Sahihi kusema Arusha ndio Jiji bora Tanzania?

mdazi

JF-Expert Member
May 10, 2016
661
541
Ni miaka 10 tu imepita tangu mji huu maarufu kama Geneva of Africa utangazwe kuwa jiji.

Kutoka kuwa mji wa 9 kwa wingi wa watu hadi kuwa mji wa 3 kwa sensa ya mwaka 2012 na halmashauri ya jiji ya pili kwa wingi wa watu, licha ya upya wake.

Lakini ndio jiji lenye hospitali nyingi za private kwa uwiano wa watu kuliko mji wowote Tanzania sambamba na international schools.

Ndio wilaya inayoongoza kwa Ufaulu kwa matokeo ya shule za msingi na sekondari kwa miaka minne mfululizo.

Arusha inaongoza kwa kuwa na vyuo vya kimataifa vingi mf. Esami, TMA, na Nelson Mandela

Arusha pia ina hoteli 5 zenye hadhi ya kimataifa.

Ujenzi wa satellite cities ambazo zimepimwa kwa asilimia 100 mf. Safari City na Bondeni City.

Ujenzi wa mradi mkubwa wa maji unaotosheleza Arusha yote na maeneo ya jirani sambamba na ujenzi wa sewage system unaoufanya kuwa mji wa kwanza nchini kuunganishwa na sewage system mji mzima.

Usafiri wa haraka kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Arusha inahudumiwa na viwanja viwili vya ndege.

Arusha ndio mji wa pili kwa kuwa na largest foreign community nje ya Dar same as real estate licha ya kuwa na moderate population.

Kuzungukwa na kambi nyingi za Jeshi mf. Makuyuni, Ngaramtoni, Moshono, Oljoro na Duluti

Ufikaji wa urahisi Arusha kutoka kwenye miji mikubwa ya jirani mf. Nairobi, Mombasa, Dar es salaam na mji wetu mkuu Dodoma

Pia ni katikati ya Barabara ya mwanzo kabisa kuunganisha miji mikuu miwili ya utawala wa waingereza barani Afrika yaani Cape town na Cairo na kuwa na alama yake pale Clock tower jijini Arusha.

Uwepo wake karibu na vivutio bora zaidi vya utalii duniani ikiwemo mt. kilimanjaro, serengeti na ngorongoro

Bila kusahau leisure & conference facilities, shopping centers, office za kimataifa na hali ya hewa ya kustaajabisha inayoufanya mji huu kupokea asilimia 80 ya wageni wote wanaotembelea nchi yetu.

Zote hizi zimeshawishi uwepo wa ofisi kuu za mashirika na taasisi kubwa za ndani na nje ya nchi kama vile EAC, Mahakama ya Afrika, Papu, Tanapa n.k

Je, ni sahihi kusema Arusha ndio sehemu bora zaidi ya kuishi Tanzania.

Update: Arusha has been named by the CNN as one of the 10 most trending destinations in the world 2022. (Trip Advisor)

IMG_20211121_170157.jpg


IMG_20211125_103951.jpg


Screenshot_20211124-172702.png


IMG_20211121_170059.jpg


IMG_20211121_170219.jpg

.

IMG_20211213_201955.jpg


images.jpeg


Screenshot_20220429-115544.png
 
Ni miaka 10 tu imepita tangu mji huu maarufu kama Geneva of Africa utangazwe kuwa jiji.

Kutoka kuwa mji wa 9 kwa wingi wa watu hadi kuwa mji wa 3 kwa sensa ya mwaka 2012 na halmashauri ya jiji ya pili kwa wingi wa watu..lakini licha ya upya wake...
Ni kweli Arusha ni pazuri ila mimi kusema kweli palinikataa lile vumbi na baridi la pale! Hapana Dar ndo naona nikikaa nakaa vizuri!
 
Ni miaka 10 tu imepita tangu mji huu maarufu kama Geneva of Africa utangazwe kuwa jiji.

Kutoka kuwa mji wa 9 kwa wingi wa watu hadi kuwa mji wa 3 kwa sensa ya mwaka 2012 na halmashauri ya jiji ya pili kwa wingi wa watu..lakini licha ya upya wake...
Acheni kutafuta sifa. Jengeni barabara. Barabara za mitaa Arusha yote ni mbovu, za vumbi na matope hazipitiki wakati wa mvua. Kuna maeneo watu wameamua kutengeneza wenyewe barabara sababu ya ubinafsi wa viongozi wa jiji. Haieleweki ofisini hao wanaojiita maofisa wanafanya nini
 
Mimi nimefika Arusha ila sioni maajabu. Zaidi ya serikali kulazimisha kuufanya mji wa utalii na makao makuu ya EAC hakuna kingine kipya.

Soon inapitwa hata na Dodoma.

Nielekezeni basi niende wapi ila nijue kweli Arusha ni hatari.
 
Ni miaka 10 tu imepita tangu mji huu maarufu kama Geneva of Africa utangazwe kuwa jiji.

Kutoka kuwa mji wa 9 kwa wingi wa watu hadi kuwa mji wa 3 kwa sensa ya mwaka 2012 na halmashauri ya jiji ya pili kwa wingi wa watu..lakini licha ya upya wake...
Ukiondoa hali nzuri ya hewa, Arusha ni jiji la ovyo kabisa. Nyumba za ovyo zipo hadi ndani ya CBD, barabara ni nyembamba na hazina hadhi. Barabara nyingi hazina lami nenda makao mapya uone vumbi la ugoro. Arusha ndani ya miaka 60 ya uhuru inafaa kuitwa squalor of Africa
 
Sio kweli,mji huu bado upo nyuma sana, ingawa ulipaswa kuwa mbele kwani unaingizia serikali mapato makubwa kwa njia za utalii. Huu ni mji ambao makazi yake hayajapimwa na wala serikali haijawekeza kwenye mji huu bali kuchua kodi tu.

Wakati miji mingine iliruhusiwa kwenda bank kukopa kwa ajili ya upimaji wa viwanja mji huu na wa Moshi hawakuruhusiwa kukopa ili kupima na kuendeleza makazi yake.

Now concentration imeshift nguvu zote ni Mwanza na Musoma kuigeuza miji ya kitalii hili ni zuri ila Arusha serikali haijawekeza vya kutosha.
 
Back
Top Bottom