Sagrada Esperanca haooo kutua Dar kesho, Yanga yawasubiri

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
sagrada.jpg

KIKOSI cha wachezaji 22 wa Grupo Desportivo Sagrada Esperança ya Angola kinatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam kesho Alhamisi tayari kukabiliana na Yanga katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Taifa ambapo Yanga inahitaji ushindi mnono ili kuweka mazingira mazuri kabla ya kurudiana Mei 18 mjini Dundo.

Kwa habari zaidi kuhusu mpambano huo, soma hapa => Sagrada Esperanca haooo kutua Dar kesho, Yanga yawasubiri | Fikra Pevu
 
Chonde chonde baadhi ya mashabiki wachache wa simba msijitoe ufahamu safari hii mkachukua uraia wa Angola!
 
hawa sagrada ndio wanavaa jezi za kijani.sasa sijui wamatopen watavaa hzo jez za kijan km kawaida yao ya kuvaa na kushangilia timu pinzan na wakimataifa,?
 
Mimi huwa sielewi kwanini mala nyingi lazima timu ngeni zianzie nyumbani kwa timu za Tz sio njia ya kuzibeba kisha timu zetu zifell tunapoenda kwao.
 
Mimi huwa sielewi kwanini mala nyingi lazima timu ngeni zianzie nyumbani kwa timu za Tz sio njia ya kuzibeba kisha timu zetu zifell tunapoenda kwao.

Huo ndio utaratibu wa FIFA wanaangalia viwango vya Soka so wewe dhaifu match zitaanzia kwako na utamalizia kwa mwenye kiwango cha juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom