Sahara Magharibi wajifunzeni kutoka Sudani Kusini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Sudani Kusini ndani ya Sudani ilikuwa na hadhi, raha na amani kuliko ilivyo sasa nje ya Sudani. Kutokana na mafuta yao Sudani Kusini ilidanganywa na wanyang'anyi ili wajitenge na Sudani ili waweze kujizolea mafuta yao, sasa hivi wanaitamani Sudan waliyoikimbia. Wanauana nchi yote inanuka damu kila kona. Sahara Magharibi nao wanachochewa na matapeli ili wajitenge na Morocco ili yapate urahisi wa kuyavabua mafuta yao kiulaini ambayo kwasasa wanashindwa kutia mkono kwasababu ya kuwa chini ya Morocco.

Believe me, kama Sahara ikijitenga watauana na kutamani tena kuungana na Morocco. AU ni ndumila kuwili, huku wanahimiza Afrika kuungana na hapohapo wanawachochea watu wajitenge.

Siungi mkono Sahara kujitenga, kama kuna matatizo ya kikatiba wakae wazungumze badala ya kutafuta Uhuru upya. Hata Palestine na Israel ingekuwa vizuri wangeungana na kutengeneza taifa moja kubwa na lenye nguvu lenye tamaduni mbalimbali badala ya kutafuta Palestine na Israel yawe mataifa mawili tofauti kwani kiasili Wayahud na wapelestina wana uhusiano wa karibu na undugu kwanini dunia inawachochea watengane badala ya kuungana na kuubakiza uhuru wao wa kuabudu palepale?
 
Wewe hujajua historia ya Sahara Magharibi, na nikuambie tu haifanani na ya Sudani Kusini.

Sahara Magharibi ilikua Nchi hapo kabla, kisha ikatwaliwa na Morroco pamoja na Mauritania. Sudani Kusini haikuwahi kua Nchi kamili hapo kabla. So wanachokidai Sahara Magharibi ni kilikuwepo kabla kikachukuliwa.

Pale ni Nchi moja inatawaliwa na Ingine, sio kwamba Morroco na Sahara ni nchi moja inayobidi kutenganishwa, la hasha.
 
Wewe hujajua historia ya Sahara Magharibi, na nikuambie tu haifanani na ya Sudani Kusini.

Sahara Magharibi ilikua Nchi hapo kabla, kisha ikatwaliwa na Morroco pamoja na Mauritania. Sudani Kusini haikuwahi kua Nchi kamili hapo kabla. So wanachokidai Sahara Magharibi ni kilikuwepo kabla kikachukuliwa.

Pale ni Nchi moja inatawaliwa na Ingine, sio kwamba Morroco na Sahara ni nchi moja inayobidi kutenganishwa, la hasha.
Mkuu umenifungua akili
 
Mkuu umenifungua akili
Muungano ni muungano bila kujali umepatikana vipi, iko miungano hapa duniani ambayo njia zilizotumika kupatikana kwao zinatia kinyaa kuzisikia, lakini umoja ni nguvu bila kujali historia yake, 80% ya Wasahara hawaijui Sahara yao huru hivyo wanaitaka Sahara ya nini? kinachotakiwa hapo ni kuangalia kama kuna usawa kati ya Morocco na Sahara? kama kuna shida kwenye mgawanyo wa mapato wakae tu chini waone watafanyeje kusawazisha. Hata muungano wa majimbo ya Marekani hayakupatikana kwa hiari na baadhi yake yana malalamiko yao hadi leo lakini hakuna anayewachochea wajitoe kwenye USA, Urusi, China, n.k hivyohivyo, why Sahara?
 
Back
Top Bottom