Kitambaa cheusi nyuma kulia kwenye magari yote ya Saibaba ni cha nini?

KASRI

Member
May 2, 2009
93
22
Nikiwa njiani nakuja Arusha kwa sikukuu nilielezwa kuwa mabasi yote ya Saibaba yana HIRIZI nyeusi kwa nyuma nje upande wa kulia juu.

Kwa niliyopishana nayo siku hiyo niliona kitu kama kitambaa cheusi kweli.
Je, ni kweli ni hirizi au ni aina ya kitambulisho?

Kama ni hirizi wanategemea nini kwa wateja/wasafiri wanaoiona?

Nawasilisha.

Picha inayoonesha kitambaa cheusi.
saibaba.jpg
 
ni kweli hiyo kitu ipo........
lakini nadhani ni urembo tu.....
 
ni kweli hiyo kitu ipo........
lakini nadhani ni urembo tu.....
kweli hio kitu ipo-
nazani ni zaidi ya urembo maana kijitambaa chenyewe ni kidogo,na usipokuwa makini hukioni,so kama ni urembo ungewekwa sehemu kila mtu auone
 
ukitoa tatoo,shanga za viuoni,vipini n.k hivyo vinaweza kuwa wazi au la
ila urembo wa sai baba ni tofauti na hivyo nilivyotaja

lazima uwe tofauti na urembo mwingine.....ili waweze kuvutia wateja wao......
 
ni kweli hiyo kitu ipo........
lakini nadhani ni urembo tu.....

hakuna urembo wa namna ile, urembo gani umefichwa kwenye kona kiasi kwamba si rahisi kuona mpaka uwe mdadisi, ninavojua mimi urembo ni kitu kinachotakiwa kionekane ili kuleta taswira nzuri au yenye mvuto, mimi nadhani kale kakitambaa keusi kana uhusiano na ushirikina!
 
hakuna urembo wa namna ile, urembo gani umefichwa kwenye kona kiasi kwamba si rahisi kuona mpaka uwe mdadisi, ninavojua mimi urembo ni kitu kinachotakiwa kionekane ili kuleta taswira nzuri au yenye mvuto, mimi nadhani kale kakitambaa keusi kana uhusiano na ushirikina!

je kama mwenye mabasi ameona aweke urembo ule unaomvutia yeye....na kuna baadhi ya abiria wanaupenda.....
kila siku yale mabasi yapo barabarani......inawezekana ndio huo mvuto unaovutia abiria.......

 
Happy Xmas wanaJF!
Nikiwa njiani nakuja Arsha kwa sikukuu nilielezwa kuwa mabasi yote ya Saibaba yana HIRIZI nyeusi kwa nyuma nje upande wa kulia juu. Kwa niliyopishana nayo siku hiyo niliona kitu kama kitambaa cheusi kweli.
Je ni kweli ni hirizi au ni aina ya kitambulisho?
Kama ni hirizi wanategemea nini kwa wateja/wasafiri wanaoiona?
Nawasilisha.
Hivi haya mabasi yanavyopishana kwa kasi uliwezaje kuona kitu kidogo kama hirizi, tena ikiwa juu wakati wewe uko kwenye basi linalokwenda upande linakotokea basi unalolichunguza?
 
Back
Top Bottom