upya suala hilo kwa kuwa tofauti na hivyo wakati utapofika wanaweza kupiga kura za hasira.

Arfi alilazimika kusimamisha hotuba yake kwa zaidi ya dakika 10 na alipoendelea, aliwaeleza kuwa kilio chao amekisikia, hivyo wampe muda wa kutosha atafakari, lakini siku ya mwisho wataelewana.

Akizungumza kwa simu akiwa safarini kwenda Namanyere wilayani Nkasi ambako kumefanyika mkutano wa hadhara cha Chadema, Arfi alisema vilio na kauli za wananchi kwenye ule mkutano zimemgusa sana na anafikiria upya uamuzi wake.

"Dhamira yangu ni kutogombea tena mwaka 2015 kutokana na mabadiliko ya kisiasa yanayojitokeza nchini ukizingatia kwamba vijana wana mvuto zaidi wa kisiasa, lakini kwa hali ilivyojitokeza jana, imenilazimu niheshimu maamuzi yao ili nisiwavunje moyo. Lakini bado ni mapema tusubiri muda ukifika," amesema Arfi mwenye kipindi cha pili sasa cha ubunge katika jimbo hilo la mkoani Rukwa.

Akihutubia umati wananchi wa Mpanda Mjini, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alikemea siasa za chuki nchini na kuwataka wananchi kuelewa kwamba, wanachokifanya Chadema ni kuikosoa Serikali ili kuhakikisha nchi inakuwa na mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi na si vinginevyo.
Alisema, maendeleo ya kisiasa na kiuchumi katika nchini yanaweza kupatikana iwapo kutakuwa na viongozi waadilifu na wasio mafisadi.
 
daaaaah hivi JK wamewahi kumlilia mahali???? daaah eeeh mungu muumba wa mbingu na ardhi nipe afya njema na moyo wa subira niione nvhi hii ikichukuliwa na CHADEMA 2015
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom