Sahihi 75 au G75, Je tuwaenzi vipi hawa WAZALENDO WA LEO

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
472
Zimepatikana Sahihi 75, hii inamaana ni wabunge 75 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi kasoro UPD vimeshiriki katika zoezi la kihistoria,

Je hawa wabunge 75 aka G75 tuwaenzi vipi, wanatuhitaji sana na kuna wengine ambao sasa wanapata tabu kutoka kwa viongozi wa vyama vyao kwa kushiriki zoezi hili, je G75 tunawaenzi vipi ili kuonyesha tuko pamoja nao.
 
Nimrod nae anahitaji kuenziwa?Hakuna cha G75 hiyo ni sehemu ya kazi yao na wako pale kwa ajili hiyo...............Baada ya miaka 50 ya Uhuru leo ndo wamejua majukumu yao kama wabunge..............Mi nafikiri swali liwe kwa wale ambao hawajapiga kura na walibwabwaja kujifanya wanamachungu na nchi
 
They Deserve mass respect and reward(kuwachagua tena 2015) for their Uzalendo!
 
Zimepatikana Sahihi 75, hii inamaana ni wabunge 75 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi kasoro UPD vimeshiriki katika zoezi la kihistoria,

Je hawa wabunge 75 aka G75 tuwaenzi vipi, wanatuhitaji sana na kuna wengine ambao sasa wanapata tabu kutoka kwa viongozi wa vyama vyao kwa kushiriki zoezi hili, je G75 tunawaenzi vipi ili kuonyesha tuko pamoja nao.

tuko nao pamoja ndio maana tuliwachagua na wanalipwa kodi zetu kwa kazi hiyo ya kusimamia serikali,
sasa wewe unataka kufanya kipi cha ziada kama unachakuwapa wape
 
They Deserve mass respect and reward(kuwachagua tena 2015) for their Uzalendo!
Hawa wamefanya tu stahili yao na hawahitaji reward ya ainna yoyote zaidi ya kusema wamefanya kazi tuliyoqatuma. Mawazo ya kuwapa ubunge ni mawazo ya JK ndivyo alivyoiua nchi
 
That is how it should be kutumikia wananchi wa Tanzania na siyo kutumika tumbo lako
 
Wale wa CCM waliosaini wapewe heshima katika harakati za Vyama vya Upinzani kwenye mikutano yao.
 
Yani wapewe reward kwa kutekeleza wajibu wao?
Ndo yale yale ya sitting allowance!!
 
Kiapo cha utumishi kinaelekea kueleweka kwa hatua hii, hatukuwatuma kukaa na kuzunguka kwenye viti kisha kuishia kuunga mkono. Hapa wameanza kuelewa kuwa sasa ni wakati wa kazi na sio kusinzia. Kimsingi hakuna cha ziada ila kuwataka waendelee kutenda wajibu wao. sisi nasi tutimize wajibu wetu.
 
zimepatikana sign 75 so what? hii kitu itakuja kuisha tu kitaratibu kama zingine na mawaziri na wabunge wote watapeta mpaka 2015 hamna kitu hapo, wabongo amkeni muone kua hakuna kitu kitu yote hiyo ni mchanga wa macho
 
kimsingi wametekeleza wajibu wao km wawakilishi wa wananchi so waungane pia kujibu hoja bunge lijalo wasimuachie zito pekee.
 
...kabla ya kufikiria tuwaenzi vipi,mi nadhani wao kwanza wafikiri kwa kina watafanya nini ili kufanikisha mpango huu wa kurudisha uwajibikaji.Kazi bado haijakamilika kwa hiyo si dhani kama ni wakati mzuri wa kuwatafuta zawadi ya kuwapa,cha kuwapa kwa sasa ni kuwatia moyo na kuwaunga mkono kwa hali na mali ktk mapambano haya.Wamethubutu,hii ni hatua ya kwanza lakini bado safari ni ndefu...
 
Anaeona anapata taabu kutoka kwa viongozi wake achukue uamuzi mgumu, Ajiuzulu ubunge na uanachama wa hicho chama kinachomsumbua alafu arudi jimboni kwake awaeleze wapiga kura wake kuwa anajiunga katika timu ya ukombozi, hapo ataongeza kura bungeni. wakifanya hivyo wengi wezi watakosa uhalali wa kuendelea kuiba raslimali za umma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom